Kijana afariki dunia mgodini Mara

Kijana afariki dunia mgodini Mara

Boran Jakutay

Senior Member
Joined
Apr 8, 2023
Posts
110
Reaction score
259
MARA: Kijana aliyefahamika kwa jina la Masasa Tungulilo, amefariki dunia kwa kuangukiwa na kifusi katika machimbo ya mgodi mdogo wa dhahabu wa Nyarufu uliopo Halmashauri ya Musoma mkoani Mara wakati akijaribu kuingia katika mduara huo.

Mashuhuda wa tukio hilo ambao ni wachimbaji wadogo katika mgodi huo, wamesema kifo cha kijana huyo kimetokana na muhusika kutochukua tahadhari zilizowekwa wakati akifanya kazi.

Mgesa Kaini Magesa ambaye ni Mwenyekiti wa Kitongoji cha Nyarufu, amesema marehemu aliporomoka na kujigonga katika miamba iliyopo mgodini hapo hali iliyosababisha kifo chake.

Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Mara, Augustine Magere, amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kusema kwamba, wamefanikiwa kuutoa mwili wa marehemu kwa kushirikiana na wachimbaji wadogo wa dhahabu mgodini hapo huku akitoa rai kwa wachimbaji hao kuchukua tahadhari na kufuata miongozo iliyopo.
 
Back
Top Bottom