Kijana ahukumiwa miezi 6 jela kwa kuva sare za JWTZ ili kumshawishi mchumba wake kuwa yeye ni Askari

Kijana ahukumiwa miezi 6 jela kwa kuva sare za JWTZ ili kumshawishi mchumba wake kuwa yeye ni Askari

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Tunaposema vijana muwe makini na mapenzi hii ndio maana yake

=================================================

Mahakama ya Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza imemhukumu kifungo cha miezi sita Rajabu Reli (22), mkazi wa Sengerema baada ya kukutwa na hatia ya kuvaa sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) bila ruhusa.

Hukumu hiyo imetolewa jana Januari 07, 2025 katika shauri la jinai namba 445 la mwaka 2025 na Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo Mhe. Evodius Kisoka mbele ya mwendesha mashtaka wa Serikali Nyamhanga Tissoro.

Mshtakiwa alitenda kosa hilo mnamo Desemba 5, 2024 huko kijiji cha Kasisa, Wilaya ya Sengerema kinyume na kifungu cha 178 (1) cha sheria ya kanuni ya Adhabu sura ya 16 marejeo ya mwaka 2022.

Mshtakiwa alifikishwa mahakamani Januari 7, 2025 na kusomewa shitaka la kuvaa sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania bila ruhusa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo baada ya kusikiliza pande zote za ushahidi hakimu Evodius Kisoka alijiridhisha kuwa ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri ni mzito na haukuacha shaka lolote.

Aidha mshtakiwa huyo alipopewa nafasi ya kujitetetea kwa nini asipewe adhabu; aliomba mahakama hiyo imuachie huru kwa kuwa ni mkosaji wa mara ya kwanza na alivaa ili akubaliwe na mchumba wake.

"Mhe. Hakimu naomba nisamehewe kwa kuwa ni kosa la kwanza na nilivaa na kwenda kumuonesha mchumba wangu kuwa mimi ni Askari ili asinikatae," aliomba Rajabu.

Ombi hilo lilitupiliwa mbali na Hakimu Kisoka na kutoa hukumu hiyo ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama ya Rajabu.

sare jwtz.png

Source: Manara TV
 
#HABARI: Mahakama ya Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza imemhukumu kifungo cha miezi sita Rajabu Reli (22), mkazi wa Sengerema baada ya kukutwa na hatia ya kuvaa sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) bila ruhusa.

Hukumu hiyo imetolewa jana Januari 07, 2025 katika shauri la jinai namba 445 la mwaka 2025 na Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo Mhe. Evodius Kisoka mbele ya mwendesha mashtaka wa Serikali Nyamhanga Tissoro.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka iliyosomwa na mwendesha mashtaka wa Serikali Nyamhanga Tissoro mbele ya hakimu Evodius Kisoka, mshtakiwa alitenda kosa hilo mnamo tarehe 05.12.2024 huko kijiji cha Kasisa, Wilaya ya Sengerema kinyume na kifungu cha 178(1) cha sheria ya kanuni ya Adhabu sura ya 16 marejeo ya mwaka 2022.

Mshtakiwa alifikishwa mahakamani Januari 07.2025 na kusomewa shitaka la kuvaa sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania bila ruhusa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Baada ya kusikiliza pande zote za ushahidi hakimu Evodius Kisoka alijiridhisha kuwa ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri ni mzito na haukuacha shaka lolote.

Hata hivyo, mshtakiwa alipopewa nafasi ya kujitetetea kwa nini asipewe adhabu; aliomba mahakama hiyo imuachie huru kwa kuwa ni mkosaji wa mara ya kwanza na alivaa ili akubaliwe na mchumba wake.

"Mhe. Hakimu naomba nisamehewe kwa kuwa ni kosa la kwanza na nilivaa na kwenda kumuonesha mchumba wangu kuwa mimi ni Askari ili asinikatae," aliomba Rajabu.

Ombi hilo lilitupiliwa mbali na Hakimu Kisoka na kutoa hukumu hiyo ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama ya Rajabu.
 
Attachments

  • 1736335904159.jpg
    1736335904159.jpg
    266.7 KB · Views: 5

Alipata wapi?
 
Habari za bongo huwa hazikamiliki ndio maana waandishi wanakandiwa kila leo
Sasa hizo sare kapewa na nani maana mpaka crown kwenye kofia
Labda sijaelewa maandishi
 
Bora angefanya kama Mimi nilikuwaga najifanya mwalimu wa shule ya msingi ( enzi hizo ualimu dili)so nilikuwa nawaandikia barua kwa kutumia kalamu nyekundu ( kalamu ya kusahihishia) ili wajue Mimi mwalimu kweli.

Niliwatafuna ile laana.

Kuna mmoja alinikubali kinomanoma alisoma shule ya EM msingi alikuwa anaitwa Joannah
 
Niliwahi kutana na mrembo Fulani mkoa Fulani hapendi wanajeshi akadai anahofia sare za jeshi ( baka baka).

Sasa huyu bwa'mdogo anaenda kutongozea kabisa vitenge vya watu! Duhh
 
Wapewe ajira yeye na mpenzi wake ili tatizo liishe.

Maana jamaa akitoka huko jela anaweza jinyonga baada ya kukataliwa kwakuwa sio askari.
 
Mahakama ya Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza imemhukumu kifungo cha miezi sita jela Rajabu Reli (22), mkazi wa Sengerema baada ya kukutwa na hatia ya kuvaa sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) bila ruhusa.

Hukumu hiyo imetolewa Januari 7, 2025 katika shauri la jinai namba 445 la mwaka 2025 na Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Evodius Kisoka mbele ya mwendesha mashtaka wa serikali, Nyamhanga Tissoro.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka iliyosomwa na Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Nyamhanga Tissoro mbele ya hakimu Evodius Kisoka, mshtakiwa alitenda kosa hilo Desemba 5, 2024 katika Kijiji cha Kasisa, Wilaya ya Sengerema kinyume na kifungu cha 178(1) cha sheria ya Kanuni ya Adhabu sura ya 16 marejeo ya mwaka 2022.

Mshtakiwa alifikishwa mahakamani Januari 7, 2025 na kusomewa shitaka la kuvaa sare za Jeshi la wananchi wa Tanzania bila ruhusa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
"Mhe. Hakimu naomba nisamehewe kwa kuwa ni kosa la kwanza na nilivaa na kwenda kumuonesha mchumba wangu kuwa mimi ni Askari ili asinikatae," aliomba Rajabu.
Aliyesema
Elimu
Elimu
Elimu
Hakukosea

Aliyemkopesha sare amehukumiwaje
 
  • Rajabu Reli amehukumiwa miezi sita jela kwa kosa la kuvaa sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania, huku akijitetea kuwa alivaa kumuaminisha mchumba wake yeye ni askari ili asimkatae.
Alivyopewa muda wa kujitetea
''Mhe Hakimu naomba nisamehewe kwa kuwa ni kosa la kwanza na nilivaa na kwenda kumuonyeshha mchumba wangu kuwa mimi ni askari ili asinikatae,'' aliomba Rajabu.

Hata hivyo,ombi lake lilitupiliwa mbali na Hakaimu Kisoka na kumhukumu miezi sita jeala ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama yake.

Hakimu alisema mwenye mamlaka ya kumruhusu mtu kuvaa sare ya Jeshi ni Amiri jeshi mkuu peke yake ambaye ndio raisi wa Tanzania.

Source Mwananchi Jumatano, Januari 08, 2025

Mawazo yangu
hii ingefaa iwe Valentine day yetu watanzania na waafrika tungeiita Rajabu day sio jambo la mchezo mtu kuvaa sare za jeshi ajili ya mpenzi wake.
Tunaiga mambo ya wazungu siku ya tarehe 14 feb kila mwaka kusherehekea siku hiyo.Tatizo kila kitu na baadhi ya tamaduni tunaona za mtu mweupe ndio za maana.
 
Attachments

  • Rajabu.png
    Rajabu.png
    234.7 KB · Views: 6
Back
Top Bottom