Yaani iwe kila ifikapo tarehe 5 Desemba au siyo?🤣Alivyopewa muda wa kujitetea
- Rajabu Reli amehukumiwa miezi sita jela kwa kosa la kuvaa sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania, huku akijitetea kuwa alivaa kumuaminisha mchumba wake yeye ni askari ili asimkatae.
''Mhe Hakimu naomba nisamehewe kwa kuwa ni kosa la kwanza na nilivaa na kwenda kumuonyeshha mchumba wangu kuwa mimi ni askari ili asinikatae,'' aliomba Rajabu.
Hata hivyo,ombi lake lilitupiliwa mbali na Hakaimu Kisoka na kumhukumu miezi sita jeala ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama yake.
Hakimu alisema mwenye mamlaka ya kumruhusu mtu kuvaa sare ya Jeshi ni Amiri jeshi mkuu peke yake ambaye ndio raisi wa Tanzania.
Source Mwananchi Jumatano, Januari 08, 2025
Mawazo yangu
hii ingefaa iwe Valentine day yetu watanzania na waafrika tungeiita Rajabu day sio jambo la mchezo mtu kuvaa sare za jeshi ajili ya mpenzi wake.
Tunaiga mambo ya wazungu siku ya tarehe 14 feb kila mwaka kusherehekea siku hiyo.Tatizo kila kitu na baadhi ya tamaduni tunaona za mtu mweupe ndio za maana.
ndio mkuu hii haijawahi kutokea hata huyo mwanamke amkubali tu.Yaani iwe kila ifikapo tarehe 5 Desemba au siyo?🤣
Wewe ni mwanajeshi?Alizitoa wapi nguo hizo. So Kama nimechukua za bro wangu mjeda nikavaa ndani kwa ndani mie Nina makosa
Usipost vaa uko uko usipost utaumiaAlizitoa wapi nguo hizo. So Kama nimechukua za bro wangu mjeda nikavaa ndani kwa ndani mie Nina makosa
Wewe utakuwa tayari kuadhimisha siku ambayo tapeli (kama unavyomchukulia wewe kutokana na muonekano wa sura yake) alitenda kosa?ndio mkuu hii haijawahi kutokea hata huyo mwanamke amkubali tu.
ila tatizo sura imekaa kitapeli
Hivi huwaga hakuna hukumu ya kutumikia jamii hadi mtu afungwe tu?#HABARI: Mahakama ya Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza imemhukumu kifungo cha miezi sita Rajabu Reli (22), mkazi wa Sengerema baada ya kukutwa na hatia ya kuvaa sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) bila ruhusa.
Hukumu hiyo imetolewa jana Januari 07, 2025 katika shauri la jinai namba 445 la mwaka 2025 na Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo Mhe. Evodius Kisoka mbele ya mwendesha mashtaka wa Serikali Nyamhanga Tissoro.
Kwa mujibu wa hati ya mashtaka iliyosomwa na mwendesha mashtaka wa Serikali Nyamhanga Tissoro mbele ya hakimu Evodius Kisoka, mshtakiwa alitenda kosa hilo mnamo tarehe 05.12.2024 huko kijiji cha Kasisa, Wilaya ya Sengerema kinyume na kifungu cha 178(1) cha sheria ya kanuni ya Adhabu sura ya 16 marejeo ya mwaka 2022.
Mshtakiwa alifikishwa mahakamani Januari 07.2025 na kusomewa shitaka la kuvaa sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania bila ruhusa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Baada ya kusikiliza pande zote za ushahidi hakimu Evodius Kisoka alijiridhisha kuwa ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri ni mzito na haukuacha shaka lolote.
Hata hivyo, mshtakiwa alipopewa nafasi ya kujitetetea kwa nini asipewe adhabu; aliomba mahakama hiyo imuachie huru kwa kuwa ni mkosaji wa mara ya kwanza na alivaa ili akubaliwe na mchumba wake.
"Mhe. Hakimu naomba nisamehewe kwa kuwa ni kosa la kwanza na nilivaa na kwenda kumuonesha mchumba wangu kuwa mimi ni Askari ili asinikatae," aliomba Rajabu.
Ombi hilo lilitupiliwa mbali na Hakimu Kisoka na kutoa hukumu hiyo ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama ya Rajabu.
Uhalifu wa kutaka kupata K kirahisiHivi huwaga hakuna hukumu ya kutumikia jamii hadi mtu afungwe tu?
Hiloni kosa dogo sana kumfunga huyo kijana bhana.
Mahakimu nao nadhani wana stress zao.
Angelikuwa kakamatwa kwenye tukio la uhalifu hapo sawa.
🤣🤣😜Uhalifu wa kutaka kupata K kirahisi
Anatafuta Ubumbu kwa jeziUhalifu wa kutaka kupata K kirahisi