Kijana ajifunze lugha ipi kupanua goli la ajira na fursa?

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
N.B: HADI NAFIKA HAPA NIMEONA KUNA PONGEZI NYINGIZAIDI YA MALALAMIKO KWA WALIOFANYA KAZI KWA WAZUNGU, KWA WENZETU WAHINDI, WACHINA, N.K HUKO KUNA MALALAMIKO MENGI KUZIDI PONGEZI, HIVYO NAOMBA USHAURI UWE UMELENGA LUGHA ZA ULAYA.

Habari zenu wakuu, Nina kijana kamaliza form 6 mtoto wa shangazi yupo hapa home, Dogo anaenda kusomea accounting / Uhasibu., Kama mnavyojua hii fani ipo na wahitimu wengi mno, Nikaona ni heri aanze kupanua goli kwa kujifuza lugha ya ziada

Lengo nataka hata akikosa ajira.

- ajaribu huko kwenye Ma NGO ya ujerumani, Ufaransa, Italy, Sweeden, wadachi, n.k
-awe anafanya kazi online za watu wa nchi wanaoongea lugha husika (mfano anafanyia watu book keeping online
- kwenda kuishi katika nchi anayongea lugha husika na kuanza maisha huko huku akiwa sio mgeni wa lugha

Kwa hali ya sasa kiukweli kama mnavyoona ajira zimekuwa ni ishu, Hata kufaulu form 6 siku hizi ni kama kunywa maji tu, wanaoenda vyuoni ni wengi mno, na wahitimu ni wengi mno, hivyo inabidi walau utie japo ubunifu wa kukufanya uwe unique kidogo ili kupanua goli la kutusua.

Kijana nimemshauri ajifunze lugha mpya awe unique kidogo, hiki kiingereza kiukweli japo huku kinatupa shida, siku hizi hakina dili sana linapokuja swala la fursa, Ni lugha ambayo karibu kila mtu alieelimika anaijua japo kwa kbangaiza 😂 na hata majirani zetu Kenya, Uganda, Zambia, n.k ni lugha zao rasmi.

Kigezo kimojawapo nachodhani kina uzito kwa sasa ni kujua hizi lugha za wamiliki wa makampuni haya ya NGO ya wazungu, mfano ukijua kijrumani, kidachi, ki italiano, kifaransa, n.k basi hapo huenda Tanzania nzima mkawa hamfiki hata kumi, hapo kidogo unajiongeza points,

Sasa nauliza hivi makampuni mengi haya ya NGO hasa ya azungu huwa yanakuaga ni ya nchi zipi??

Nina imani huenda akijifunza hizo lugha za hao wenye makampuni ya NGO, Huenda llabda itampuongezea wigo mpana wa kupata fursa.

Naombeni ushauri wa ziada pia
 
Afadhali kidogo kichina kinaweza kumpatia ajira moja kwa moja kwa sababu wanaojua ni wachache sana na ajira zake huwa ni za fasta hazina milolongo.
Hizo lugha nyingine ni upotevu tu wa pesa,unaweza kuzijua hizo lugha unazosema zinatumiwa na NGOs na interviews huitwi itakuwa haijakusaidia kitu.
Lakini kichina ukikijua hakunaga maswala ya interview ukiitwa wakikuona unajua ni kwenda site tu muda huo huo.
 
N.B: LUGHA ZIWE ZA ULAYA.... HADI NAFIKA HAPA NIMEONA WENGI WAKINUFAIKA KUFANYA KAZI KWA WAZUNGU BILA MATESO WALA KUPUNWA, KWA WENZETU WAHINDI, WACHINA, N.K HUKO KUNA VISKENDO KADHAA VYA WAFANYA KAZI KUNYANYASWA.
 
Aiseeh!!!kichina!!!!Mbona kigum sana!kuongelea puani si kitoto kabisa!!!
Ni sababu moja wapo nimetilia msisitizo lugha kama kichina, kihindi, kiarabu, n.k ziwekwe pembeni, kwanza zina ugumu yani inabidi uanze kujifunza herufi upya, na pia waajiri hawa kina kanjibahi na wachina, kufanya ajira kwao sometimes ni manyanyaso,
 
Kwanza mwambie aje kanda ya ziwa... Pili awe na mtaji, tatu kuhusu lugha ajifunze kisukuma, kwani ndio lugha ya biashara... Akikomaa na hayo mambo matatu katoboa tayari!
 
N.B: LUGHA ZIWE ZA ULAYA.... HADI NAFIKA HAPA NIMEONA WENGI WAKINUFAIKA KUFANYA KAZI KWA WAZUNGU BILA MATESO WALA KUPUNWA, KWA WENZETU WAHINDI, WACHINA, N.K HUKO KUNA VISKENDO KADHAA VYA WAFANYA KAZI KUNYANYASWA.
MKUU KATIKA HII MADA YAKO ILI USHAURIKE VIZURI UNGEONGEZEA NYAMA KIDOGO YAANI KWA MFANO AKIFIKA CHUO ATASOMEA FANI GANI?AU UNATAKA AKISOMA LUGHA TU NDIO ATATOBOA BILA KUWA NA TAALUMA MAALUMU?MAANA LUGHA PEKE YAKE SI KITU
 
Kwanza mwambie aje kanda ya ziwa... Pili awe na mtaji, tatu kuhusu lugha ajifunze kisukuma, kwani ndio lugha ya biashara... Akikomaa na hayo mambo matatu katoboa tayari!
Nkoi! Jogori akomana kinehe
 
MKUU KATIKA HII MADA YAKO ILI USHAURIKE VIZURI UNGEONGEZEA NYAMA KIDOGO YAANI KWA MFANO AKIFIKA CHUO ATASOMEA FANI GANI?AU UNATAKA AKISOMA LUGHA TU NDIO ATATOBOA BILA KUWA NA TAALUMA MAALUMU?MAANA LUGHA PEKE YAKE SI KITU
Dogo anaenda kusomea accounting / Uhasibu.

Kama mnavyojua hii fani ipo na wahitimu wengi mno, Nikaona ni heri aanze kupanua goli kwa kujifuza lugha ya ziada

Lengo nataka hata akikosa ajira.

- ajaribu huko kwenye Ma NGO ya ujerumani, Ufaransa, Italy, Sweeden, wadachi, n.k
-awe anafanya kazi online za watu wa nchi wanaoongea lugha husika (mfano anafanyia watu book keeping online
- kwenda kuishi katika nchi anayongea lugha husika na kuanza maisha huko huku akiwa sio mgeni wa lugha
 
Dogo anaenda kusomea accounting / Uhasibu.

Kama mnavyojua hii fani ipo na wahitimu wengi mno, Nikaona ni heri aanze kupanua goli kwa kujifuza lugha ya ziada

Lengo nataka hata akikosa ajira.

- ajaribu huko kwenye Ma NGO ya ujerumani, Ufaransa, Italy, Sweeden, wadachi, n.k
-awe anafanya kazi online za watu wa nchi wanaoongea lugha husika (mfano anafanyia watu book keeping online
- kwenda kuishi katika nchi anayongea lugha husika na kuanza maisha huko huku akiwa sio mgeni wa lugha
Hiyo fani uliyotaja haina uhusiano wowote na kujua lugha.
Ungeniambia anasomea tourism au mass communication hapo kidogo ingekuwa inamake sense.
Lakini kwa vile uko na pesa na unatafuta matumizi sitaki kukuvunja moyo.
 
Lugha ni bonasi kubwa sana... hasa hasa kwa mashirika ya kimataifa. Ukijua lugha za ziada uta interact na sehemu ya ziada ya dunia;Sio kila mtu aanaongea kiingereza
 
Ivi bado tu tunawaza utumwa baada ya kutafuta nyia za kutafuta ukipato nje ya utumwa wa ajira ! But ndo wasomi wa kitanzania na africa yani uanze tena kusoma lugha baada ya kutatua changamoto za jamii na kuoata pesa. Ukitatua changamoto za jamii utapata pesa tuache uvivu wa kuaminishana kwenye mitandao ya kijamii kuwa Maisha rahisi kiivyo Maisha sio lahisi jamani lazima ujitoe sana .ni mtazamo wangu tu mimi sio lazima ukubaliane nao
 
N.B: HADI NAFIKA HAPA NIMEONA KUNA PONGEZI NYINGIZAIDI YA MALALAMIKO KWA WALIOFANYA KAZI KWA WAZUNGU, KWA WENZETU WAHINDI, WACHINA, N.K HUKO KUNA MALALAMIKO MENGI KUZIDI PONGEZI, HIVYO NAOMBA USHAURI UWE UMELENGA LUGHA ZA ULAYA.

Habari zenu wakuu, Nina kijana kamaliza form 6 mtoto wa shangazi yupo hapa home, Dogo anaenda kusomea accounting / Uhasibu., Kama mnavyojua hii fani ipo na wahitimu wengi mno, Nikaona ni heri aanze kupanua goli kwa kujifuza lugha ya ziada

Lengo nataka hata akikosa ajira.

- ajaribu huko kwenye Ma NGO ya ujerumani, Ufaransa, Italy, Sweeden, wadachi, n.k
-awe anafanya kazi online za watu wa nchi wanaoongea lugha husika (mfano anafanyia watu book keeping online
- kwenda kuishi katika nchi anayongea lugha husika na kuanza maisha huko huku akiwa sio mgeni wa lugha

Kwa hali ya sasa kiukweli kama mnavyoona ajira zimekuwa ni ishu, Hata kufaulu form 6 siku hizi ni kama kunywa maji tu, wanaoenda vyuoni ni wengi mno, na wahitimu ni wengi mno, hivyo inabidi walau utie japo ubunifu wa kukufanya uwe unique kidogo ili kupanua goli la kutusua.

Kijana nimemshauri ajifunze lugha mpya awe unique kidogo, hiki kiingereza kiukweli japo huku kinatupa shida, siku hizi hakina dili sana linapokuja swala la fursa, Ni lugha ambayo karibu kila mtu alieelimika anaijua japo kwa kbangaiza [emoji23] na hata majirani zetu Kenya, Uganda, Zambia, n.k ni lugha zao rasmi.

Kigezo kimojawapo nachodhani kina uzito kwa sasa ni kujua hizi lugha za wamiliki wa makampuni haya ya NGO ya wazungu, mfano ukijua kijrumani, kidachi, ki italiano, kifaransa, n.k basi hapo huenda Tanzania nzima mkawa hamfiki hata kumi, hapo kidogo unajiongeza points,

Sasa nauliza hivi makampuni mengi haya ya NGO hasa ya azungu huwa yanakuaga ni ya nchi zipi??

Nina imani huenda akijifunza hizo lugha za hao wenye makampuni ya NGO, Huenda llabda itampuongezea wigo mpana wa kupata fursa.

Naombeni ushauri wa ziada pia
Kiarabu,kichina au kituruki

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom