Kijana ajifunze lugha ipi kupanua goli la ajira na fursa?

Kijana ajifunze lugha ipi kupanua goli la ajira na fursa?

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
N.B: HADI NAFIKA HAPA NIMEONA KUNA PONGEZI NYINGIZAIDI YA MALALAMIKO KWA WALIOFANYA KAZI KWA WAZUNGU, KWA WENZETU WAHINDI, WACHINA, N.K HUKO KUNA MALALAMIKO MENGI KUZIDI PONGEZI, HIVYO NAOMBA USHAURI UWE UMELENGA LUGHA ZA ULAYA.

Habari zenu wakuu, Nina kijana kamaliza form 6 mtoto wa shangazi yupo hapa home, Dogo anaenda kusomea accounting / Uhasibu., Kama mnavyojua hii fani ipo na wahitimu wengi mno, Nikaona ni heri aanze kupanua goli kwa kujifuza lugha ya ziada

Lengo nataka hata akikosa ajira.

- ajaribu huko kwenye Ma NGO ya ujerumani, Ufaransa, Italy, Sweeden, wadachi, n.k
-awe anafanya kazi online za watu wa nchi wanaoongea lugha husika (mfano anafanyia watu book keeping online
- kwenda kuishi katika nchi anayongea lugha husika na kuanza maisha huko huku akiwa sio mgeni wa lugha

Kwa hali ya sasa kiukweli kama mnavyoona ajira zimekuwa ni ishu, Hata kufaulu form 6 siku hizi ni kama kunywa maji tu, wanaoenda vyuoni ni wengi mno, na wahitimu ni wengi mno, hivyo inabidi walau utie japo ubunifu wa kukufanya uwe unique kidogo ili kupanua goli la kutusua.

Kijana nimemshauri ajifunze lugha mpya awe unique kidogo, hiki kiingereza kiukweli japo huku kinatupa shida, siku hizi hakina dili sana linapokuja swala la fursa, Ni lugha ambayo karibu kila mtu alieelimika anaijua japo kwa kbangaiza 😂 na hata majirani zetu Kenya, Uganda, Zambia, n.k ni lugha zao rasmi.

Kigezo kimojawapo nachodhani kina uzito kwa sasa ni kujua hizi lugha za wamiliki wa makampuni haya ya NGO ya wazungu, mfano ukijua kijrumani, kidachi, ki italiano, kifaransa, n.k basi hapo huenda Tanzania nzima mkawa hamfiki hata kumi, hapo kidogo unajiongeza points,

Sasa nauliza hivi makampuni mengi haya ya NGO hasa ya azungu huwa yanakuaga ni ya nchi zipi??

Nina imani huenda akijifunza hizo lugha za hao wenye makampuni ya NGO, Huenda llabda itampuongezea wigo mpana wa kupata fursa.

Naombeni ushauri wa ziada pia
 
Unataka akaifanyie nini hiyo lugha huko? Lengo haswa ni nini?
 
Sio kila mara lugha itakusaidia kwenye ajira, kwa mfano kampuni ya kichina inahitaji HR, kama wewe umesomea udaktari na unajua kichina, hawatakuhitaji
 
Unataka akaifanyie nini hiyo lugha huko? Lengo haswa ni nini?
Kuna vitu mkuu kama kufanya kazi online, hizi kazi za kiingereza huko mitandaoni unakuta mmarekani anataka aingiziwe data kwenye excel au atengenezewe website ama atengenezewe bango, basi hapo inakuwa ni vita, wahindi, wafilipino, wakenya, wanaijeria, waganda, waarabu, n.k wote wanapambania kazi hapo na wengine wanashuka dau kabisa, si kila mtu anajua kiingereza 😀 😀 na hii ni hivi hivi hata hapa hapa tz, ni nani asiejua hata kiingereza cha kuandika cv 😀😀

Ni kujiongezea wigo mkuu, just imagine NGO ya nchi flani ipo hapa bongo, mfano ni ya raia wa denmark huko, alafu mbongo anajua ki denmark, Hapo atakuwa na ka uzito flani ivi, au mnasemaje jamani??
 
Sio kila mara lugha itakusaidia kwenye ajira, kwa mfano kampuni ya kichina inahitaji HR, kama wewe umesomea udaktari na unajua kichina, hawatakuhitaji
Dogo anaenda kusomea accounting mkuu,

Hii kzi ipo na graduates shazi,

Lengo nataka hata akikosa hajira za serikalini basi ajaribu huko kwenye Ma NGO, awe anafanya kazi online za watu wa nchi wanoongea lugha husika (mfano anafanyia watu book keeping online) ama kuzamia katika nchi anayongea lugha husika
 
Kuna vitu mkuu kama kufanya kazi online, hizi kazi za kiingereza huko mitandaoni unakuta mmarekani anataka aingiziwe data kwenye excel au atengenezewe website ama atengenezewe bango, basi hapo inakuwa ni vita, wahindi, wafilipino, wakenya, wanaijeria, waganda, waarabu, n.k wote wanapambania kazi hapo na wengine wanashuka dau kabisa, si kila mtu anajua kiingereza 😀 😀 na hii ni hivi hivi hata hapa hapa tz, ni nani asiejua hata kiingereza cha kuandika cv 😀😀

Ni kujiongezea wigo mkuu, just imagine NGO ya nchi flani ipo hapa bongo, mfano ni ya raia wa denmark huko, alafu mbongo anajua ki denmark, Hapo atakuwa na ka uzito flani ivi, au mnasemaje jamani??
Tunaita pata-potea
Hakuna replacement ya Ujuzi!
 
Lugha ni bonasi kubwa sana... hasa hasa kwa mashirika ya kimataifa. Ukijua Kiingereza na Kifaransa utaongea na sehemu kubwa sana ya dunia; ukiachana na Wachina.
 
Back
Top Bottom