Mwamuzi wa Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 15,486
- 45,256
Nimefuatilia mazungumzo ya vijana kadhaa waliomaliza mikataba yao ya JKT miaka 2 na wengine kuongezewa miaka au miezi kisha kurudi nyumbani bila ajira. Wengi wao akili zao zinakuwa na walakini utadhani watu wanaotafuta Rupia ya Mjerumani mapangoni na milimani.
Unaweza ukamuuliza swali moja akakujibu na maswali usiyomuuliza. Anakaa anasubiri nafasi za jeshi anasahau kuwa makambini nako kuna vijana wenzake ambao ni wabichi zaidi yake. Nilimsikia mmoja leo ananiuliza kuna nafasi za polisi, uhamiaji, fire na zimamoto zimetoka umeziona?
Nikamjibu hakuna nafasi, anasema zipo zitatangazwa mUda wowote nazisubiri. Nilimuonea huruma sana.
Mwingine akisikia Mh. Rais anahutubia tu anasikiliza huenda Rais atatoa tamko Op. Magufuli wote waajiriwe.
Hebu serikali ibadili mfumo wa JKT, kwakweli vijana hawaendi kule kujitolea bali wanakwenda kusaka ajira ndio maana kule humkuti mtoto wa kigogo na ukimkuta huyo harudi nyumbani baada ya kujitolea.
Vijana wanaorudi wengi akili zinafyatuka kidogo na kimbilio lao ni kwenye makampuni ya ulinzi ikiwemo SUMA JKT GUARD ambako hawapati fedha ya kukidhi mahitaji yao.
Thanks.