affinitytz
JF-Expert Member
- Feb 10, 2020
- 280
- 1,151
Mwaka jana mwezi March, kabla ya utaratibu mpya wa kuomba Visa kwenye ubalozi wa China hapo jijini Dar es Salaam.
Nikiwa nimeshajaza fomu zangu na nikiwa nimeshapewa notification ya appointment na kuwasilisha fomu ya maombi ya VISA pamoja na viambatanishi vingine nikafika ubalozi wa China, mapema asubuhi.
Nikakaa pale kwenye sehemu ya kuingilia kwenda ofisi za watu wa VISA; baada ya muda mlinzi akatwambia tuingie kwa makundi.
Kwenye foleni mbele yangu kulikuwa na kijana mmoja na tulikuwa tukiongea mambo kadhaa kuanzia biashara mpaka mambo mengine ya maisha. Alionekana kuwa na focus na maisha na nikajisemea kuwa nchi yetu inahitaji vijana kama hawa.
Ikafika zamu yetu tukaingia pale ndani kwenye kile kighorofa, kwenye foleni akatangulia kuwasilisha fomu zake.
Dada wa kichina akapokea fomu; akaanza kukagua kidogo, baada ya muda anamrudishia yule kijana fomu zake na mazungumzo yanaanza. Walianza kuongea kwa taratibu lakini baadaye nikaona sauti zinapanda, hii ikavuta usikivu wangu; nikasikia dada wa Kichina anasema ''i cant not accept your application because the government has declined'' hapo sasa akainua mikono akiashiria nisogee dirishani huku akimtaka huyu kijana atoke hapo dirishani.
Nikasogea lakini sasa kijana hataki kutoka pale kwenye kidirisha; dada wa kichina akaita yule mtanzania mwenzetu mwenye panki ambaye ni mfanyakazi pale na kumwambia ''toa hii haraka''. Jamaa akamshika mkono na kumsogeza pembeni.
Nikawasilisha fomu zangu na dada akapitia fomu na passport na kuzichukua huku akinipa zile fomu za benki ya NMB kwa ajili ya kwenda kulipa na kuniambia tarehe ya kurudi kuchukua VISA.
Nilipokuwa natoka nikakutana na huyu kijana pale parking, ikabidi nimuulize mtanzania mwennzangu tatizo nini mpaka serikali ya Xi Jinping haitaki aingie China?
Kijana akiwa analengwalengwa na machozi akasema kuna tukio lilitokea Guangzhou mwaka 2024 akiwa amefuata mzigo aligombana na mchina hivyo inaonekana aliripotiwa kwenye mamlaka.
Sikutaka kujua sana nikampa pole na mimi kuendelea na mihangaiko yangu ya kujitafutia ridhiki.
Pia soma ~ Wizara: Ubalozi wa China umesema hakuna vikwazo vya kisera kwa Watanzania wanaoomba visa za China