Kijana aunguzwa kwa uji baada ya kodokoa maharage

DreezyD98

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2020
Posts
1,610
Reaction score
2,874
Kijana Elvis Shoo (27) mkazi wa kitongoji cha Bogini Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, amelazwa katika kituo cha Afya Pasua akiuguza majeraha ya moto, yaliyotokana na kuunguzwa kwa uji na shangazi yake akidaiwa kuiba maharage jikoni.

Tukio hilo ambalo linadaiwa kutokea Septemba 30 mwaka huu mchana nyumbani kwa bibi yake eneo la Bogini, linadaiwa kusababishwa na mzozo uliotokana na kijana huyo kuchukua maharage bila idhini ya shangazi yake.

Uji huo ulimuunguza kijana huyo na kumsababishia majeraha sehemu za shingoni kuelea kifuani na kulazwa hospitalini ambako anaendelea na matibabu mpaka sasa.

======
Kijana Elvis Shoo (27) mkazi wa kitongoji cha Bogini Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, amelazwa katika kituo cha Afya Pasua akiuguza majeraha ya moto, yaliyotokana na kuunguzwa kwa uji na shangazi yake akidaiwa kuiba maharage jikoni.

Tukio hilo ambalo linadaiwa kutokea Septemba 30 mwaka huu mchana nyumbani kwa bibi yake eneo la Bogini, linadaiwa kusababishwa na mzozo uliotokana na kijana huyo kuchukua maharage bila idhini ya shangazi yake

Akizungumza leo Alhamisi Oktoba 6, Kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Yahaya Mdogo amekiri kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa, tukio hilo limeripotiwa kituo cha polisi majengo na anafuatilia ili kupata taarifa kamili.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Bogini, Zubery Bakari amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa mwanamke anayedaiwa kufanya kosa hilo tayari amekamatwa na polisi.

Akielezea tukio hilo Bakari amesema, siku ya tukio akiwa kwenye kikao alipigiwa simu na kijana huyo, ambaye alimueleza kuwa ameunguzwa na uji na shangazi yake.

"Ilikuwa ni siku ya Ijumaa, nilipata simu kwa mtu nisiyemfahamu na nilipomuuliza alijitambulisha kuwa anaitwa Elvis, ndipo akanieleza amemwagiwa uji na shangazi yake ameungua na tayari amepitia polisi na wakati huo alikuwa akienda Hospitali.

"Jumamosi nilikwenda kituo cha afya cha Pasua kufuatilia nikamuona mgonjwa, kweli nilimkuta na majeraha ya kuunguzwa na uji na nilipohoji sababu alinieleza kuwa walitofautiana na shangazi yake, ndipo alipochukua uji na kumwagia," amesema.

Ameendelea kueleza kuwa, baada ya kumuuliza mwanamke huyo, alimwambia kuwa mpwa wake hajaumia sana.

Akisimulia tukio hilo, mama wa kijana huyo Ester Shayo amesema; "Siku ya tukio Elvis alirudi nyumbani akachota maharage jikoni lakini shangazi alimwambia asichukue maharage ni yake, akarudisha na kumwambia shangazi una roho mbaya hata chakula unamnyima mtu, na katika majibizano hayo ndipo alipochukua uji na kumwagia," amesema.

Source: Mwananchi
 
Kijana Elvis Shoo (27) mkazi wa kitongoji cha Bogini Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, amelazwa katika kituo cha Afya Pasua akiuguza majeraha ya moto, yaliyotokana na kuunguzwa kwa uji na shangazi yake akidaiwa kuiba maharage jikoni.

Tukio hilo ambalo linadaiwa kutokea Septemba 30 mwaka huu mchana nyumbani kwa bibi yake eneo la Bogini, linadaiwa kusababishwa na mzozo uliotokana na kijana huyo kuchukua maharage bila idhini ya shangazi yake

Uji huo ulimuunguza kijana huyo na kumsababishia majeraha sehemu za shingoni kuelea kifuani na kulazwa hospitalini ambako anaendelea na matibabu mpaka sasa.
Kweli siku hizi watani zangu wamechoka..[emoji2827]
 
Matukio mengi ya kikatili mchonganishi huwa ni kitu kimoja kinaitwa umaskini umaskini ni nusu ya uchawi ndo maana ukianza kufanikiwa ndugu wanaanza kukusema vibaya
Ndio maana sikuhizi nataka nilie noki kila kukicha hata nikifanikiwa kuwa na hela huwa nataka raia
wajue nateseka tu.
 
Kijana Elvis Shoo (27) mkazi wa kitongoji cha Bogini Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, amelazwa katika kituo cha Afya Pasua akiuguza majeraha ya moto, yaliyotokana na kuunguzwa kwa uji na shangazi yake akidaiwa kuiba maharage jikoni.
Kilimanjaro tena!!!
Huko nako kumekuwa kwa matukio kama enzi zile Kanda ya Ziwa
 
Na kwanini aunguzwe?
Jina ulochagua linaakisi ulivyo! Hivi unaona libaba la 27 years linatakiwa kukaa kwa ndugu? Kama ulivyo sema ni maamuzi yake! Sisi ni nani kupinga adhabu halali ya Bibi kwa Mjukuu wake ambaye akili yake ni ya miaka 5(analelewa) ingawa kiumbo ni 27 good years. Siku ingine ficha ujinga wako
 
Kijana Elvis Shoo (27) mkazi wa kitongoji cha Bogini Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, amelazwa katika kituo cha Afya Pasua akiuguza majeraha ya moto, yaliyotokana na kuunguzwa kwa uji na shangazi yake akidaiwa kuiba maharage jikoni.

Tukio hilo ambalo linadaiwa kutokea Septemba 30 mwaka huu mchana nyumbani kwa bibi yake eneo la Bogini, linadaiwa kusababishwa na mzozo uliotokana na kijana huyo kuchukua maharage bila idhini ya shangazi yake

Uji huo ulimuunguza kijana huyo na kumsababishia majeraha sehemu za shingoni kuelea kifuani na kulazwa hospitalini ambako anaendelea na matibabu mpaka sasa.
Kijana nampa pooe sana kwa hili janga lililomkuta. Namuombea apate nafuu mapema

Najiuliza, kijana wa miaka 27 anafanya nini kwao?
 
Back
Top Bottom