MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Inakuwaje kijana unakuwa hupatikani mida ya kazi? Utetezi ni hakuna network au ilikuwa chaji, yaani saa 4 asubuhi simu inakuwa chaji si upumbavu huo?
Ukitumiwa SMS hujibu hadi upigiwe na kujitetea sijaiona message? Kwenye email ndo majanga matupu, wengine mna biashara ila hata ku-update mara kwa mara unachofanya hakuna..😡😡
Naandika huu uzi nikiwa na mchanganyiko wa hisia za hasira na huzuni kwa pamoja. Hisia zangu zinasababishwa kuona hizi enzi za mambo kuwa digitally bado kuna watu hasa vijana wako usingizini na wasio serious kabisa na suala la mawasiliano. Napata hasira kuona wengi wao ni hawa vijana wajasiriamali waliojiajiri.
Ikumbukwe kwa wakati tuliopo mitandao ya kijamii ndo imeshika hatamu pamoja na namna nyingine za mawasiliano zilizorahisishwa. Visingizio vimekuwa vingi visivyoelezeka.
Ninawasihi vijana mbadilike.