Kijana, hii ndiyo siri bora kabisa ya kuwa tajiri, kafara yake haina madhara

Kijana, hii ndiyo siri bora kabisa ya kuwa tajiri, kafara yake haina madhara

Hizi accusations ni kali sana. Ukiniwekea uthibitisho nmefanya jambo hilo ntakulipa na kukurudishia mara 100. Siamini katika kuonea wasio nacho. Hata siku moja

Nijifunze kutoka kwenu wakati mnawaonea maskini na wake zao mnakula. Ni Matajiri wachache wanaoplay fair huku mtaani, lakini asilimia kubwa ni maumivu tu. Mtu anapesa kidogo anataka abudiwe kama Mungu, ndio maana hamuwezi kupenya kwenye Tundu la Sindano.
 
Hahahah mkuu mdau naona humuelewi kabisa ana-force but unamkataa!!

Wide forum kama hii bwana ukae kwa akili sana,mimi huwa naamini kile nilichokuwa nacho mimi tu sio kile anachoniambia mtu fulani kwamba anacho hali yakuwa simfahamu hata nikimfahamu hatonisaidia chochote but mawazo awe amebuni hakubuni nikiona ni chakula sahihi cha ubongo nabeba.

Humu wengine wanaweza kuwa wakweli,baadhi ya watu hupenda tu kiroho safi ku-share experiences ya mambo fulani fulani waliyokutana nayo hadi wamefanikiwa wengine unakuta ni msela tu na Tecno yake keshajishindia njaa huko na usiku atakula wapi hajui anaamua ku-post uzi wa kudadavua masuala seriously ya maisha aliyosikia watu wakihadithiana mahali ili apate likes mbili tatu kujibishana na member ili masaa yasogee alale.

Kipindi fulani Facebook kuna jamaa aliniomba urafiki nikamu-accept alikuwa kila jioni anafanya update ya wazo la jioni,hakika nikiri zilikuwa nondo hasa basi wadau tunakoment pale wa ku-support wanasapot wakumkataa wanamkataa alimradi ilikuwa furaha kuwa na rafiki kama yule,alipata followers wengi sana sasa siku moja mchana tumekaa sehemu na washkaji mshkaji wangu mmoja akaniomba nimuangalizie simu yake mbona kuna baadhi ya App's hazifanzi kazi kama alivyozoea hasa W'app?

Well ananiamini kuchezea chezea simu hizi kidogo naweza,kumbe tatizo alikuwa hajafanya update ya baadhi ya vitu muda mrefu so nikaingia play store zikajipanga pale App's zilizokuwa outdated Facebook ikiwepo nikazifanyia mwanzo mwisho sasa sijui ilikuwaje ktk kule kuongea ongea na kurusha rusha mikono nadhani bahati mbaya nikaufungua ukurasa wake nakuja kurudisha macho kwenye kioo nakuta tayari nipo ndani ya F'book kucheck hiv mbona profile hii kama ile tunayobadilishana mawazo kila jioni?alikuwa ameweka pic ya Dr Dre.

Sikum-diss mwana,nikampa simu yake kama sijui chochote ila since then nikajua aliyekuwa nyuma ya ule ukurasa ni mtu mmoja wa kawaida sana ila ana mawazo mapana mno iwe anayasikia mahali au sivyo alikuwa genius ila kinachosikitisha mawazo ya watu kama hawa huwa hawafaidiki nayo,mimi na yule nayachukua nachangamkia fursa nampiga gape yeye yupo pale pale.

Hapa tupo tujifunze na ndiyo matumizi mazuri na sahihi ya mtandao,tuvumiliane tu.
 
Tatizo kubwa tulilo nalo waswahili wengi ni chuki dhidi ya Matajiri. Mswahili anaweza kutuma text akisambaza kwa watu kuwa John au Juma kafulia huku akifurahia sana.

Haoni madhara ya Juma kufulia huku yeye akiwa ni maskini. Kuwa sasa Juma hatokuwa akinunua bidhaa zake, au hatoweza kumwajiri yeye au ndugu zake. N.k

Wengi tunaamini ukimchukia Tajiri unapata faraja. Nimeona nikiandika uzi nikielezea kauwezo kadogo niliko nako na jinsi watu wanavyonishukia kama mwewe. Wengine wakitaka uthibitisho.mimi sihitaji kutoa uthibitisho ili wewe uamini.

Mimi nlianza kupenda utajiri toka kwa mzee nliona ambavyo alikuwa akitulea watoto wake wawili pasipo shida.akibadilisha magari, akinunua tulicho na alichotaka. Akifungua makampuni na kuzunguka nasi duniani.

I learned a lot. Ndipo nlianza kujiambatanisha na marafik zake baba kiasi kuweza wakati mwngine kumwakilisha.nlimwambia nitatafuta pesa zangu mwenyewe nikishindwa ndo ntarudi anipe mtaji.

Nmefanikiwa. Napata mshahara mkubwa, natumia magari ambayo si haba matumizi ya Range Rover, BMW, Merceded Benz ndizo gari ambazo mzee alikuwa ananambia za kutumia.

Nliwahi uliza mtaji wa Mil 100 tutafanya biashara gani. Watu walinishambulia sana. But binafsi nlitaka nipate mtu mwenye mawazo ambayo sasa ningekaa naye tuyafanyie kazi.watu walitukana na wengine wakaandika kwa kebehi.

Kwa mwenye akili mil 100 ni nyingi sana kwa biashara. Kwa mpumbavu atakwambia hiyo haitoshi kabisa. Sikutaka ugomvi nikaiingiza kwenye mchakato mwingine maisha yakaendelea.

ILI UWE TAJIRI
Kafara unayotakiwa kuitoa ni moja. Ua kiburi, jeuri na ujuvi. Hivyo vitu vipo kwenye mwili mmoja ila ni viungo mbalimbali.

Usituchukie wenye vijicent. Jifunze toka kwetu. Badala ya kukaa majukwaa ya umbea na kufundishana styles za mapenzi kaa na watu wenye chakula ya Ubongo.

Jifunze kwa waliofanikiwa. Usiwachukie. Ni upumbavu kufurahi kuwa sasa bakhresa amefulia au Mengi amefulia. Huo ni wendawazimu.

Kakae miguu pa wenye mafanikio utafanikiwa. Mtoto akinawa vizuri anaweza kula na wakubwa. Trust me.

Fact kabisa shida ya asilimia kubwa ya watanzania wana roho mbaya
Shida ni shule na exposure!
 
Nitumie elfu kumi tu mkuu ili nijue kweli wewe umefanikiwa na hauna madhara
 
Pesa ni mhimu sana ili mtu usije ukaishi store ,, umasikini ni mbaya sana ,ukiwa masikini unakuta chini ya uvungu wako kuna kuku anaatamia ,,kuna majembe ,,kuna mahindi ya mbegu ya msimu ujao,kuna mapalage ,kuna matoborwa pia.. Yaan umasikini ni tabu sana
Mkuu Nimecheka sana mzee duh! Umenikumbuka mbali
 
Aise mimi natafuta utajiri kinyama tokea 2014 natafuta sijapata , nilifyeka kiwanja mpaka sasa sijamwaga hata tofali

Ila afe simba afe chui ,ifufike mizimu ya ukoo mimi nataka pesa aise ile kinyama.

Kikubwa nipambane kwa njia za halali ,nisipo kuwa na hela nitaendelea kudharaulika sana kwenye familia .
mkuu naomba uni pm namba yako naona tunaendana
 
Back
Top Bottom