Kijana, hii ndiyo siri bora kabisa ya kuwa tajiri, kafara yake haina madhara

Hizi accusations ni kali sana. Ukiniwekea uthibitisho nmefanya jambo hilo ntakulipa na kukurudishia mara 100. Siamini katika kuonea wasio nacho. Hata siku moja

 
Hahahah mkuu mdau naona humuelewi kabisa ana-force but unamkataa!!

Wide forum kama hii bwana ukae kwa akili sana,mimi huwa naamini kile nilichokuwa nacho mimi tu sio kile anachoniambia mtu fulani kwamba anacho hali yakuwa simfahamu hata nikimfahamu hatonisaidia chochote but mawazo awe amebuni hakubuni nikiona ni chakula sahihi cha ubongo nabeba.

Humu wengine wanaweza kuwa wakweli,baadhi ya watu hupenda tu kiroho safi ku-share experiences ya mambo fulani fulani waliyokutana nayo hadi wamefanikiwa wengine unakuta ni msela tu na Tecno yake keshajishindia njaa huko na usiku atakula wapi hajui anaamua ku-post uzi wa kudadavua masuala seriously ya maisha aliyosikia watu wakihadithiana mahali ili apate likes mbili tatu kujibishana na member ili masaa yasogee alale.

Kipindi fulani Facebook kuna jamaa aliniomba urafiki nikamu-accept alikuwa kila jioni anafanya update ya wazo la jioni,hakika nikiri zilikuwa nondo hasa basi wadau tunakoment pale wa ku-support wanasapot wakumkataa wanamkataa alimradi ilikuwa furaha kuwa na rafiki kama yule,alipata followers wengi sana sasa siku moja mchana tumekaa sehemu na washkaji mshkaji wangu mmoja akaniomba nimuangalizie simu yake mbona kuna baadhi ya App's hazifanzi kazi kama alivyozoea hasa W'app?

Well ananiamini kuchezea chezea simu hizi kidogo naweza,kumbe tatizo alikuwa hajafanya update ya baadhi ya vitu muda mrefu so nikaingia play store zikajipanga pale App's zilizokuwa outdated Facebook ikiwepo nikazifanyia mwanzo mwisho sasa sijui ilikuwaje ktk kule kuongea ongea na kurusha rusha mikono nadhani bahati mbaya nikaufungua ukurasa wake nakuja kurudisha macho kwenye kioo nakuta tayari nipo ndani ya F'book kucheck hiv mbona profile hii kama ile tunayobadilishana mawazo kila jioni?alikuwa ameweka pic ya Dr Dre.

Sikum-diss mwana,nikampa simu yake kama sijui chochote ila since then nikajua aliyekuwa nyuma ya ule ukurasa ni mtu mmoja wa kawaida sana ila ana mawazo mapana mno iwe anayasikia mahali au sivyo alikuwa genius ila kinachosikitisha mawazo ya watu kama hawa huwa hawafaidiki nayo,mimi na yule nayachukua nachangamkia fursa nampiga gape yeye yupo pale pale.

Hapa tupo tujifunze na ndiyo matumizi mazuri na sahihi ya mtandao,tuvumiliane tu.
 

Fact kabisa shida ya asilimia kubwa ya watanzania wana roho mbaya
Shida ni shule na exposure!
 
Nitumie elfu kumi tu mkuu ili nijue kweli wewe umefanikiwa na hauna madhara
 
Mkuu Nimecheka sana mzee duh! Umenikumbuka mbali
 
mkuu naomba uni pm namba yako naona tunaendana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…