Uchaguzi 2020 Kijana Ibzan Michael (24) atia nia Ubunge jimbo la Arusha Mjini kupitia CCM

Uchaguzi 2020 Kijana Ibzan Michael (24) atia nia Ubunge jimbo la Arusha Mjini kupitia CCM

Arusha kumtoa Lema nisawa nakupta PhD ya Magufuli
endelea kuota ..hata wana arusha ukiwauliza sasa lema ni nani utaishia kutukanwa tu, si vijana bodaboda si nani, wote hawamtaki,,arusha inarudi ccm kwa kishindo kizito
 
Watia nia kwenye kinyang'anyiro cha ubunge Arusha mpaka sasa wanakadiliwa kufikia 40 kwa wale walichokua fomu na miongoni mwao ni kijana mdogo wa chuo kikuu cha Dodoma UDOM ambaye amejitokeza kuchukua fomu na kusubiri kwa hamu kurudisha fomu na kuomba kudra za kikao cha kuteua jina moja.

View attachment 1506743
PICHA: Ibzan Michael (kushoto) akipokea fomu za kuwania ubunge jimbo la arusha mjini kutoka kwa katibu wa ccm.

Ibzan mwenye umri wa miaka 24 ameoneka kuwa ndiye mtia nia ya ubunge mdogo yawezekana kuliko wote wanaochukua fomu kwa tiketi ya CCM, anasema ana sababu nyingi zilizompelekea kuchukua fomu, japo muda wa kampeni bado ila anasema miongoni mwa sababu kama kijana anaona vijana wenye rika kama yeye wengi bado hawajapewa nafasi na fulsa hivyo wana changamoto ikiwemo ajira.

Ameongeza kuwa amejipanga kimwili, kiakili, akiwa na akili timamu huku akitambua kila mtu amezaliwa akiwa na utofauti wa kitu chake cha msingi, hicho ndicho kinacholeta utofauti katika nyanja ya uongozi.

Hata hivyo Ibzan anajiandaa kukumbana na majina makubwa ambayo bado hayajachukua fomu ukiachilia mbali meya aliyepita Kalist Lazaro ambaye kachukua fomu leo, majina hayo yanatajwa lakini bado wanatizamiwa kuchukua fomu siku za mbele kabla ya tatehe ya mwisho July 17.2020.

Mtia nia Ibzan anatembea akiwa na nia inayopewa nguvu ya kauli mbiu yake isemayo I born to impact the societies.



NB. Vijana wanaonyesha ujasiri wangali na damu changa kwenye wigo wa siasa zenye ushindani.
Kwa umri huu anagombea CCM?? Akiwa Mzee llazima atakua mchawi
 
Kumbe ndio maana leo nimeona tweet ya Lema, anasema angependa wote wanaochukua fomu kuomba kugombea hiyo nafasi ya ubunge Arusha Mjini kwa tiketi ya CCM wapitishwe wote kama ingekuwa inawezekana, halafu akawachape wote kwa pamoja kwenye sanduku la kura.
Lema mwenyewe kwenye chujio la Chama hapiti. Kwa Mromboo wamegoma
 
Hivi fomu ni Tsh ngapi? Mwenye kujua
Fomu TZS Laki 1 tu ili kupunguza ushindani unaweza kuandaa Milioni 3 ukagawa kwa vijana wasiojielewa wakajichukulie fomu ili kamati iwaone sio mtu mzima unapita kwa kunyata
 
Sasa kila Mwananchi anataka kuwa Mbunge ili kuwatumikia Wananchi.

Inaonekana hakuna anayeitaka taabu ya kubaki kama Mwananchi na kutumikiwa....kuna kila dalili kuwa ki siasa kutumikia ni neema kuliko kutumikiwa.
Watia nia wamekuwa wengi nadhani kuliko hata wapiga kura
 
Mwaka huu wagombea wengi kuliko wapiga kura
 
umri huo alafu HAJAOA, KICHWANI HANA LOLOTE...zaidi akizeeka atakuwa mchawi si bure huyo
 
Kila la kheri kwake kam atawez kuptishwa maan asilimia kubw maendleo uletwa na vijana na wazee kam yao zaid ni kuptisha
 
Back
Top Bottom