Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kumuomba Mungu kwa mambo yaliyo ndani ya uwezo nao ni uzwazwa!. Mungu tunamwomba mambo yaliyo juu ya uwezo aliotupatia.Yote hayo hayawezi kuGuarantee chochote. Alipangalo Mungu litakuwa tu. Cha maana ni kuomba msaada na maongozi ya Mungu katika maisha yetu!
MwanaumeNgono inapigiwa chapuo sana, halafu muhanga eti mwanamme tu….. utafikiri wanawake hayo maradhi hayawahusu.
Hii ndo sababu maisha ya mwanamme yamejaa mateso, na kufa mapema ni stahiki yake….. mke ana miaka 50 eti bado niwaze kuchapiwa hell NO!!!
Uzuri ni kwamba pia alitupa uwezo mkubwa sana wa kudeal na hayo majukumu. Yupo vizuri. Namkubali sana!Dah! Wanaume Mungu katupa majukumu makubwa sana.....
Hakuna jinsi yote maisha........
Nakubali sana taikonKwema Wakuu!
Hatufuatiliani wala hatupangiani maisha. Ila tunakumbushana huku nami nikijikumbusha pia Kwa Nia nzuri tuu. Ili baadaye tusijekujikuta katika Huzuni kuu.
Vijana tunapoambiwa tule na tunywe Kwa nidhamu sio Kwa sababu tunaonewa wivu au kuna mtu anataka kuwa juu yetu Kwa kutupa amri. HASHA! Bali ni Kwa faida yetu.
Kisukari na Presha sio magonjwa mazuri Kwa ustawi wa Ndoa zetu. Ukisikia pigo Baya basi ni kukosa nguvu za kiume. Tena Kwa miaka 40 Kwa mwanaume bado ni kijana. Na Kwa bahati nzuri miaka hiyo wengi neema ndio zinazidi kufunguka na wamesha-settle.
Sasa ume-settle alafu unajikuta huna nguvu za kiume. Asikuambie mtu inahuzunisha Sana..
Ukiona Taikon anaelezea Jambo Fulani basi kaa nalo macho, lizingatie Sana. Kwa sababu Taikon nipo kwaajili ya kujenga na wala sio kubomoa.
1. Kula na kunywa vizuri,
i. Kula Mbomboga Kwa wingi, Kula Protein Kama nyama nyeupe, maziwa, mayai, Kwa wingi,
Kula wanga kidogo Sana. Mfano unapoka maharage mengi alafu unakula na wali kidunchu, au ugali kidogo na Samaki au nyama au maharage mengi.
ii. Matunda, pendelea Kula matunda,
Kama umeoa, pendelea Ndizi zilizoiva angalau kila siku moja hasa usiku, hii itafanya uume wako kuwa na nguvu kutokana na madini ya Potassium,
Mkeo aweke Kachumburi yenye Nyanya, vitunguu, limao na pilipili hizi zinaongeza Libido.
Safisha figo Kwa Matikiti, matango, usisahau mapapai na maembe, pia machungwa huku utapata vitamini
Kula Milo miwili ukiwa age ya 25-50 iwe balanced.
iii. Kunywa maji mengi, angalau Lita mbili na nusu mpaka tatu na nusu Kwa siku.
Pombe kunywa kiasi Kwa STAREHE sio kujiumiza. Angalau kwa wiki mara moja na hakikisha usinywe mpaka ukazima.
Maji mengi ni dawa kwani yanafanya seli za mwili wako kufanya kazi Kwa ufanisi zaidi. Maji hupunguza pia sumu mwilini na kuufanya mwili wako kuwa na Nuru,
Yaani mtu anayezingatia kunywa maji ngozi yake hung'aa
Pia maji mengi husababisha mtu kutokuzeeka Kwa haraka. Na hii ni kutokana na Uzalishwaji wa seli za mwili kufanyika Kwa ufanisi
2. Fanya mazoezi,
Mazoezi hujenga mwili na kuufanya kuwa na Afya, kwani hufanya mzunguko WA damu kufanya kazi vizuri. Kumbuka Damu ndio hubeba virutubisho na kuvisafitisha mwilini. Kumbuka pia ndani ya damu ndio kuna Seli nyeupe zinazolinda mwili dhidi ya magonjwa, Seli nyekundu ambazo husafirisha hewa ya Oksijeni kuzipa Seli, tishu na ogani Uhai. Hasahasa Ubongo.
Hii ni kusema mazoezi yanaimarisha ufanyaji kazi WA viungo vya Mwili Kama vile Ubongo. Hii inafanya akili kuwa active.
Aina ya mazoezi
i. . Mazoezi ya Mwili
Haya yanalenga zaidi viungo na organ za mwili. Kukimbia, Push-up n.k.
ii. Mazoezi ya Akili/Ufahamu.
Haya yanalenga zaidi tafakuri, uchanganuzi, uchambuzi, n.k. haya ni Kwa kusoma Nyaraka na vitabu, michezo na Bangua bongo, Game zinazoshughulisha akili n.k.
Pia mazoezi ya ubongo hufanyika Kwa kujaribu kufanya vitu vipya ili kutafuta changamoto mpya. Kama ni biashara, au kazi au miradi unaanzisha ili akili ipate changamoto mpya.
iii. Mazoezi ya Kiroho na Nafsi.
Haya hulenga zaidi roho na Nafsi yako.
Kudhibiti Nafsi yako na matamanio yake, mfano Kufunga Kula na kunywa,
Kama unapenda kunywa pombe kujizuia kutokunywa Kwa muda wa siku kadhaa.
Kama unapenda Kulala na wanawake, kujizuia hata Kwa miezi sita bila kuchepuka, hayo ni mazoezi ya kiroho na nafsi.
Pia kutoa Zaka au Sadaka Ile inayouma. Ni zoezi la Nafsi au kiroho.
Hii itakusaidia kujidhibiti, pia kuzuia Nyege mshindo au ukosefu wa maamuzi.
3. Mapumziko na Burudani/STAREHE.
Angalau Kwa siku ulale masaa yasiyopungua Nane.
Starehe au burudani angalau Kwa wiki au Kwa mwezi mara moja. Hii itakufanya usiyachoke maisha na kuyaona hayana maana.
Usingizi utakusaidia kutunza Ubongo wako na hii itakusaidia nyakati za uzeeni kwani utakuwa haupotezi kumbukumbu kijinga jinga.
Kabla watu hawajaona uzee wako wewe mwenyewe utaanza kuuona Kwanza Kwa kujikuta unasahau sahau mambo, na hiyo huanza kutokea miaka 30+ kama hutokuwa mtu wa kuzingatia mapumziko.
Kijana wa sasa unapaswa ujidhibiti mwenyewe ili isijekula kwako ufikishapo miaka 40.
Hakuna kitu kibaya Kama kufikisha umri huo yaani 40+ alafu ujikute hauna pesa, alafu magonjwa Kama kisukari na Presha vikupige. Ni hatari Sana.
Kupigiwa nje nje! Yaani mwanamke wako wala hatakuwa na Woga, nawe utakuwa unajua na chakumfanya hauna.
Wale mnaolalamika andiko refu nimewasikia. Nipumzike sasa!
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Nabii Musa alikufa na miaka mingi (80 kama sikosei) na alikufa huku macho, meno yakiwa vizuri kama teenager. Enhee hapa wasemajeLakini wote tutazikwa chini
Lakini wote tutazikwa chini
Umezunguka Sana,,
Ulipaswa ujumuishe kitambi ktk hayo magonjwa .
Kadiri tumbo linavyojitokeza mbele na dushe linaingia ndani kama kichwa cha Kobe.
Mazoezi ya push ups ndy muarubaini wa kila kitu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Ngono inapigiwa chapuo sana, halafu muhanga eti mwanamme tu….. utafikiri wanawake hayo maradhi hayawahusu.
Hii ndo sababu maisha ya mwanamme yamejaa mateso, na kufa mapema ni stahiki yake….. mke ana miaka 50 eti bado niwaze kuchapiwa hell NO!!!
Pamoja sanaa mkuu...somo zurii...umetumia njia nzur kuufikisha ujumbe wako.....upo kweny mfumo wa taarifa lkn pia kama onyo...kongole kwako
Hapa kwenyewe nina miaka 28 nina show mbovu kabisa haijawahi tokea tangu dunia iumbwe nimeshaachwa na Wanawake kama 5 hivi,nikifika miaka 40 si ndio balaa ilo.
Uzuri kiuchumi nipo vzr acha niendelee kugonga vyombo kwa kwenda mbele nguvu kizibo hata pombe nisinywe kweli ? nimeshakuwa chronic kwa kuachwa nimeshazoea
Kuna kuwa na hisia lakini ukashindwa kufanya, hapa inawezekana ukachezewachezewa nawe ukachezea chezea inaweza kuwa fantacy pia.
Kuna kutokuwa na hisia kabisa ~ hii nayo inaweza isiwe issue maana huna hisia na wala hufikirii chochote kuhusu kugonga.
Naamini mwenyezi Mungu ana makusudi yake kwenye kila jambo, ila tumuombe atupe vile ambavyo ni bora zaidi.
Ni kweli ndugu magonjwa yasio ambukiza ndio yanatutesa Kwa SASA
Bandiki Suri sana, ngoja tuzingatie pale panapo wezekana.
Kufa hamfi ila mtakufa huku mmechoka sana hata huko mbinguni mtaenda kwakubulutwa