Kijana mpambanaji, hatma yako ipo mkononi mwako

Daudi anasema nalikuwa kijana sasa ni mzee sijawahi ona mwenye haki ameachwa wala watoto wake wakiomba mkate barabarani.

Nilitaka kusema hivi kila mtu huzaliwa na kitu (kipaji/uwezo) fln ukiutumia uwezo au kipaji iko kufanikiwa ni sawa na kusukuma mlevi tu.Mleta uziamepiga kwenye mshono.

Mfano mimi sina furaha kabisa kwenye ajira ninayo ifanya hii japo malipo ni mazuri lakini kamwe sijawahi kuipenda. Mimi huwa nikiwa shamba napiga kilimo watu huja na kusema wewe huko .....ulienda tu kwa bahati mbaya wewe rudi huku tujifunze kwako!
 
Hakika, Asante kwa huo ushuhuda wakweli kabisa
 
mimi ajira ndio inanipa kula na kuendesha maisha yangu ,lakini huwa sipendi kabisa mambo ya ajira.Nikiona biashara ya nafaka napagawa kabisa,nimegundua kuna kitu Mungu atakuwa amenipangia kwenye nafaka maana sio kwa mahaba hayo.Nimenza na gunia 50 na msimu huu naona kabisa hali sio mbaya Feb nazitoa
 
Mwezi wa1 mimi naachana na haya ma ajira. Nilimshirikisha jamaa akanishangaa akasema unaachaje kazi yako inayokulipa vzr.
Jibu nilimwambia moja tu sina furaha nayo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…