Kijana mwenzangu una nafasi ya kuwa na kila unachohitaji

Kijana mwenzangu una nafasi ya kuwa na kila unachohitaji

kelphin

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2019
Posts
9,872
Reaction score
16,319
Kila kitu kizuri kinachoonekana mbele ya macho yako leo.,elewa ya kua ni mipango ya watu nyuma. Maisha ni kama story yana kila hatua na matukio mbalimbali.

Yakuhuzunisha, kufurahisha na hata kuvunja moyo ila isiwe kama sababu kwako au pengine tunatofautiana mpango wa fedha kutokana na familia zetu.

Tunazidiana na tunatofautiana pakubwa. Yamkini familia yenu nyumbani inakutazama wewe
Ila bado nayo isiwe kama sababu ya kukurudisha nyuma.

Hebu tupange malengo madogo kwenda makubwa kisha tugawanye malengo hayo kwenye kipato pamoja na muda

Ni kweli unatakiwa ku enjo(kama wasemavyo wa darisalamu) ila iwe kwa 1/10% ya kipato unachokipata
Tujifunze ku balance chupi kwa namna yoyote ile.

Kwasababu hilo ni moja ya mambo yanayomaliza sana uchumi wetu.

Tujifunze kuishi kwa malengo.na sio kufikili juu ya kufanya mambo wanayowapenda watu wengine


Ishi kwenye uharisia wako,panga malengo yako
Kua bahiri(ubahiri ni sifa njema kwa wanaume wanaojielewa)

Tunakumbushana tu.
 
Back
Top Bottom