Nevergive up
JF-Expert Member
- Dec 24, 2024
- 600
- 945
Kijana MWENZANGU acha kukata tamaa maisha yanawezekana ni kuamua na kusimamia ndoto zako.
Nilimaliza form 4 mwaka 2017 ndoto zangu ni kuwa doctor lakini matokeo yalipotoka Aiseee sikuamini nilipiga 4 ya 28 ingawa masomo ya sayansi nimepiga D zote. Nikawacheki wazazi nikawaomba wanipeleke chuo wakasema hawana pesa hivyo ikabidi nikae kitaa miaka 2 huku nikiwa ni mebeba maono siku Moja nitasoma tu
Basi kitaa nikajifunza kunyoa,kuchomerea,umeme na kuumganisha madishi kama azam,dstv ,Zuku n.k,lakini moyoni naona bado Kuna kitu kimepungua .hivyo Kwa hasira nikaamua kwenda DSM 2019 kutafuta maisha na nikafikia Kwa mjomba naye mjomba akanitelekeza hivyo nikawa mtoto wa mtaani Sina pakuishi.basi ikabidi nianze kutafuta kazi hatimae 2020 miezi ya mwanzo Mungu akajalia nikapata job kiwandani pale Kwa mkapa external .
Pale nilifanya kazi mwaka mzima nikameki pesa nikaenda kuomba chuo mwaka 2021 nikapita. na nikalipia ada mwaka mzima nikaingia darasani, hivyo napiga job huku najisomesha Kwa mshahara wa 99000 Kwa mwezi na huku nimepanga chumba cha 30000 mabibo.nimesoma miaka 3 nikamaliza na matokea yakatoka poa sana. Leo hii siyo yule Tena Mungu Ni Mkuu. Kifupi now nimelamba asali. Ujumbe ni nini? Nikwamba vijana wenzangu piga moyo konde usikate tamaa simamia maono yako Utafika.