Kama Mozambique, uchaguzi wa TAMISEMI 2024 Tanzania kulikuwa na mamlaka mbili zinazosimamia uchaguzi 2024.
Moja ni kikundi kificho cha watu wachache chenye kunufaika kungangania kubaki madarakani.
Na kikundi kingine cha wazalendo wenye kuhoji vipi mbona faulo nyingi. Soma uzoefu wa mbinu za kuwezesha uchafuzi wa uchaguzi kutoka kwa FRELIMO ya Msumbiji chama rafiki cha CCM:
Kigogo wa Tume ya Uchaguzi Mozambique ktk mahojiano exclusive - Mchakato na Uchaguzi uligubikwa na uchafuzi
View: https://m.youtube.com/watch?v=2B_xQtuZLW8
Naibu mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Bw. Fernando Mazanga asema uchafuzi wa uchaguzi na uchafuzi wa chakato wa uchaguzi, Tume haiwezi kusema nani alishinda..
Kwanza kiukweli kulikuwa na Tume mbili zinazosimamia mchakato, moja ni Tume ya Uchaguzi halisi isiyo na meno, na nyingine ni Tume Kificho ya Watu Wachache wa Frelimo waliokuwa na meno, rasilimali fedha na maamuzi ya kupika matokeo asema Fernando Mazanga
Alipoulizwa kuhusu Tume Kificho ya Watu wachache wa Frelimo ikifanyaje kufanya uchachuzi wa mchakato wa mzima wa matayarisho ya uchaguzi, uandikishaji na upigaji kura siku ya uchaguzi tarehe 9 Oktoba 2024 kigogo Fernado Mazanga alifunguka ...
Tume ya Ukweli ya uchaguzi ilinyimwa fedha na wizara ya fedha ya Mozambique na hata pesa zikipotolewa kidogo zote zikitumika makao makuu ya tume huku mikoani, wilayani na mitaani wasimamizi na wasimamizi uchaguzi walikuwa hoi si kifedha bali hata kimafunzo ya kuwapa uwezo wa kuandikisha wapiga kura, uteuzi na rufaa za mapingamizi.
Wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi walikuwa hawaelewi kanuni, sheria na miongozo ya kufanikisha uchaguzi ulio wa kiwango cha kukubalika ni huru, usiopendelea upande wowote na wakuweza kutoa matokeo sahihi ya kura zilizopigwa na mgombea yupi kazoa kura halali.
Fernando Mazanga anaongeza kuwa kutokana na Tume halisi kunyimwa uwezo wa kila aina, Tume kificho ya FRELIMO iliingia kazi kutangaza idadi ya watu waliojiandikisha ambayo haiwiani na takwimu za sensa ya taifa ya Mozambique ikiyofanyika 2023.
Wasimamizi wakuu na wasimamizi wasaidizi katika majimbo na wilaya walikosa kuwa na idadi za kulinganisha idadi ya watu katika maeneo yao ya majimbo, wilaya, kata na mitaa hivyo kura za ziada ya kuongezwa na FRELIMO ziliweza kutangazwa.
Huku wananchi hawafahamu idadi ya watu rasmo ktk maeneo yao kama sensa ya taifa ilivyokuwa ikionesha eneo kwa eneo, kijiji kwa kijiji, mtaa na kata.
Ingawa vyama makini vya upinzani zilipiga kelele kuwa idadi ya kuandikishwa watu katika sensa hailingani idadi ya wapiga kura watarajiwa na kura za matokeo yaliyotangazwa zimezidi kwa mbali idadi ya watu katika ripoti za sensa za taifa .
Wananchi baada ya kustuliwa kuhusu wafanye rejea za idadi ya watu na idadi ya wapiga kura wakabaini uchafuzi uliofanyika na kupelekea maandamano nchini Msumbiji kupinga matokeo yaliyotangazwa.
Mahakama ya Kikatiba iliyopewa mamlaka kusikiliza mapingamizi ya matokeo, imeomba tume ya uchaguzi ya taifa iwasilishe nyaraka ili ukaguzi ufanyike. Tume ilipewa siku 8 iwe imewasilisha nyaraka zote za uchaguzi uliofanyika 9 Oktoba 2024 zipitiwe na kufanyiwa ukaguzi wa kina.
Bw. Fernando Mazanga Naibu mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Mozambique anasema siku 8 zimepita na zinaonesha kuwasilishwa nyaraka zote zilizohifadhiwa katika Ofisi za Majimbo na Wilaya.
Lakini pamoja na nyaraka hizo kukusanywa sehemu, Mahakama ya Kikatiba hawajapewa makaratasi hayo ya kura na rejister za wapiga kura leo.
Inasemekana serikali inalaumu kutofika makaratasi hayo kutokana na vurugu za maandamano, lakini kigogo huyo Fernando Maganza anatillia shaka sababu hiyo kuwa vurugu zimezuia katatasi hizo kufika mji mkuu wa Mozambique Maputo.
Pengine Tume fiche ya Uchaguzi ya FRELIMO imeshikilia makaratasi hayo katika kituo salama (safe house) ikiyapitia matokeo hayo ya uchafuzi wa uchaguzi na kujiuliza wayawasilishe au la. Pia wanatafuta njia nyingine ya kuingilia mchakato wa Mahakama ya Kikatiba n.k n.k kujiokoa kutoka skandali hilo zito.
Fernando Mazanga alipoulizwa kama matokeo yanaweza kufutwa kutokana na uchafuzi wa wazi wa mchakato na uchaguzi sawia, kigogo huyo mzalendo wa Tume Halisi ya Uchaguzi anasema hawezi kutoa mawazo yake sasa kwa kuwa yeye ni mtu wa ndani kabisa katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mozambique.
Hivyo anaiachie Mahakama ya Kikatiba ibebe majukumu yake kuhakiki na kutoa hukumu sahihi baada ya kujiridhisha na ushahidi wote anahitimisha naibu mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa nchi Mozambique Bw. Fernado Mazanga.
Muito Abrigado kwa kutusikiliza
Source : DW Português para África : DW Kireno Africa
More info :
Maputo, Mozambique
Mahakama ya Katiba Mozambique yataka wasimamizi wa uchafuzi wa uchaguzi kujitetea madudu ya wazi yaliyojitokeza katika uchaguzi wa 9 Oktoba 2024 nchini Mozambique
Picha : Waheshimiwa majaji wa Mahakama ya Kikatiba Mozambique