Kijana ni Taifa la leo. Tukatae kusahaulika na kutumika Kisiasa na Kiuchumi

Kijana ni Taifa la leo. Tukatae kusahaulika na kutumika Kisiasa na Kiuchumi

Librarian 105

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2023
Posts
261
Reaction score
356
Kila nikitafakari hatma yetu sisi vijana naumia kutoiona kesho yetu katika nchi ya ahadi. Kiuchumi tunakabiliwa na ukosefu wa ajira na kisiasa tunaambiwa ni taifa la kesho. Ingawa tuna hussle na maisha lakini hatupo pamoja kiroho na kimwili kupamambania haki zetu kitaifa. Tufanyaje?

Kupitia uzi huu, kuna mbaya tukiwa tunatupia mawazo yetu kwenye uzi huu ili yasomwe na washika dau? Na tuvuke zaidi kwa kuomba msaada JamiiForums wa mawazo yetu kufikishwa kwa serikali yetu na vyombo husika?

Naona imetulia, kama poa, tuchukue hatua.

Nawasilisha uzi jamvini.
 
Mawazo ukiyafikisha yatafanyiwa kazi na nani? utaishia kuambiwa jiajiri, nchi hii hakuna kiongozi mwenye nia njema na wananchi hata kidogo kila mtu anataka kuiba pekee anufaike binafsi
 
HAITATOKEA KWA TANZANIA HII VIJANA KUWA "TAIFA LA LEO" KWA KATIBA HII.IWAPO VIJANA MNATAKA KUWA "TAIFA LA LEO" BASI PAMBANENI KWANZA KUPATA "KATIBA MPYA" WATAWALA WATAENDELEA KUIMBA WIMBO ULE ULE WA KILA SIKU KUWA VIJANA NI "TAIFA LA KESHO" NA HIYO KESHO HAITAFIKA MILELE NDIO MAANA WASTAAFU WA NAFASI ZA JUU WANAENDELEA KUTEULIWA TENA BADALA YA KUPIMZIKA KUPISHA VIJANA.
 
Report ya CAG kiko wapi?
Ikiwa tutazama nyuma mioyo itakufa, lakini tukitazama wakati ujao na kuchukua maamuzi ya kuthubutu, matumaini yatapatikana kama sio kwetu basi ni kwa kizazi chetu kijayo. Vipi kama wazee wetu waliojitoa mhanga kupambana na ukoloni na badaye wengine kudai uhuru wangekaa kimya na kukubali udhalili?
 
HAITATOKEA KWA TANZANIA HII VIJANA KUWA "TAIFA LA LEO" KWA KATIBA HII.IWAPO VIJANA MNATAKA KUWA "TAIFA LA LEO" BASI PAMBANENI KWANZA KUPATA "KATIBA MPYA" WATAWALA WATAENDELEA KUIMBA WIMBO ULE ULE WA KILA SIKU KUWA VIJANA NI "TAIFA LA KESHO" NA HIYO KESHO HAITAFIKA MILELE NDIO MAANA WASTAAFU WA NAFASI ZA JUU WANAENDELEA KUTEULIWA TENA BADALA YA KUPIMZIKA KUPISHA VIJANA.
Wazo zuri mkuu, changamoto iliyopo ya kwanini tunakuwa taifa la kesho, ni kuwa tumekubali kulishwa sera na mikakati ya kukombolewa. Na pia kutoshiriki kikamilifu harakati za mapambano ya kujikwamua kiuchumi pamoja na kisiasa. Vipi tutatambulika pasina kujipambanua ya kuwa tuna fikra za kimageuzi na mitazamo chanya ya kulitumikia taifa letu? Vipi tutashinikiza kufumuliwa kwa sera za utumishi wa umma kwa kulia vijiweni na kulaumu kwenye mitandao ya kijamii?
Vijana kuunganisha nguvu haimaanishi kuwa nyuma ya vyama vya siasa nyakati za uchaguzi au kusubiri wanasiasa kutuwakilisha kwenye majukwaa ya kisiasa. Kuwa na jukwaa la uchumi la kujadili namna sera na mikakati ya kitaifa inavyotuweka pembeni, ni mojawapo ya kujua jinsi mifumo inavyotunyonya na nini tunatakiwa kufanya kuleta magaeuzi, hakuna jamii iliyojikomboa bila kuchukua hatua.
Na mtazamo wangu wa harakati hii sio kufanya vurugu na kutukana utawala. Ila kuwazindua watawala na sisi wenyewe kupeana hamasa na kusaidiana fikra za kujijenga kiuchumi na kijamii.
 
Back
Top Bottom