Librarian 105
JF-Expert Member
- May 6, 2023
- 261
- 356
ni sawa, lakini bora kuthubutu kuliko kuendelea kukaa kimyaMawazo ukiyafikisha yatafanyiwa kazi na nani? utaishia kuambiwa jiajiri, nchi hii hakuna kiongozi mwenye nia njema na wananchi hata kidogo kila mtu anataka kuiba pekee anufaike binafsi
Report ya CAG kiko wapi?ni sawa, lakini bora kuthubutu kuliko kuendelea kukaa kimya
Ikiwa tutazama nyuma mioyo itakufa, lakini tukitazama wakati ujao na kuchukua maamuzi ya kuthubutu, matumaini yatapatikana kama sio kwetu basi ni kwa kizazi chetu kijayo. Vipi kama wazee wetu waliojitoa mhanga kupambana na ukoloni na badaye wengine kudai uhuru wangekaa kimya na kukubali udhalili?Report ya CAG kiko wapi?
Wazo zuri mkuu, changamoto iliyopo ya kwanini tunakuwa taifa la kesho, ni kuwa tumekubali kulishwa sera na mikakati ya kukombolewa. Na pia kutoshiriki kikamilifu harakati za mapambano ya kujikwamua kiuchumi pamoja na kisiasa. Vipi tutatambulika pasina kujipambanua ya kuwa tuna fikra za kimageuzi na mitazamo chanya ya kulitumikia taifa letu? Vipi tutashinikiza kufumuliwa kwa sera za utumishi wa umma kwa kulia vijiweni na kulaumu kwenye mitandao ya kijamii?HAITATOKEA KWA TANZANIA HII VIJANA KUWA "TAIFA LA LEO" KWA KATIBA HII.IWAPO VIJANA MNATAKA KUWA "TAIFA LA LEO" BASI PAMBANENI KWANZA KUPATA "KATIBA MPYA" WATAWALA WATAENDELEA KUIMBA WIMBO ULE ULE WA KILA SIKU KUWA VIJANA NI "TAIFA LA KESHO" NA HIYO KESHO HAITAFIKA MILELE NDIO MAANA WASTAAFU WA NAFASI ZA JUU WANAENDELEA KUTEULIWA TENA BADALA YA KUPIMZIKA KUPISHA VIJANA.