Kijana ufahamu usimpe na madhara yake ili ujiepushe

Kijana ufahamu usimpe na madhara yake ili ujiepushe

Zemanda

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2021
Posts
10,999
Reaction score
23,540
Kijana najua upo katika hali ya sintofahamu kuwa ukiacha kusimp utaishi vipi katika jamii hii ambayo imeamini kuwa simp ndie mwanaume bora kwa mwanamke.

Mimi ninae kuandikia hapa sio simp na ninaishi nje ya mfumo wa usimp. Awali ya leo nikiandika hapa nilishawahi kusimp na niliona ni sawa na ufahari ila nikwambie tu mwisho wa siku nilipokuja kuchakata kichwa nikayatazama maisha kwa uhalisia wake plus kujifunza kwa walionitangulia experience nikaona namna ninapoteza zaidi kwa kuwa simp.

The moment ukiacha kuwa simp ndio utaanza kuona potential yako kama mwanaume na nguvu ya kimaamuzi uliyo nayo na utawajua wanawake kwa asili yao na tabia zao na utaweza kwenda nao kwa namna inayotakiwa na sio kuburutwa kama ng'ombe machinjioni au ngamia jangwani.

Kusimp ikiwa ni tabia yako kuna mengi sana utapoteza na utatumika na kutumika tena na tena na tena kwa maslahi ya wanawake na kwa faida yao pekee yao na sio yako.

Utasifiwa na kupewa majina mazuri na hadhi ya uongo ambavyo vitaondoka mara utakapoacha tumika. Mbaya zaidi, wewe kama mwanaume utakua fedheha kubwa sana kwa mtoto wako wa kiume ambaye anakutegemea umfundishe principles za kiume na namna atakuwa na maamuzi ya msingi kwenye maisha yake na familia yake kama mwanaume.

Ukichagua kuwa simp na kuishi katika usimp utapitia mateso na mfumo ambao hauna faida na wewe kama;

Utakataliwa sana kwasababu wanawake wanawatumia masimp ila hawawahitaji sababu wanajua ni wanaume dhaifu ambao hawatajenga nao familia imara.

Mwanamke akikaa na simp jua ni ana pesa na mali na hapo anamlia timing azipune zote ziishe amtoroke.

Utaliwa na kunyonywa kidogo ulicho nacho bila kupata unachostahili. Wanawake watakununulisha chakula cha gharama kwa shukurani ya asante tu.

Utawasindikiza kwa wabwana zao ambao hawawatumii kama wanavyokutumia wewe na utarudi mwenyewe ukiamini ipo siku atakuweka wewe katika nafasi hiyo, utanunulishwa vocha na bundle za internet, utalipishwa kodi, utatumika kipindi akiwa mpweke na anahitaji kampani ila wewe ukitaka kampani yake ni hadi ulipie gharama kubwa au atake yeye kupanga muonane.

Utapoteza heshima yako kama mwanaume. Mwanamke akiwa anakuburuta anajua kuwa ni kwasababu anakumudu otherwise mwanamke ni YES person kwa mwanaume anayemuamini na kumuona kidume haswa.

Atakupangia ratiba, atapanga matumizi ya pesa na mali zako, atakutumia akiwa anajiskia ila asipojiskia atakughost na kukupotezea sababu anajua akibonyeza tu simu unakuja kasi kama mbwa kamuona boss wake.

Utakuwa kituko cha jamii na utaharibu self-esteem. Hakuna mtu hatajua kuwa unasimp sababu huwa masimp wanaonekana mchana kweupe kwa maneno na matendo. Vijana wadogo watakudharau sana kwasababu wanaona namna huyo mwanamke unayemtukuza namna anakutumia na kuna wanaume wengine wanamtumia kama kiburudisho.

Kijana fanya kama unaacha kuwa simp na kuanza kuwa na sura na character ya kiume isiyopelekeshwa na hisia za kizembe.

Jitambue kwa kuanza kidogo kidogo japo hata vitu hivi vifuatavyo;

Anza kujenga thamani yako ambayo mtu akijiuliza wewe ni nani na unafanya nini then haiba yako itakuwekea nafasi ya heshima. Mwanamke anakuomba pesa ya saloon leo mpatie,halafu mtazame atabehave vipi baada ya hapo.

Kama ataonyesha kukupuuza then jiulize kwanini kwenye shida wewe ulikuwa kipaumbele yake. Msubirie akirudi siku nyingine na shida kama hiyo au nyingine, mwambie tu straight forward,”ina maana mimi huwa unaniwaza ukiwa na shida tu” au? Nadhani ni muda muafaka unambie mimi na wewe tunamahusiano ya namna gani hadi mimi natafutwa wakati wa shida tu”.

Kwa wanawake wa sasa wasivyo na aibu atajibu “eeh am sorry kama nimekufanya ujiskie vibaya” halafu atakaa kimya akijua utaendeleza mawasiliano na kutaka kumplease umbembeleze ili ajue ni simp ama la aanze kukutumia.

Hapo ndio nafasi yako ya kuonyesha wewe sio simp. Kaa kimya na fanya kufuta namba.
Weka mipaka yako. Usitumie nguvu kusema unataka nini ila kuwa na sentensi Rafiki ila zenye msisitizo.

It's okay kumwambia mwanamke mzuri sana na mwenye mvuto kuwa upo busy anapoomba umsindikize shopping, its okay kumwambia mwanamke kuwa hauna hela ya kumpatia anapokupigia ghafla na shida zake hata kama una milioni 10 kwenye account.

It’s okay kumwambia single mother kuwa watoto wake sio jukumu lako hivyo anavyo kulaumu kwasababu umeshindwa mpatia pesa ya mahitaji ya watoto wake wakati ninyi si wazazi bali wapenzi ni kukukosea heshima na kama anakuona tatizo then kwanini alizaa na mtu wa hovyo.

Its okay kuacha kumtext mwanamke ambaye anakuonyesha hana muda wa kuwasiliana na wewe na kufuta namba yake wanawake wazuri wapo wengi sana huko nje.

Chochote unachofanya hakikisha unazingatia mipaka yako ambayo umejiwekea.
Kuishi kwa mrejesho.

Maisha ni kusaidiana na kushirikiana. Ukikutana na mwanamke ambaye ametengeneza mahusiano ya kupata kupitia wewe ila yeye kujitoa kwako ni tatizo au ukiona tu unafuatilia mwanamke ambaye hakupi mrejesho wa jitihada unazotoa then mapema kabla haujawa mjinga hebu achia ngazi na uondoke mapema ukatafute mwanamke mwingine ujenge upya mahusiano mengine.

Kuwa mtu wa ujitoa sio kwasababu unawekeza. Kanuni za maisha zinatufundisha kusaidia wenye uhitaji kama maagizo ya MUNGU ila sio kuwasaidia wengine ili tuje watumia kwa mahitaji yetu binafsi. Toa kwasababu umehurumia ila sio kwasababu unatafuta validation ya kupewa mahusiano.

Kwa kuhitimisha, kusimp hakuna uhusiano na ukarimu wa kiume au mwanaume anayejitoa kwa mwanamke kwaajiri ya upendo au mapenzi bali ni mapungufu ya kitabia na udhaifu kwa mwanaume.

Uhusiano bora ni two-way street ambapo wahusika wanajiwekeza kila m'moja kwa mwenzake kihisia, muda, kifedha, jitihada, thamani,na hata kiroho. Kuwa simp sio flex ya kiume ni red flag. The real flex ni kujiheshimu kiasi kwamba unaingia katika mahusiano bila kupoteza utu wako ili uonekane ni muhimu kwa mwanamke.

Don't simp it brings shame to your manhood and taint your personality.
 
images (8).jpeg
 
Bro you nailed it, hakika umetoa elimu kubwa sana,hope Ma home boys watajifunza kitu kikubwa sana
Shukrani sana brother. Lazima tujengane na kupeana elimu juu ya uhalisia wa maisha badala ya kuishi kinafiki.
 
Wanaume wanaoishi uanaume wao ni wachache sana na wamebatizwa majina mabaya kama mabahili, wakorofi, wakoloni.

Mwanaume lazima upambane kusimamia principles zako za maisha bila kuyumbishwa, vinginevyo wanao wa kiume utakosa cha kuwafunza na utaua uanaume wao.
 
Shukrani sana brother. Lazima tujengane na kupeana elimu juu ya uhalisia wa maisha badala ya kuishi kinafiki.
Kweli kabisa leo nilikuwa na home boy mmoja anakula cha arusha,akaniambia big brother mimi huwa demu akiniomba hela huwa namwambia nipe mda kidogo kwasababu umenipa taarifa leo

Akaendelea kusema yeye haoni baya kumwambia demu 70,000 unayotaka Sina hapa kuna 30,000 tu
 
Wanaume wanaoishi uanaume wao ni wachache sana na wamebatizwa majina mabaya kama mabahili, wakorofi, wakoloni.

Mwanaume lazima upambane kusimamia principles zako za maisha bila kuyumbishwa, vinginevyo wanao wa kiume utakosa cha kuwafunza na utaua uanaume wao.
Very true. Na jamii imeshape mentality za vijana na mabinti kuamini kuwa kijana anyesimamia misimamo yake basi hafai kwaajiri ya mahusiano na pengine ana matatizo ya kiakili.

But huwa nawapanga madogo kuwa wasiendekeze sana maoni ya watu kwasababu wanapofeli hakunaga mtu katika jamii atakuonea huruma wala kukukinga ila watakushambulia na kukusema vibaya.

But ukisimamia misimamo yako,kila mtu katika jamii atafuata njia yako na hiyo misimamo. Ni ngumu sana kuwin haya maisha bila principles.
 
Kweli kabisa leo nilikuwa na home boy mmoja anakula cha arusha,akaniambia big brother mimi huwa demu akiniomba hela huwa namwambia nipe mda kidogo kwasababu umenipa taarifa leo

Akaendelea kusema yeye haoni baya kumwambia demu 70,000 unayotaka Sina hapa kuna 30,000 tu
Na hata wanawake ukiwa hivyo anaheshimu kuliko ukiwa unazitoa tu anajua unazo nyingi atazichezea.
 
Naona hii wikiend ni ya kuwapa simp za uso. Mungu akitujalia uzima kesho nami nitaandika chochote kuhusu hawa masimp
Nilitoa ahadi ya vita kwao na nilishawaambia kama wapo tayari waunge majeshi na mafeminist na masingle mother waje pamoja vita vitapigwa pande zote kama mjerumani wakati wa vita vya pili vya dunia.

Hakuna kuwapa nafasi ya kupumua.😂
 
Ngoja tutest degree zetu za saikolojia tulizosomea the the university of Google na masters tulizosomea the university of hard knocks.

Hawa wafuasi wa kina Andrew Tate ni hawa:

You gave your all to someone who betrayed you in the end. Now you hate yourself for being so giving and think it's weakness,

and are now looking for a victim to re write the story: this time you won't be weak, this time you'll be the one making someone else feel weak.

Superman weweee. Batman huyooo. Hulk himself! ! ! Look at you Goliath!

I almost started writing a remedy for this then I remembered it's useless.

Endeleeni kuteseka.
 
Kwanini msiachane na wanawake mkafanye mambo mengine? ?

Daily wanawake this wanawake that.

Ni kama wale wakana Mungu, haamini Mungu but he talks about him all day everyday hadi anakufa :2Head:
 
Embu jaribuni for a second, cancel women.

Don't talk about them, or to them. And anyone who deals with them dont talk about them.

You will have a new world with no women!

Just Alpha males roaming around with biceps, mnapishana tu barabarani mnatunishiana misuli, mrudi majumbani kwenu mpost jinsi ya kupata misuli mikubwa zaidi.

Repeat till death.

Oh msisahau kutafuta hela na kutununiana Hela.

Hadi raha, just a world full of happy rich men with the biggest biceps.
 
Big five master, hii natamani iwe published kila jinsia ya kiume ione.
Nimesoma uzi wa jamaa nikamkumbuka demu mmoja alikuja ofisini kwa muda tu nikampokea vizuri kama mgeni siku kama tatu nne ivi nikawa namsave chai na chakula cha mchana basi baada ya hapo nikamkaushia nikawa napiga chai na lunch kama kawaida bila kumjari sasa sijui alidhani endelevu basi kuna siku akaniomba hela ya chai nikamwambia vipi bado hujajipanga? eti akakasirika na ukimwangalia kuna muda anaongea na mshikaji kama mtu wake ivi. Siku uliyofuata akajitutumua akapiga chai fresh bila kuhitaji kitu kwangu lakini baadae usiku wake akaniandikia sms eti mbona siku unanikataa Sana nimekukosea nini? nikamwambia hamna ulichokosea tuko pamoja kesho yake akanikalisha akawa analalamika oooooh nilipofika ulikuwa unanijali saivi sijui inakuwaje mimi kwa haraka nikaona labda ananitaka usiku wake nikamwomba mzigo akawa anazunguka kama hataki ivi nikasema hapo ndio umebugi nikamkaushia sikumwambia chochote tena nikawa bize na mambo yangu tu namwona yuko anahangaika kunisalimia asubuhi lakini mimi hata sms najibu nikisikia
 
Back
Top Bottom