Kijana ukioa tu lazima wazee wa "Kitonga" wamchukie mkeo tu, chunguzeni

Kijana ukioa tu lazima wazee wa "Kitonga" wamchukie mkeo tu, chunguzeni

2019

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2018
Posts
3,130
Reaction score
4,735
Nimechunguza mengi sana ndani ya ndoa. Kabla hujaoa ulikua huru kwenda na kurudi muda wowote na tabia za kibachela. Ndugu jamaa walikua huru kukuomba na kuwasaidia bila vikwazo vingi.

Ukishaoa kijana lazima ubadilike ili uendane na mwezio, yaani uache tabia ulizokuwa nazo unaze kuishi kutokana na chama kipya.

Huezi tena kuchelewa nyumbani sababu ya kuwa na marafiki mkinywa, una majukumu huwezi kutoa misaada sawa na mwanzo tena.

Wakati yote ukifanya wale waooote wanufaika wako, ndugu, jamaa na washkaji wanaona kabisa sababu ya mabadiliko yako ni mkeo.

Kwa hiyo wanabaki na wazo MKEO MBAYA, ANA ROHO MBAYA,AU AMEKUKALIA.

Jambo lipi jema, kuishi na familia yako vizuri au kukosana na familia kisa watu wengine?
 
Tatizo unashindwa kutofautisha kati ya kusaidia na kutapanya. Hakuna mke atakayekuzuia kusaidia wahitaji. Ukiona anakuzuia basi huyo siyo mke ni mchumaji. Lakini pia hakuna mwanamke atakaye mvumilia mwanaume anayetapanya mali kwa kisingizio cha kuwafurahisha ndugu na marafiki.
 
Huwa mnajitahidi kuwa kama malaika kwa muda mfupi sana ila mnajisahau na kurudi kule mlikotoka hapo ndo na wanawake wanayakumbuka makoloni yao ya ujanani.

Tatizo ni moyo.
Mpaka kufikia hatua ya kusemwa ina maana ni muda umepita,kwa kipindi kifupi bado haujajulikana una majukumu
 
Tatizo unashindwa kutofautisha kati ya kusaidia na kutapanya. Hakuna mke atakayekuzuia kusaidia wahitaji. Ukiona anakuzuia basi huyo siyo mke ni mchumaji. Lakini pia hakuna mwanamke atakaye mvumilia mwanaume anayetapanya mali kwa kisingizio cha kuwafurahisha ndugu na marafiki.
Kweli mke akukatazi kunywa, unakunywa kwa kiwango na muda maalum ili uwahi nyumbani, marafiki wanaona unamwogopa mkeo, je ni sawa?
 
Kweli,mke akukatazi kunywa, unakunywa kwa kiwango na muda maalum ili uwahi nyumbani, marafiki wanaona unamwogopa mkeo, je ni sawa?
Hiyo kampani huendani nao. Huwezi kuwa na kampani ambayo mna mitazamo tofauti. Kama ni kunywa kanywe vijiwe vya wastaarabu utapata marafiki mnaoendana.
 
Hiyo kampani huendani nao. Huwezi kuwa na kampani ambayo mna mitazamo tofauti. Kama ni kunywa kanywe vijiwe vya wastaarabu utapata marafiki mnaoendana.
Ukibadili kampani ndio kabisaa watajua umewatenga na mkeo ndio amekuamuru uwatenge. Watazidi kumchukia zaidi
 
Sasa ndiyo umeoa unakaa kijiweni unapiga ulabu mpaka saa 8 huyo mke kwao nakuacha kitanda? Ukioa huku umekomaa akili wala haimpi shida na marafiki, misaada kwa ndugu lazima ipungue tu hata iweje, ukiwa mwenyewe unaondoka tu unaweza kula mbele kwambele, lakini kama kuna mke nyumbani lazima uache mahitaji sasa hapo akili kichwani mke aachwe bila mahitaji lakini ukawasaidiye ndugu huko na wengine hawana matatizo yeyote!
 
Asante kwa kujazia, na ni vizuri kutimiza majukumu hayo yote ila mkeo anachukiwa utafanyaje?
 
Asante kwa kujazia, na ni vizuri kutimiza majukumu hayo yote ila mkeo anachukiwa utafanyaje?
Huwezi kuwaridhisha watu wote, kuna watu hawana jema hata moja, kuna mtu mmoja alikuwa akitoa misaada kwao kila mara na siku zote, wakati mwingine hata mkewe hamshirikishi, sasa maisha yakabadilika pesa hakuna, lawama zote zikamwangukia mkewe ndiye mchoyo ndiyo maana hasaidii familia, kwa hali hiyo utafanyaje kama si kuachana nao?
 
Hafu anatokea fala anasema nioe.

Maziwa napata, nyama napata, mbolea napata, sa nifuge ng'ombe wa nini aniletee ma Inzi Tu.
🤣🤣🤣Kuna faida bhana ww hujui tu
 
NIWE MKWELI. KATIKA UJINGA AMBAO SITAKUJA KUFANYA KATIKA MAISHA YANGU NI KUWA NA RATIBA YA KURUDI KWANGU KISA KUOA.

Yaani nianze kuwa naangalia saa kuangalia kama masaa ya kwenda nyumbani yamefika?? HUO UPUMBAVU KWANGU NOOO!!!
 
Huwa mnajitahidi kuwa kama malaika kwa muda mfupi sana ila mnajisahau na kurudi kule mlikotoka hapo ndo na wanawake wanayakumbuka makoloni yao ya ujanani.

Tatizo ni moyo.

Umejibu kama umekunywa K vant ya kichina.[emoji1787][emoji1787]

Lunatic [emoji2957][emoji2957][emoji2957]
 
Nimechunguza mengi sana ndani ya ndoa. Kabla hujaoa ulikua huru kwenda na kurudi muda wowote na tabia za kibachela. Ndugu jamaa walikua huru kukuomba na kuwasaidia bila vikwazo vingi.

Familia yako ni Watu wa kwenu Siyo mke wako
 
Back
Top Bottom