Ndio hivyo japo watu watazunguka kule na huko lakini ukweli ndio huo!Kweli nilikutana na bibi mmoja kule Kyela nikamuuliza mbona unapenda ccm akasema sio naipenda na wala siipigii kura natafuta pesa tu. Wakati wa Uchaguzi alipata jumla elfu 80 za hapa na pale kama hongo
Wanavyuo wanajua hasa wa pale kanda ya kati Dodoma jinsi wanavyopata pesa ya kula kupitia wabunge wa CCM kipindi cha bunge.
Kijana akishanufaika na CCM inabidi akitetee kwa nguvu zote kwa sababu anajua ananufaika nacho.
Uchaguzi wa mwaka 2010 & 2015 vijana wa upinzani walijitolea kuwa mawakala sehemu fulani. Vijana wale walikuwa mawakala bila kulipwa chochote na kushinda njaa tangu asubuhi mpaka usiku ilimradi tu kuhakikisha zoezi la uchaguzi linaenda sawa. Kwa upande wa CCM wao walikuwa wanawapelekea mawakala msosi wa maana na posho za kutosha kwa mawakala wao.
Kiukweli moyo ule ungeendelea kwa vijana wale wa upinzani Tanzania ilikuwa inaenda kukombolewa. Sema bwana yule akaja kupiga spana na kuwadhoofisha vijana, hivyo kuwa machawa ili wapate pesa mana njaa kali, huku wengine wakihofia usalama wao. Hii ni baada ya bwana yule kugundua udhaifu wa Mtanzania ni woga, na jamaa alikuwa hatanii, ukizubaa anakumaliza kweli!