Kijana Unawezaje kuishi Dar bila kufika bar ya "Mama Kamche"?

Kijana Unawezaje kuishi Dar bila kufika bar ya "Mama Kamche"?

Sisi wazawa wa dar es salaam na hasa watoto wa mjini..kwa kawaida baada ya mizunguko yoote na stress za mjini jioni tunajumuika kwa mama kamche pale mwenge kupata moja moto moja baridi.

Hapo ndipo tunakutaga na wadau wote wa mjini kuweka mambo sawa.
Kuna siku gari likiacha njia lazima liwaparamie,mama kamche choo chafu na finyu
 
mi nimezaliwa dar.. nimesoma dar, na ajira dar.. ila sipajui hata kwa mama kamche ndio wapi

je ni bar nzuri kuliko tips, havoc, governor, high spirit etc??

je kuna malaya wengi kuliko corner bar au kimboka?

je kuna mziki mzuri kuliko element au next door?

je kuna upepo mwanana kuliko slip way?


je kuna msosi mtamu kuliko mandi almaida lumumba au kwa sele bonge?
Ni Bar ya kawaida sana sema ina wateja na inafikika kirahisi ipo Mlimani Kwa Mbele kidogo.Vyoo vyake vichafu
 
mi nimezaliwa dar.. nimesoma dar, na ajira dar.. ila sipajui hata kwa mama kamche ndio wapi

je ni bar nzuri kuliko tips, havoc, governor, high spirit etc??

je kuna malaya wengi kuliko corner bar au kimboka?

je kuna mziki mzuri kuliko element au next door?

je kuna upepo mwanana kuliko slip way?


je kuna msosi mtamu kuliko mandi almaida lumumba au kwa sele bonge?
Almaida lumumba,nikikanyaga dar lazima nikawatembelee wasomali
 
Pale mnaenda kula “mkuu wa meza” na hakuna cha ziada zaidi ya hiyo kitu. Hakuna hewa, hakuna nafasi za kutosha na kimsingi hapana hadhi. Ni mara 100 mtu ashuke mpaka Calabash au across over aende Catalunya
 
Hahaaa mkuu acha kututisha ile miti itatukinga na hayo magari bhana, pale napenda kwa ajili ya mdudu na kulipa kodi
 
Hapo kwa mama kamche mkienda acheni magari hata sheri mwenge chukua zako bajaj..watakuvunjia kioo wajue una laptop kumbe begi tu lina documents za muhindi
 
Wee kamche ni mjanja sana. Ile mbege ijumaa usisahau
 
Back
Top Bottom