Kuna Jamaa wako kwa Mahusiano lakini Hawajui hata yanahusiana nanini mahusiano ambayo sio yenye Afya kwao.
Leo nawasaidia kwa huu Uzi, hili liwafanye kabla hujajiruhusu kumfanya Mwanamke awe wa kudumu , basi uwe tayari umeshajua Hatima yako.
Wanaume baadhi tunachopungua ni uwezo wa Kuitabiria wakati ujao ... Tunaenda enda, kufanya matumizi mabaya ya Pesa, Muda,Hisia , Uwekezaji, Bila kujua wanawake tulonao ,HAWATUFAI,na sababu HAWATUFAI, siku wakituacha tunaanza kulilia na kuwaza juu ya Pesa, uwekezaji tuloufanya n.k
Sasa basi, Kama unahuyu Mwanamke, au bado yuko kwa nje ya 18 na unamuhitaji kwa Kufanya naye Maisha ....... Chukua Hatua mapema UMUACHE ,kama hujapiga na nia ni kupiga basi Piga sepa ...waachie wazee wa makazi!!
[emoji117]AINA YA "CHANGU NI CHANGU".... Hujawah kutana na Mwanamke Mahali, au Kusikia, au kuongea naye au tu humu JF kwenye maandiko anasema " Mimi Changu ni changu ", pesa yangu ni yangu"?????......... Yaaan maana yake ni Mbinafsi wa maisha yake , wewe ndio unayetakiwa kua mpiganiaji wa pendo lenu, kwamba yeye anachoona kinafaa ni vile anavyokupa Mzigo tu .... Achana na huyu Demu Broo Hakufai, Mwanamke makini atakua supportive kwako , utaona kuna mahali Pesa yake inawajibika kwako.
...Usidanganywe na maneno ya " Sisi wanawake tumeumbwa kupokea "....wanawake ni wajanja sana katika kucheza na Saikolojia ya mwanaume, kabla hajakupiga mzinga atakufanyia kitu ambacho ama kinajarib kushusha uanaume wako, au kufanya uwe juu....ili wewe katika Kuthibitisha anachokisema ,YEYE AFAIDIKE....yaan wee Mwanaume unakua like " Ngoja sasa nifanye ndio ujue Nina PESA[emoji23]"..
[emoji117] AINA YA " MIMI BADO SIKO TAYARI". ni demu wako right? Alafu unamkubali kinyama, lkn kila unapozungumzia suala la KUMUOA,, majibu anayokupa ni 'Mimi bado sijawa tayari'..., achana naye , Unapoteza muda wako ... Amewapanga , bado anajaribu kuangalia ni wapi apumzikie, Huyu Hawapendi wote mnaomla.
[emoji117]AINA YA " MWENYE KUJUA KILA KITU,MWENYE KUJIONA YEYE YUPO SAHIHI TU "
Ujuaji naozungumzia niule mpaka wewe mwanaume unajihisi Husikilizwi, huheshimiwi ,Demu yeye ndio anayejifanya yupo sahihi kila kitu, mbishi kwa jambo lake ,akisema kasema jambo,na anataka liende ivo, yeye muda wote anataka aone umemfanyia lilo zuri . Acha kujisumbua, Ondoa mipango ya kudumu, Usiweke makazi.... ukikomaa ,Ndoani utakipatapata.
[emoji117]ASIYEFANYA IBADA.
yaaan hili lizingatie sana, Kuna umri mwanamke kama alikua starehe anatakiwa kuacha, kwa sababu kagonga 35, 40 , sasa huyu ikiwa kwenye miaka yake 20--30, Kufanya IBADA ni Sifuri , kwa Dini yake lkn Hata kanisan hamnaaa, Msikitini hamnaaaaa ... TEMANA NAYE ....NI najua hapa watakuja na hoja za "kuna wanaosali lkn ovyo, kuna sijui nn"..... Achana na hayo maneno ya WANAWAKE DHAIFU ,kumbuka Mwanamke ni mjenzi wa Familia yako, unapokua umeenda Congo kikazi, miezi miwili. Ni yeye, Wa kufanya wanao wakue na tabia gani......USIJE KUTHUBUTU KUFANYA NDOA NA MWANAMKE ASIYEFANYA IBADA.... NALIKAZIA HILI, KATIKA DUNIA YETU ILOKWISHA MAADILI, USIJE KUTHUBUTU KUOA MWANAMKE AMBAYE MAISHA YAKE YOTE, HAWEZ KUSHIKA KITABU KITAKATIFU KUSOMA HEKIMA, NA KUFANYA IBADA..
Hata kama wewe mwanaume ni MLEVI , NARUDIA USIJE OA MWANAMKE ASIYE NA IBADA.
[emoji117]AINA YA " ASOJIAMIN ,ASOJIONA YUKO SALAMA MIKONONI KWAKO.
MTU anaweza niambia ohoooo anakupenda ndio maana, ...hamna kitu kama hiko, Demu hapendi Uone umesimama na Mwanamke, hapendi uwe na Marafiki wa kike, hapendi hata kazin kajikuta anakufanyia Visa kwa wanawake wenzio, Simu zako anapokea kama ni mwanamke anatukana tukana na majibu ya ovyo, Ukichelewa pokea simu maneno, uko na Mahawala zako, unafanya uhuni, Demu aki shika simu zako nikwenda kwa mafail ya meseji tu... Huyu ni INSECURE WOMAN .....Insecure woman is not smart , is not beautiful..HAFAI.
[emoji117]AINA YA"MPENDA VITU" .. Hawa ni wale Madem ambao Wa napenda vitu sana kuliko kupenda masuala mengineyo kiakil, kijamii , yaan yeye anachotaka awe na kila kitu chenye kupendeza machoni kwake, ni kweli tumeumbiwa kupenda vitu, ila amini nakuambia, Mwanamke mpenda vitu ,Moyoni mwake haupo,kwa sababu ile nafasi yako imekua replaced na vitu vimpendezavyo , na Hajali , hajali pesa zako, anachotaka ni kitu anachokitaka... ACHANA NAYE CHAP.
[emoji117] AINA YA "CHA WOTE ,MUDA WOTE ".... Yaaan Sungura mjanja, huyi mwanamke ana flirt na kila mwanaume yaan she is there ..anytime, unajua yeye anakuambia " Asilimia 100% napenda kua karibu na jinsia Me "... ... Ngoja nikuambie kitu, MWANAMKE ANAYEJITAMBUA, ANA MIPAKA YAKE BUANA" akishajua now yuko kwa mahusiano thabiti, kama alikua wa muda wote , basi anajipa mipaka, na anajipa ili tu akuondolee wakati mgumu ndani ya macho yanayomtizama yaan ile "Huyu dem kachumbiwa lkn daaahhh wahuni wanambeba tu".
[emoji117]AINA YA " MWONGO"... nyie mlishawah kutana na mwanamke Mwongo?? Yaaan ule uongo asokua na Faida....unajua kuna uongo wa " Niko Njiani kuna foleni nipe dakika 30 ".... Kumbe mwanamke kwanza kapita saloon ili aje kapendeza.....huu kawaida.
Sasa kuna ule uongo yaan mwanamke muongo muongo tu akiahidi atekelezi, unajikuta .mpaka umeacha kuamini lolote toka kwake....ACHANA NAYE.
[emoji117]AINA YA " MTUMIAJI PESA "... ulishawah kutana nawanamke anapenda mspend tuuu mahela ?? Alafu maajabu kwenye kuspend koteeeee yeye hachangii hata mia ???? Basi ndo huyu mwanamke nayemsemea, ukiona demu ulonaye ni mtumiaji tu wa pesa zako, yaaan Hataki umuinie nayeye awe na pesa zake, ika a nachotaka ni " Nitumie Laki tatu hapo basi "..... Kuna kitu nmekiona twende uninulie .... Vipi Jpl tuingie kiwanja X .... Yaaan yote kwa yote ni Pesa yako tu ndio inayotumika , ACHAA, PIGA CHINI KAMA UMESHAPIGA MZIGO.
Uchaguzi ni pamoja na kuchanganya na zako ... Ila huo ndio ukweli halisi wa mambo yalivyo.
#Stuka siku hizi wanaingia kwako kwa hesabu zao za kibinafsi Japo kua wanakua hawajakupenda.... Umeyagundua hayo ,then usimtreat kama Malaika, kwa sababu vyovyote vile ufanyavyo HATOKAA KUA MWEMA WA KUFAA KIASI CHAKUA MKEO.