ChekoFagia
Senior Member
- Sep 20, 2025
- 115
- 339
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- Maendeleo ya Vijana, Joel Nanauka ameendelea na ziara yake maalum ya kukutana na kuzungumza na vijana katika Mkoa wa Ruvuma ambapo ameonya dhidi ya watendaji wa serikali wanaokwamisha shughuli za vijana kuwa hawatavumiliwa.
Akiwa wilayani Songea leo Ijumaa tarehe 28 Novemba 2025 amekutana na vijana wajasiriamali wanaofanya shughuli katika Soko la Bombambili na Stendi ya magari ya Ruhuwiko ambapo amesikiliza mawazo na ushauri wa vijana ikiwemo kutatua kero.
Katika mazungumzo hayo vijana wa Manispaa ya Songea wamelalamikia ucheleweshaji wa upatikanaji mikopo kutoka Halmashauri, mazingira yasiyoridhisha ya kufanyia biashara ikiwemo kero ya tozo na ushuru.
Waziri Nanauka amewaeleza vijana hao kuwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan anayo dhamira ya dhati kuona vijana wanashiriki kikamilifu kwenye ujenzi wa nchi hivyo kuwasihi waitunze amani na kutumia njia ya mazungumzo kutatua changamoto ndio maana akaamua kuundwa kwa wizara maalum ya vijana.
Katika hatua nyingine, Waziri Nanauka amewataka viongozi wa mkoa na wilaya kuweka utaratibu wa kutoka ofisini na kuwafuata vijana walipo ili kusikiliza hoja na kero zinazowakabili.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Songea Wilhelm Ndile amesema wamepokea maelekezo na kwamba wataratibu vikao na wajasiriamali vijana pamoja na waendesha bodaboda ili kuzitafutia suluhisho changamoto walizozitoa kwenye ziara ya Waziri.
Kijana Arnold Mgawo wa Bombambili amesema anapenda kuona Rais Samia Suluhu Hassan anadhibiti vitendo vya utekaji na kupatikana kwa demokrasia ya vijana kuzungumza.
Omary Amad pia kutoka Bombambili amesema aliomba Serikali iweke utaratibu nzuri wa utolewaji mikopo ya Halmashauri ili vijana wengi waifikie kwa urahisi bila vikwazo.
Naye Benedict Tembo amemshauri Waziri asikubali kusikiliza watendaji wake kwa kuwa baadhi hawasemi ukweli kuhusu changamoto za vijana na badala yale achukue hatua kwa wazembe.
"Wewe ni Waziri mpya wa vijana, watakaokuangusha ni wafanyakazi wanaokusaidia kutekeleza shughuli. Mama Samia ana lengo zuri na watanzania lakini wanaomharibia ni wafanyakazi wanaoshindwa kutatua kero za Vijana" amesema Tembo.