Narcissist_saint
New Member
- Sep 28, 2015
- 0
- 1
“Kwa kuwa sisi wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumeamua rasmi na kwa dhati kujenga katika nchi yetu jamii inayozingatia misingi ya uhuru, haki, udugu na amani. Na kwa kuwa misingi hiyo yaweza tu kutekelezwa katika jamii yenye demokrasia ambayo serikali yake husimamiwa na bunge lenye wajumbe waliochaguliwa na linalowawakilisha wananchi.
Hivyo basi, katiba imetungwa na bunge maalum la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa niaba ya wananchi, kwa madhumuni ya kujenga jamii hiyo, na pia kwa ajili ya kuhakikisha kwamba Tanzania inaongozwa na serikali yenye kufuata misingi ya demokrasia na ujamaa.” Kwa kunukuu utangulizi huu naona umuhimu wa bunge katika nchi yenye chachu ya maendeleo ya jamii zetu.
Hivi karibuni ni aibu sana kuona muhimili huu unavyoyumba, kwanza kwa kushindwa kutimiza wajibu na hata kutokuwa mfano mzuri kwa wazalendo wengine wanao wakilishwa bungeni. Napata wakati mgumu kuelewa ilivyokazi ngumu kwa walimu kutoa mifano wa viongozi wa muhimili huu madarasani kama ambavyo sisi tuliwasikia kina Mhe. Pius Msekwa na Sokoine katika utumishi, ni aibu. Ila najipa moyo naiona kesho nzuri kuliko leo kwa Maisha ya kijana ninaewaza.
Je, huyu Mbunge wangu aliye katika muhimili huu anamkumbuka bosi wake ama wajibu uliompeleka? Labda hakumaanisha alichosema kwa kuwa ulikua mchongo alioufukuzia tangu kitambo? Mchongo flani ulionona kwa mambo kama kulipwa 3.8mil Tsh kwa mwezi kama mshahara, Posho za vikao na za kujikimu zinazokaribia Laki 3 na elfu 40, Mchongo wamilioni 90 kwa gari lenye hadhi ya mbunge, Pia aliiwaza sana bima itakayo muwezesha kutibiwa ndani na nje ya nchi. Labda aliuwaza sana huu mchongo wenye mambo mengi ya kutamanisha.
Sasa, kama lengo sio kumtumikia mwananchi je, anafanya nini:
Pili, Mama zetu ambao ni mioyo ya familia anasubir kesho mchongo wangu utiki nimsaidie kubadili kesho kuliko ile ya kanga na tshirt kwenye kampeni.
Pia, Baba ambae ni kichwa cha familia anajitahidiwadogo zetu misingi bora ya kitanzania anashindwa kwa kuwepo tuhuma, kashfa na ugaidi anaovikwa.
Mwisho mchongo uwe nafasi kuwatafutia katiba mpya, itakayo simamia Tanzania yetu kwa Imani yenye dhati inayozingatia misingi ya uhuru,amani, pia kwa ajili ya kuhakikisha kwamba Tanzania inaongozwa na Serikali yenye kufuata misingi ya demokrasia na ujamaa, ambao kama kijana mwenye michongo mingi Tanzania nijivunie na yoyote atakaechaguliwa kwenye mchongo huu nikiamini atajituma kwa ajili yetu sote, Watanzania.

- kushindwa kutimiza wajibu wake kama mfanyakazi kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri serikali ya jamhuri ya muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa sheria, ambayo haimfaidishi mwananchi daraja la chini ambae ndie anateseka sana. na kuunga mkono kwa asilimia kubwa miradi inayoongeza ustawi wa jamii zetu Tanzania. kama alivyo fanya marehemu mhe Samueli Sitta kuwa mfano mzuri wa kufuata sharia na kanuni bungeni ili kutimiza wajibu wake.
- Kuiambia serikali kuacha kununua ndege kwanza kujitathmnini kwa kukubali baadhi ya makosa na kuangalia eneo jingine ambalo litamfaidisha yule mpwa jimboni kwake ambae anapoteza uhai kwa kukosa huduma bora za afya, miundombinu na elimu ila anatamani sana ile story ya mama mjamzito na muuguzi wa afya isijisirudie maana ilimuumiza sana kama ambavyo alifanya Mhe.Tundu Lissu bungeni wakati akitumikia watu wa Singida Mashariki kuhusu mikataba ya madini katika kuchangia mapendekezo yake katika bajeti kuu ya Serikali kwa mwaka 2017/18 kwa kuiambia serikali mapungufu yao katika sekta hiyo nadhani kumbukumbu zitakuwepo kilichotokea wakati huo akipigania maslahi ya mtanzania.
- Ikiwa lengo limebadilika anashindwa vipi kufanya kama kamanda, Aliyekua na mchongo wake Arusha mjini, kusimama bungeni nakuhoji magumu katika matumizi ya serikali na bunge kama vile ilivyokuwa katika kipindi cha kujadili mapitio ya mapato na matumizi ya fedha za ofisi ya Waziri mkuu na ofisi ya bunge kwa mwaka wa fedha 2017/2018, ni aibu sana kwa sasa kuutolea mfano muhimili huu unaoyumba.
- Wasimkandamize yule mama atakae nipigia vigeregere wakati wa kampeni , kwa kuwa ana familia inayomuangalia yeye pia kijana chuoni anamtegemea kwa mahitaji yote kwa kukosa mkopo. Wasimuangalie sana bosi wangu huyu maana kipato chake kinanufaisha wengi tusimuonee sana kwa kumuongezea makato yaliyo onevu ya tozo ya ongezeko bei katika bidhaa na huduma inakua ni kumuonea sana.kama vile ilivyokua kwenye miamala ya simu Kwa kila muamala , isidhurumu mama huyu , kwa kutaka kutimiza sera za serikali anmbazo ni zile zile zinazorekebishwa kila chaguzi. Wao wanae mtetea ni yupi? Au yule kijana mwenzangu atakae piga kura, Anae umia moja kwa moja pindi anapomjali mama huyu alieteseka kumsomesha, Ila anashindwa kwa sababu ya Athari za kiuchumi zinazoweza kutokea kama alivyojadili Mchambuzi wa Uchumi, Tanzania Ndugu Walter Nguma athari hizo ni kama Kuzorota kwa biashara za mitandaoni, Mzunguko wa fedha kudorora,nk
- Anipishe mimi kijana mwenye mchongo wangu bungeni nikaikumbushe serikali na bunge kabla hawajaangalia namna ya kumkandamiza kazini au kudhurumu baba zetu kwa kuwacheleweshea na kutowalipa stahiki zao baada ya kustaafu, waniangalie mimi kijana mzalendo mwenye mchongo wangu bungeni nitakae pigiwa kura na huyu baba anaeangaika nije nipambane kumpunguzia mzigo wa Maisha magumu, kwa kuhakikisha serikali inanipa haki ya uzalendo kwa taifa langu kwa kuniwekea kodi katika kifurushi changu cha mishahara na posho, ikatumike kutimiza ilani na baadhi ya ahadi zetu, kwa bibi zetu kule kijijini kuhakikisha nchi inaendelea katika misingi ya waasisi wa taifa letu na kuwa mfano mzuri kwa kizazi kinachofata kuwafundisha uzalendo kama enzi za Hayati baba wa Taifa mwl. Julius kambarage Nyerere kwa viongozi kwa kutumia nguzo hizo kama mwanga wa kusaidia mihimili mingine ya serikali bila kumsahau baba mpiga kura kujivunia kuwa mtanzania.
- Anipishe niwahi kufikisha ujumbe wa dada angu kijijini, Nimrudishie tabasamu kwa kuamini nitafikisha kwa kulenga matatizo sugu yanayomkuta ikiwemo maji na mimba za utotoni,Anipishe mchongo wangu utiki, nikawe mwenye nidhamu kwa kufuata kanuni na sharia za bunge, kuwe na utulivu na ufuatiliaji wa karibu kwa miradiyote ya serikali hasa ya kijamii kwa kuhakikisha inakua bora kwa huyu mama mtarajiwa kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kumuwezesha kupata muda wa kufatilia elimu ya mwanae anaesoma shule ya kata ili atimize lengo la kufaulu na ahadi ya anko itimie, kumpeleka mbugani Serengeti kwa ndege kama bombardier ambazo alifundishwa na mwalimu wake kama ni fahari ya kila mtanzania kwa bei ya chini kama ilivyokua wakati wa kasuku, enzi anko alivyokata tiketi mapema akaangalie mechi ya simba na yanga.
- Anaeteseka ni yule mdogo wangu alieswekwa rumande baada ya kupiga kura akiamini mchongo ukitiki nitamtoa huko kwani hakua na kosa Zaidi kuunga mkono jitihada za kampeni za siasa na kuonekana sio mmoja ya wapenda maendeleo katika jamii na baadhi ya viongozo wa serikali waliolewa madaraka.
- Anayeumia ni yule mjomba polisi, aliyekula kiapo kutumikia nchi na jeshi la Polisi, kwa kulinda raia na mali zake, kumuongezea adui mwingine mtaani kwa kupewa amri ya kumkamata raia asiekuwa na kosa lolote bali ikiwa anatimiza haki yake ya kidemokrasia kuwepo na haki ya usawa, haki ya uhuru wa mawazo na haki ya kufanya kazi, kwa kulinda heshima mwananchi anaeteseka mtaani na marungu ikiwa katika jamii ni jirani, shemeji hata mtani wake alieenda kusikia sauti tofauti katika jukwaa la siasa.
Pili, Mama zetu ambao ni mioyo ya familia anasubir kesho mchongo wangu utiki nimsaidie kubadili kesho kuliko ile ya kanga na tshirt kwenye kampeni.
Pia, Baba ambae ni kichwa cha familia anajitahidiwadogo zetu misingi bora ya kitanzania anashindwa kwa kuwepo tuhuma, kashfa na ugaidi anaovikwa.
Mwisho mchongo uwe nafasi kuwatafutia katiba mpya, itakayo simamia Tanzania yetu kwa Imani yenye dhati inayozingatia misingi ya uhuru,amani, pia kwa ajili ya kuhakikisha kwamba Tanzania inaongozwa na Serikali yenye kufuata misingi ya demokrasia na ujamaa, ambao kama kijana mwenye michongo mingi Tanzania nijivunie na yoyote atakaechaguliwa kwenye mchongo huu nikiamini atajituma kwa ajili yetu sote, Watanzania.
THE END.
Narcissist_saint.
Narcissist_saint.