Kijana wa kiume unakuwaje chawa? Kuna shida mahala

Kijana wa kiume unakuwaje chawa? Kuna shida mahala

Pride au ego ni luxury kwa mwenye tumbo lenye njaa mkuu..

Ila kwa kiasi cha uchawa, sometimes natamani niwaelewe au nisiwachukulie tofauti Ila impact ya kile wanachokifanya, imeshaanza kuonekana na siku si nyingi itaripuka. Shortcuts shortcuts na kuwatia moyo watu kujizima data ili wapate kipato, haitoishia kwenye kusifia matajari, picha kamili litakuja tu
 
mimi mwenyewe sio chawa ila hakuna nilichosaidia kwenye uchumi wa nchi,,ila mimi ni (KE),,ila nmetoa mfano.
Acha walishe familia zao,nchi ina watu wake wa kuipa faida sio lazma wote.
sema watasaidia kwa kulipa kodi,tozo,bili za maji,kununua umeme........nk.
Ndio maana nakuambia kuna kazi nyingi za kufanya kulisha familia zao, uchawa sio option pekee..

Nguvu kazi ya taifa inapotea, uchawa kwenye siasa ndio unapelekea na wewe usitoe mchango wowote kiuchumi kwenye taifa, uchawa ni kupotoka, uchawa ni uongo, uchawa ni ukandamizaji.

Chawa wanasifu wanasiasa na kufanya kampeni zinazopotosha jamii, kusifu viongozi wanaokosea. Acha wasemwe hawana msaada wowote.

Kuhusu familia kila mmoja ana familia hata nyau ina familia.

Chawa wanakera, kazi ya chawa ni kuficha uovu, hatuwezi kuwa na taifa la namna hio.

Uchawa na ushoga havipo mbali.
 
Back
Top Bottom