Kijana wa miaka 15 kagoma kujiunga na form one kisa kijiweni kwao kuna wa degree zaidi ya watano wanaendesha boda-boda mgine anauza matunda

Covax

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2021
Posts
10,198
Reaction score
35,323
"Baba kama Pascal mtoto wa baba mkubwa amesoma degree ya uchumi anauza matunda barabarani na rafiki yake kasomea ualimu anaendesha boda boda kuna haja gani ya mimi kuenda kusoma wakati naweza kufanya hizo kazi hatakabla ya kujiunga na sekondari......"
hiyo ndo hoja aliitowa mtoto alio maliza darasa la saba mwaka jana na kufauli kwa Grade A. kwa Baba yake mzazi ambaye ni mfanya biashara.

Kuna wimbi la wapotoshaji kurubuni watoto wadogo kwa kubeza elimu yetu kwamba haina manifaa kusoma ni kupoteza mda kwasababu ya mifuano michache wanao taja kwa wale walio shindwa kupata ajira.

Jamani elimu ina umuhimu wake, nyie Boda boda acheni kupotosha watoto na vijana kwa kutaja mifuano ya uongo, mtu ambaye hajaenda shule hata kama wote wana endesha bajaji hawalingani, ambaye hajaenda shule akikosa ajira maisha yanakua magumu kwake mara mbili ya yule alioenda shule.

"Elimu ni zaidi ya ajira"
 
Vipi wale wa degree ambao wamepata mafanikio hawakuwaona pia? Katika jambo tulilofanikiwa katika jamii yetu sisi ni kuwaepusha watoto wetu na vijiwe
Mkuu hongera kama unaishi uzunguni ila kwetu watoto wetu wanachangamana na watoto wa waendesha boda boda, huwezi kuepuka vijue vyao kwasababu wana sindikizana kuenda kwa baba zao
 
"Baba kama Pascal mtoto wa baba mkubwa amesoma degree ya uchumi anauza matunda barabarani na rafiki yake kasomea ualimu anaendesha boda boda kuna haja gani ya mimi kuenda kusoma wakati naweza kufanya hizo kazi hatakabla ya kujiunga na sekondari......"
hiyo ndo hoja aliitowa mtoto alio maliza darasa la saba mwaka jana na kufauli kwa Grade A. kwa Baba yake mzazi ambaye ni mfanya biashara.

Kuna wimbi la wapotoshaji kurubuni watoto wadogo kwa kubeza elimu yetu kwamba haina manifaa kusoma ni kupoteza mda kwasababu ya mifuano michache wanao taja kwa wale walio shindwa kupata ajira.

Jamani elimu ina umuhimu wake, nyie Boda boda acheni kupotosha watoto na vijana kwa kutaja mifuano ya uongo, mtu ambaye hajaenda shule hata kama wote wana endesha bajaji hawalingani, ambaye hajaenda shule akikosa ajira maisha yanakua magumu kwake mara mbili ya yule alioenda shule.

"Elimu ni zaidi ya ajira"
Kashauriwa ama kuchukua maamuzi mabaya mno.. Slimy si kwa ajili ya kuajiriwa bali ni kukupa ufahamu na maarifa ya kuweza kupambana na maisha katika njia bora zaidi
 
Ni kweli wengine tulisoma only to be able to fit in family and community sio kupata ajira, ila vijana wengi wasiku hizi wanasoma kupata pesa sio kuishi vizuri na maarifa katika jamii yetu, ndo wamefanya elimu kuonekana haina maana.
 
Tulikosea sana tulipoipa siasa thamani kubwa kuliko taaluma.. Haha ndio matokeo yake sasa
 
Siasa zetu ndo zimeua elimu yetu kama strategic plan ya kuendelea kutawala watanzania bila kua na upinzani wa dhati, unampa mtu wa darasa la saba ubunge watowe mawazo pamoja na professor uko bungeni, kweli kuna mtu atakae hrshimu hiyo elimu, if primary seven graduate can deliver the same intellectual work as a university professor so what is the relevance of education?
 
Huyu mtoto ni mjinga kuliko watoto wote duniani na nahisi hata mkoa anaotoka ni upi.
Akili yake inafikiri mtu anasoma ili aajiriwe
Ajiulize kwanini Mo Dewji baba yake alimpeleka shule wakati ni tajiri na pia ajiulize kwanini Mo Dewji amepeleka watoto wake shule wakati ni tajiri.
Ajiulize kwanini Reginald Mengi watoto wake wote ni Wasomi wakati hela ipo
Ajiiulize Dangote ana elimu gani.
Ukiwa hata una hela nyingi lakini hujasoma utajiri wako unakuwa wa kifala sana.
Aende mkoa wa Kilimanjaro ataona kuna watoto wana usomi wa hali ya juu lakini wanachoma nyama choma na wameajiriwa mahoteli makubwa wanaongea na wazungu na wanajua lugha nyingi za kimataifa.
Abaki na msimamo wake ila baadae atakuja kujuta sana
Naomba mungu asinipe toto la hivi
 
Mkuu toa hoja acha kutukana huyu kijana bado mdogo sanaa kuelewa jinsi maisha yanavo enmeshed, uko Kilimanjaro unako sema watu wote ni wasomi hakuna walio achia shule wakiwa darasa la saba?
 
Mkuu toa hoja acha kutukana huyu kijana bado mdogo sanaa kuelewa jinsi maisha yanavo enmeshed, uko Kilimanjaro unako sema watu wote ni wasomi hakuna walio achia shule wakiwa darasa la saba
Kilimanjaro wako walio ishia la saba ila ni kutokana na umasikini ila sio kukataa shule wakati mtoto amefaulu vizuri sana na baba ana uwezo wa kusomesha.Hili ni gonjwa narudia na ujinga kumuita mtu mjinga sio tusi tusi ni kumuita mpumbafu.
Halafu nikuambie hakuna mtu duniani asiyekuwa mjinga.Ujinga ni ile hali ya kutokujua kitu flani.Mfano kama hujui kuendesha ndege basi wewe ni mjinga kwa taaluma hiyo ila ukijifunza ule ujinga unakutoka.
mfano mwingine mimi hapa ni mjinga wa kutokujua taaluma ya umeme ila nikijifunza ujinga huo utanitoka
Sasa huyu kijana ni mjinga kwa kutokutambua umuhimu wa elimu akishatambua huo ujinga unamtoka
 
Back
Top Bottom