JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Tonny Kurwa Zuchu [18] Mkazi wa Misungwi Mwanza amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela baada ya kukutwa na hatia ya kuruhusu kuingiliwa kinyume cha maumbile.
Hukumu ya kesi hiyo ya jinai namba 91/2023 imetolewa Aprili 19, 2023 katika Mahakama ya Wilaya ya Mbarali Mkoa wa Mbeya mbele ya Mheshimiwa Hakimu Aliko Mwandumbi baada ya mshitakiwa kukiri kutenda kosa hilo.
Mshtakiwa alitenda kosa hilo Aprili 12, 2023 huko maeneo ya Klabu cha Songambele kilichopo ndani ya Wilaya ya Mbarali kinyume na kifungu namba 154 (1) (c) cha sheria ya kanuni ya adhabu sura 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2022.
Mshtakiwa alikuwa akitumia mbinu ya kuvaa gauni na sindilia na kujichanganya kwenye maeneo ya walevi (vilabu vya pombe). Mshtakiwa baada ya kusomewa shitaka lake, alikiri kutenda kosa ndipo Hakimu alitoa hukumu ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama yake.