Kijana wa namna hii tukimfukuza ni kosa?

simple sana,kama mmempatia hifadhi mkaamua hadi kumshirikisha kazi mnazofanya
maamuzi ni kubaki kuwa na hifadhi lakini ofisini hafiki.
 
Basi kulikua hakuna sababu za kuja kuomba ushauri humu maana kwanza, unajichoresha tu maana nyinyi ndio mnajuana huko so kwaiyo usitegemee kila mtu atakupa ushauri utakaoupenda au utegemea
 
Tumieni changamoto kama mtaji wa kuvukia usikubali kukosana kisa kawazidi ujanja na wewe tafuta mbinu kumzidi yeye ipo atakua na nafasi nzuri mtashindwa kisaidiana kwa kitu kidogo kama hiki
 
Huyo dogo asije akawa ni jamaa niliwahi ishi nae anaswaga hizo, nilikuwa namchukulia kama ndugu namnunulia hadi vocha, msosi kwangu kila kitu anapata utafikiri mtoto wangu, akanitongozea dem wangu bahati nzuri dem wangu akaniambia nikampotezea jamaa.

Baadae akaanzisha kunikopa hela tena kwa lazima et nimpe pesa, nikawa namkopesha kumbuka hapo anakaa kwangu, siku moja dem wangu kaja jamaa akaanza kuni mind, aisee tabia zilinishinda siku namtimua hakuamini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…