Engager
JF-Expert Member
- Jan 12, 2011
- 1,522
- 3,255
Kama kunamtu anauelewa au alishawahi kukutwa na hali hii naomba ushauri au experience yake.
Tuligundua mtoto ana mafindofindo yamevimba alipokuwa na umri wa miaka miwili. Tulijaribu kumtibu traditionally. Kuna dawa flani tuu ya kienyeji ya kuyachua kwa siku mbili yanakwisha yenyewe. Tumekuwa tukitumia njia hii tangu sisi tukiwa wadogo na tunapona. Ajabu kwa dogo iligonga mwamba. Hayakunyauka. Zoezi la kumchua tulilifanya kwa wiki kadhaa lakini hayakuisha..
Ilipita miezi kama sita, mafindofindo yamevimba vile vile. Tukaamua kumpeleka hospitali. Tukapewa dawa, tukaambiwa ikiisha bila kuonesha matokea, turudi tena. Dogo alitumia dozi ikaisha, yako vile vile. Tukarudi hospitali, tukabadilishiwa dawa bado hayakuisha. Tukashauriwa tumpeleke akafanyiwe upasuaji yaondolewe kwa njia hiyo. Huo ushauri sikuuafiki moja kwa moja.
Sasa hivi dogo anamiaka minne. Tumebadilisha dawa za kuchua mara kibao. Kila mwenye kudhani anaweza kusaidia, anatia utaalamu wake pale lakini mtoto kila ukimwangalia yapo tuu yamevimba vile vile. Kiasi nimeanza kuufikiria ushauri wa kumpeleka kufanyiwa upasuaji, lakini kunavitu vinanitatiza.
1. Tangu tumeyagundua, hakuwahi kuonesha dalili yoyote kwamba pengine yanamsumbua. Tunajua jinsi mafindofindo yakivimba yanavyouma, yanavyoumiza kichwa na kuleta vihoma homa, yanavyosumbua kumeza etc... lakini kwa huyu mtoto hatujawahi kuona mabadiliko hayo.
Mwanzo tulidhani labda anashindwa kuyatambua maumivu pengine sababu ni mdogo sana. Lakini sasa anamika mi4 walau anajua kuumwa kukoje na kuwa salama kukoje. Lakini ukimuuliza kama anaumia kumeza au makoo yanamuuma au kichwa anakataa, yaani hata kwa kumwangalia tuu unajua kabisa hapati taabu yoyote. Ila yapo. Yamevimba. Miaka miwili na sehemu sasa.
2. Muonekano wake. Hayaonekani kuwa na usaha au rangi ya kutatanisha. Yanaonekana kuwa na rangi sawasawa na ile ya kinywa chake tu ya kawaida. Ila yapo yamevimba. Kuna muda tunawaza au labda nae ni wa hivo hivo kimaumbile?!
Naona shida kubwa yanayo msababishia ni kwenye kupumua. Kunamuda akitulia, anapumua kwa sauti kama mtu aliye usingizini. Hii inatokea hasa usiku, sijawahi kumsikia mchana. Pia baadhi ya siku uwa anakoroma akisinzia.
Tatizo lingine ni kuugua mafua na kikohozi mara kwa mara. Mtoto hapitishi wiki mbili bila kuugua mafua, yakipona kikohozi kinapokea, kikipona anakuwa sawa chini ya wiki mbili anaugua tena.
Sina ushahidi wowote kama hayo matatizo yanahusiana moja kwa moja na mafindofindo aliyo nayo.
JF inawatu wengi, natarajia kupata chochote cha manufaa hapa kabla sijaamua kumpeleka kwenye upasuaji.