A
Anonymous
Guest
Tulipofuatilia suala hili tulielezwa kuwa kuna ratiba ya mgao wa maji, na tulipewa ratiba hiyo. Hata hivyo, siku zilizopangwa kwa mujibu wa ratiba hiyo maji hayatoki kabisa, jambo ambalo limeendelea kutusababishia usumbufu mkubwa.
Soma Pia: Wiki tatu bila maji: Wananchi wa Unyinga, Mamise na Unyakumi tunataka ufafanuzi kutoka SUWASA
Kutokana na hali hii, wananchi wengi wanalazimika kuchota maji kwenye madimbwi, hali inayohatarisha afya zetu na kuongeza ugumu wa maisha ya kila siku.