Wakazi wa Kijiji cha Manga, Mkoa wa Singida, tunaomba msaada wenu kuhusu changamoto kubwa ya upatikanaji wa huduma ya maji, tumefikisha takribani miezi miwili bila kupata huduma ya maji. Hata kabla ya kipindi hiki, maji yalikuwa yakitoka kwa kusuasua, mara moja tu kwa wiki au wakati mwingine hayakutoka kabisa.
Tulipofuatilia suala hili tulielezwa kuwa kuna ratiba ya mgao wa maji, na tulipewa ratiba hiyo. Hata hivyo, siku zilizopangwa kwa mujibu wa ratiba hiyo maji hayatoki kabisa, jambo ambalo limeendelea kutusababishia usumbufu mkubwa.
Kutokana na hali hii, wananchi wengi wanalazimika kuchota maji kwenye madimbwi, hali inayohatarisha afya zetu na kuongeza ugumu wa maisha ya kila siku.