KERO Kijiji cha Nabweko, Ukerewe hatuna umeme wa TANESCO wala maji ya uhakika tangu Uhuru

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Wananchi wa Kijiji cha Nabweko, kilichopo Kisiwa cha Irugwa, Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, tunaendelea kukabiliwa na changamoto kubwa za huduma za msingi.

Kwanza, tangu Tanzania ipate uhuru, kijiji chetu hakijawahi kufikiwa na huduma ya umeme wa TANESCO. Hadi leo, wananchi wanalazimika kutegemea umeme wa sola na jenereta, jambo linaloongeza gharama za maisha na kukwamisha shughuli za kiuchumi pamoja na maendeleo ya kijiji.

Pili, licha ya eneo letu kuzungukwa na maji ya Ziwa Victoria, huduma ya maji safi na salama ni duni sana. Mara nyingi hupita hadi mwezi mzima bila maji kutoka kwenye mabomba yaliyopo. Kutokana na hali hiyo, wananchi hulazimika kutumia maji ya ziwani kwa matumizi yote ya kila siku, hali ambayo inahatarisha afya zao na kuongeza hatari ya magonjwa ya mlipuko.

Tunaiomba Serikali na mamlaka husika kutupatia ufumbuzi wa haraka kwa kuhakikisha kijiji chetu kinapatiwa huduma ya umeme wa TANESCO na maji safi na salama. Huduma hizi ni haki ya msingi na ni muhimu kwa maendeleo na ustawi wa wananchi.
 
Mbunge wenu ni w chama cha upinzani? Kama siyo kazi na utu.
 
Mna mbunge, na diwani? Ikifika kipindi cha uchaguzi mnapewa kanga na baiskeli mnatamba nazo, wakishaondoka mnakuwa na majuto mpaka mitano ifike tena, endeleeni mbele
 
Habari, ndugu wateja wetu.

Kwanza, tunawaomba radhi kwa kuchelewa kuona taarifa yenu na kutoa mrejesho. Asanteni sana kwa kutufahamisha kuhusu jambo hili.

Tumepokea taarifa yenu na tutaifikisha kwenye idara husika ili ifanyiwe kazi kwa mujibu wa taratibu.

Tunaendelea kuwakaribisha kuwasiliana nasi na kutujulisha changamoto nyingine zozote zinazohusu huduma ya umeme mnazokutana nazo. Maoni na taarifa zenu ni muhimu katika kutusaidia kuendelea kuboresha huduma zetu.

Asanteni sana kwa ushirikiano wenu. GK
 
Tunaiomba Serikali na mamlaka husika kutupatia ufumbuzi wa haraka kwa kuhakikisha kijiji chetu kinapatiwa huduma ya umeme wa TANESCO na maji safi na salama. Huduma hizi ni haki ya msingi na ni muhimu kwa maendeleo na ustawi wa wananchi.
Kura tunawapigia na bado tunaomba wafanye kazi..... Maisha ya uanasiasa raha sana .. maana huna tofauti na mungu wa "duniani"..
 
CCM B watafuta uzi huu.
Na huu ndio ukweli wenyewe kabisa.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Wananchi wa Kijiji cha Nabweko, kilichopo Kisiwa cha Irugwa, Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, tunaendelea kukabiliwa na changamoto kubwa za huduma za msingi.

Kwanza, tangu Tanzania ipate uhuru, kijiji chetu hakijawahi kufikiwa na huduma ya umeme wa TANESCO. Hadi leo, wananchi wanalazimika kutegemea umeme wa sola na jenereta, jambo linaloongeza gharama za maisha na kukwamisha shughuli za kiuchumi pamoja na maendeleo ya kijiji.

Pili, licha ya eneo letu kuzungukwa na maji ya Ziwa Victoria, huduma ya maji safi na salama ni duni sana. Mara nyingi hupita hadi mwezi mzima bila maji kutoka kwenye mabomba yaliyopo. Kutokana na hali hiyo, wananchi hulazimika kutumia maji ya ziwani kwa matumizi yote ya kila siku, hali ambayo inahatarisha afya zao na kuongeza hatari ya magonjwa ya mlipuko.

Tunaiomba Serikali na mamlaka husika kutupatia ufumbuzi wa haraka kwa kuhakikisha kijiji chetu kinapatiwa huduma ya umeme wa TANESCO na maji safi na salama. Huduma hizi ni haki ya msingi na ni muhimu kwa maendeleo na ustawi wa wananchi.
Habari, ndugu mteja pamoja na wananchi wa kijiji cha Nabweko - Irungwa, Ukerewe, Mwanza.

Tafadhali fahamu kua mradi wa kusambaza umeme kwa kutumia nishati ya jua katika Kisiwa cha Irugwa, Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, unaendelea kutekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kupitia mpango wa kusambaza umeme katika visiwa.

Mradi huu unatekelezwa kwa awamu, ambapo katika hatua ya kwanza unahusisha vijiji vya Sambi na Nabweko. Jumla ya kaya 1,968 zinatarajiwa kunufaika na huduma ya umeme, zikiwemo kaya 872 za Kijiji cha Nabweko.

Mkandarasi wa mradi tayari ameanza kazi eneo la mradi na anaendelea na utekelezaji wa shughuli mbalimbali za ujenzi, kwa lengo la kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati na wananchi wa maeneo husika wanapata huduma ya umeme salama na ya uhakika.

Asante sana na usisite kuturudia kama unamaswali mengine kuhusu huduma zetu za umeme katika eneo lenu.
 
Back
Top Bottom