Mary Abely
New Member
- Jun 15, 2023
- 4
- 4
Katika kijiji kiitwacho Utawala Bora, watu walikuwa wakiishi katika hali iliojawa na machafuko, utata, na kutoridhika. Rushwa ilitawala, hali ya kutokuwa na usawa ilikithiri na sauti za watu hazikusikika (wananchi). Hatahivyo, katikati ya machafuko hayo, mwangaza wa matumaini ulijitokeza, mwangaza uliokuwa na miale mikali ya mabadiliko katika mioyo ya watu. Safari ya kuuendea utawala bora ikaanza kama ilivyokuwa jina la kijiji chicho.Safari ilianza na kikundi cha watu wachache wenye nia na dhamira waliopata maono ya maisha bora baadae. Walikuwa watu walio barikiwa ujuzi na uwezo wa kipekee, wakaungana kwa lengo moja ambalo ni "kutengeneza jamii yenye haki, usawa na fursa ama nafasi sawa katika jamii"
Cha kwanza, waliongeza elimu ya kujitambua miongoni mwa wanajamii, waliandaa vikao ambavyo waliweza kuongelea maswala ya rushwa na udhalimu, waliamsha hali ya uwajibikaji na mshikamano. Watu walianza kuelewa kuwa mabadiliko yanakuja kwa kushirikiana wote kwa pamoja ikiwa na maana ya wananchi pamoja na serikali yao.
Pili, waishirikiana pamoja na vyama vya siasa, viongozi na wanaharakati ambao tayari kupambana na hali iliopo katika jamii yao. Kwa kushirikiana waliunda nguvu isio ya kifani, nguvu iliokuwa na lengo moja tu la kuondoa na kufuta rushwa na udhalimu uliokuwa unachafua na kuipaka matope hadhi ya nchi na jamii yao. Wanaharakati nao walichukua nafasi na kuandaa mpango mkakati wa kutatua sababu kuu za rushwa na udhalimu. Wakaielimisha jamii yao juu ya haki zao na jinsi ama namna ya kuwawajibisha viongozi wao. Wakawapatia vijana elimu na ujuzi, wakitambua kuwa vijana ni chachu ya kuleta mabadiliko baadae.
Kwa kuhakikisha kuwa kuna uwazi na uwajibikaji. Kikundi kile cha watu kikaanza kutumia teknolojia na kutengeneza majukwaa mtandaoni ambayo wananchi wataweza kuyatumia kuripoti vitendo vya rushwa. Walishirikiana na vyombo vya kutekeleza sheria kushunguza na kuwa wajibisha viongozi na watu wenye tuhuma za kujihusisha na vitendo vya rushwa, pia kutuma ujumbe madhubuti kwamba vitendo vya rushwa havitovumilika wala kuchekelewa tena. Hivyo, wala rushwa na wapokea rushwa watakutana na nguvu ya muungano wa wananchi na serkali yao. Juhudi na umahiri wa watu wa kijiji cha Utawala Bora zilianza kuonekana na kusambaa nje ya mipaka yao. Mashirika ya kimataifa na serikali za kigeni zilitambua harakati hizo na kuziunga mkono. Mshikamano wa kimataifa uliwapatia wanamabadiliko (wanaharakati)ujasiri wa kuendelea kupambana na kujua kuwa jitihada zao zinazaa matundwa na kuwa mfano wa kuigwa na jamii nyingine mbali na nchi yao.
Baada ya muda, mabadiliko yalianza kuonekana dhahiri. Wadhalimu, wala rushwa na wapokea rushwa waliwajibishwa na kupokea adhabu kali zilizowakanya kutorudia makosa tena, Imani ya wananchi juu ya serikali yao ilirudi tena, wawekezaji walianza kuvutiwa na kuja kuwekeza katika nchi ile, matunda ya haki na usawa yakaanza kuonekana kwenye huduma za afya, elimu, ofisi za uma na miundo mbinu zikiwa zimeboreshwa. Kwa mara ya kwanza, jamii ambazo zilikuwa zimetelekezwa zikainuliwa na kupewa nafasi ya kushiriki katika kutoa maamuzi. Kijiji cha Utawala Bora kikawa mfano wa jamii ilioungana na kushirikiana kuleta mabadiliko.
Mwisho, watu wa kijiji cha Utawala bora walidhihirisha kwamba mabadiliko yanwezekana, licha ya ugumu na vikwazo vya namna mbalimbali. Kwa dhamira, ujasiri, ustahimilivu na mshikamano waliweza kubadilisha jamii kutoka katika jamii iliogubikwa na rushwa na ubadhilifu na kuwa jamii iliogubikwa na matumaini na maendeleo.Safari haikuwa rahisi lakini matunda yaliopatikana yanastahiki kila hatua ilopigwa.
Ni matumaini yangu kuwa andiko hili litaleta mabadiliko chanya katika nchi yetu ya Tanzania hasa katika jamii ambazo zimejitenga au hazipo tayari kusimama na kushirikiana na serikali katika kupinga rushwa na ubadhilifu katika mali za umma. Pia natumai kuwa viongozi watakua mstari wa mbele kuichukia na kupambana na rushwa na udhalimu.

NUKUU: "Rushwa ni adui wa haki. Tunamtaka raisi atakae litambua hilo, atakayeichukia rushwa hata ukimuangalia aonyeshe kweli anaichukia rushwa, sio rais anaesema kweli rushwa ni adui wa haki....... lakini ukimuangalia usoni unashangaa na kusema......aaah kweli huyu?".... Maneno haya ni ya baba wa Taifa letu Mwalimu JK Nyerere.
Upvote
1