SI KWELI Kijiji kizima chafutwa kwa tetemeko la ardhi nchini Morocco isipokuwa majengo mawili tu ya Msikiti

SI KWELI Kijiji kizima chafutwa kwa tetemeko la ardhi nchini Morocco isipokuwa majengo mawili tu ya Msikiti

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Tetemeko la aridhi nchini Morroco limeua zaidi ya watu 5000, kuna kijiji kimoja cha mlimani chote kimefutwa na tetemeko isipo kua majengo mawili tu, hayo majengo mawili ni msikiti wa kijiji na nyumba ya huyu alio jenga huo msikiti, hiivi hili lina uhusiano wote na Imani au ni ecological force tu, wenye uelewa mambo theology na geography tuambieni.

Screenshot_20230913-072231_WhatsApp.jpg

 
Tunachokijua
Usiku wa Septemba 9, 2023, tetemeko kuu la ardhi lilitokea nchini Morocco na kuharibu vibaya moja ya maeneo muhimu ya kihistoria katika milima ya Atlas ya Juu, msikiti wa ardhi na mawe uliojengwa na nasaba ya enzi za kati iliyoteka Afrika Kaskazini na Uhispania.

Vyombo vya habari vya Morocco viliripoti kuwa sehemu za Msikiti wa Tinmel zimeporomoka. Picha zinazosambaa mtandaoni zilionyesha kuta zilizoanguka, mnara ulioanguka nusu na marundo makubwa ya uchafu.

screenshot-2023-10-05-161114-png.2772728

Mwanaume akitembea karibu na Msikiti wa Tinmel, ambao uliharibiwa na tetemeko kuu la ardhi, huko Tinmel, Morocco, Septemba 11. REUTERS/Hannah McKay
Kikijibu swali la Reuters kuhusu uharibifu ulioripotiwa kwa Tinmel, chanzo cha Wizara ya Utamaduni ya Morocco kilisema Wizara imeamua kukarabati na kuurejesha msikiti huo na wangetoa bajeti ya kutosha kufanikisha kazi hiyo.

Msikiti wa karne ya 12 ulijengwa ambapo nasaba ya Almohad ilianzisha mji mkuu wake wa kwanza katika bonde la mbali la Atlas kabla ya kwenda kuteka Marrakech, kumtangaza kiongozi wake Khalifa, na kuandamana katika eneo hilo kwa kuchochewa na bidii ya kidini.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kitamaduni UNESCO limesema limesikia "uharibifu muhimu sana kwa Msikiti wa Tinmel", ambalo limeongeza kuwa lilipendekezwa kuorodheshwa kama eneo la Urithi wa Dunia, lakini likaongeza kuwa bado linasubiri kutuma timu kutathmini uharibifu huo.

Hadi Septemba 11, 2023, takriban watu 2,000 wamekufa katika tetemeko hilo la kipimo cha 6.8, ambalo ndilo lililoharibu zaidi eneo hilo tangu mwaka 1900. Lilipiga siku ya Ijumaa usiku, na kuharibu majengo ya jadi katika Atlas Kuu na kuanguka kwa nyumba za matofali na mawe katika vijiji vingi vinavyoonekana.

Tetemeko hilo pia lilisababisha uharibifu katika mji wa zamani wa Marrakech , eneo la Urithi wa Dunia wa UNESCO, ambapo mnara ulipinduka na sehemu za kuta za jiji la kihistoria kuanguka pamoja na baadhi ya nyumba za jadi.

JamiiForums imebaini kuwa Madai ya msikiti kutokuharibiwa na tetemeko hayana ukweli, na hakuna taarifa zinazothibitisha jambo hili.
Mungu wa kweli hawezi kubakisha msikiti unaoswaliwa na imani iliyo kinyume naye, labda mungu wa kwao asiye Mungu wa Israel. matendo yao ni ushahidi wa wanachoamini.
Uko sahihi mkuu
Kidini Mungu (anaweza kuepusha vyote) hahusiki hapo kwenye kubakia msikiti na hiyo nyumba moja
 
Hili linajionesha bayana watu wa eneo hilo walifanya machukizo sana kwa mwenyenzi mungu, walimchukiza sana mungu kwa kudharau watu na kuwa wabinafsi wao kwa wao, linawezekana alijenga msikiti alimcha mungu na kutoa vile alivojaliwa.

Zinaa ziliwazidi, fitina, roho za husda, wivu, ubinafsi na choyo, dharau na kiburi, mengine watamalizia waislamu......mimi si muislam ila hili linaonesha jamii hiyo ilikuwa ni waja wa mungu walio kiremiwa vizuri sana na walipata tawala za juu za kifalme kwa wakirstu tunaamini hivo ila sasa tamaa za dunia ziliwazidi wakaona mungu kwao ni ziada.
Unakufuru siyo? Kama ni dhambi kuna nchi yenye dhambi kama Tanzania?
 
Kungekuwa na Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote kusingekuwa na tetemeko la ardhi lolote, popote wakati wowote to begin with wewe bwege mtozeni.
Mungu wa Islam sio hana upendo wote, Chek your facts
 
Mungu wa Islam sio hana upendo wote, Chek your facts
Hujui hata majina ya Mungu katka Kiislamu.


Ar- Rahmaan, Ar-Raheem

The beneficent. Most gracious, most merciful.

He who wills goodness and mercy for all His creatures

He who acts with extreme kindness

Sasa kama Mungu huyo yupo kweli, na ana upendo wote, uwezo wote, ujuzi wote, kwa nini aumbe ulimwengu ambao unaweza kuwa na tetemeko la ardhi wakati aliweza kuumba ulimwengu ambao hakuna tetemeko hata moja linaloweza kutokea?
 
Hujui hata majina ya Mungu katka Kiislamu.


Ar- Rahmaan, Ar-Raheem

The beneficent. Most gracious, most merciful.

He who wills goodness and mercy for all His creatures

He who acts with extreme kindness

Sasa kama Mungu huyo yupo kweli, na ana upendo wote, uwezo wote, ujuzi wote, kwa nini aumbe ulimwengu ambao unaweza kuwa na tetemeko la ardhi wakati aliweza kuumba ulimwengu ambao hakuna tetemeko hata moja linaloweza kutokea?
Samahani, hii Umeitoa wapi?
 
Miezi michache imepita Tetemeko -uturuki ,likaenda piga Morocco,jana Libya imepigwa na mafuriko watu 2000 wamekufa na zaidi ya 10000 hawajulikani walipo,wengine wamesukumizwa baharini huko

Ni Mwendo wa Mapigo tu kwa Waarabu mpk wamrudie Mungu wa Kweli😇
Mimi mkristo lakin wewe apa unakosea
 
Inaonesha wakazi wa hapo ni masikini sana wasiweze kujenga nyumba imara. Jengo pekee bora na imara ni hilo lililojengwa na aidha serikali au wafadhili, kama sio michango yao wenyewe.

Funzo: Wanadini ni wapuuzi, wameacha RAIA wafe, wamejali uimara wa jengo, sasa wafuge mbuzi humo ndani liwe na tija.
 
Miezi michache imepita Tetemeko -uturuki ,likaenda piga Morocco,jana Libya imepigwa na mafuriko watu 2000 wamekufa na zaidi ya 10000 hawajulikani walipo,wengine wamesukumizwa baharini huko

Ni Mwendo wa Mapigo tu kwa Waarabu mpk wamrudie Mungu wa Kweli😇

mungu wa kweli ni nani?
 
Miezi michache imepita Tetemeko -uturuki ,likaenda piga Morocco,jana Libya imepigwa na mafuriko watu 2000 wamekufa na zaidi ya 10000 hawajulikani walipo,wengine wamesukumizwa baharini huko

Ni Mwendo wa Mapigo tu kwa Waarabu mpk wamrudie Mungu wa Kweli[emoji56]
Binadamu wa kwanza tangu nione jua kuona anafurahia vifo kwa binadamu wenzake

Dont tell me huyo mungu wa kweli ni man made
 
Hivi .miujiza ya kiislam ni ya madhara tu huenda ndio maana wanapinga sana uponyaji.
 
Naona nyie amuangalia hata talifa zakimataifa hashimu haebara wa aljazeera mvona anali report tukio hili kala baada ya saa kwenye taarifa za habari akiwa eneo la tukio au hujui kiingereza kabisa, ila ungeona picha tu.
Naona umeanza kuhubiri mkuu
 
Back
Top Bottom