Ushauri mzuri sana mkuu. Tatizo ni kuna wachache wanaona wana birth right ya kutukana wenzao na wao wasitukanwe.Unapojadili mada wanakuja na lugha zao za matusi wakijibiwa ndio wana play role ya victim. Unapowasha moto at least uwe na uwezo wa kuhimili joto lake.Ustaarabu huzaa ustaarabu. Ukija na ujahilia utakuwa treated as jahili.Wana JF tulindeni heshima ya jamvi. Naelewa kuna baadhi ya majibu yanayoidhi wengine. Nawasihi wenye majibu kama hayo wajiziwie kuyatoa, na nawasihi pia wanaohisi wameudhiwa na majibu aina hiyo nao wawatukane wajibuji wao kimoyomoyo. Tusipochunga tataishia kuliko lilivyokuwa Bunge Maalum la Katiba!