Kwa suala la
AROON kuwa zamani alikuwa hivyo mi sioni kuwa ni tatizo kwa sababu yeye sio MALAIKA.
Alipitia matamanio akiwa kama BINADAM aliyekamilika la sivyo hawezi kuwa BINADAM KAMILI.
Ameshajirudi na kujitambua sasa hivi kuwa yale ya nyuma natumai haendelei kuyafanya sasa yupo katika kuwaelimisha ambao wanaenda njia si sahihi. Hili ni jambo jema kabisa.
Sidhani kama ntaona mtu ana akili sawasawa eti kwa kumdhihaki
AROON kupitia makosa yake ya nyuma ambayo natumai ameshaachana nayo na kuacha kumshangaa MCHUNGAJI ambae bado anakunywa KONYAGI na huku akiendelea kuchunga kondoo wa bwana na mikondoo ikiendelea kumskiliza na kumfata huku imeinamisha vichwa chini.
Mi naona
AROON yuko sahihi kabisa kwa sasa coz makosa yake ya nyuma ambayo natumai amejitambua na kujisafisha na kuzaliwa akawa MSAFI KABISA. Makosa yake ya nyuma hayazuii hizi mada anazoweka hapa kupokelewa na watu na kuzisoma.
Watu watazipokea na kuendelea kubaini machafu yote yanayofanywa na hao wanayoyafanya.
Safi kabisa mkuu
AROON kwa kufanya kazi ya MUNGU kwa kufichua maovu yao. MUNGU AKUTIE NGUVU NA AKUTANGULIE, AKULINDE DHIDI YA JICHO LIKUTAZAMALO VIBAYA.
BWANA YUNAWE MKUU. VYEMA KABISA.