Nilichosema jana, kimo kwenye ripoti ya bomani. Ripoti hii ni 'public document' na tayari nilishaitoa kwa mod aiweke hapa toka mwezi May.
Madai ya Mkono kuhusu Buhemba ni madai sahihi kabisa. Kamati yetu ilijadili suala la Buhemba na kukuta lina utata mkubwa sana na hivyo kutaka Uchunguzi wa kina ufanyike. Nilichosema jana ni kuwa Kamati ya Shelukindo imetaka uchunguzi maalumu katika Bulyanhulu, Kiwira na mwadui. Mimi nimesema uchunguzi huo maalumu wa kibunge uhusishe Buhemba.
Mimi binafsi nimeridhika sana na Taarifa yetu. It is the best we could get. It will reform the mining sector. I am proud to serve in that committee. I am proud of my inputs to the report. I passed a test, watu wengi walidhani nitazibwa mdomo! Nikawaambia sina bei................. nimedhihirisha.
Pili, watu wengi waliamini ripoti hii haitakuwa wazi. Nikasema serikali isipoiweka wazi mimi nitaiweka wazi. Serikali ikaiweka wazi bila kubadili kitu wala kuandika upya. Zaidi ya hapo imejadiliwa Bungeni na kupewa siku nzima ya shughuli za Bunge. Haijawahi kutokea kwa Ripoti yeyote ya Madini kuwasilishwa Bungeni na kujadiliwa. Lolote linalowasilishwa Bungeni ni la Umma.
Mkono na Buhemba yake yupo sahihi kabisa. Kuna tatizo la 158bn walizolipwa Meremeta kupitia benki ya NEDBANK ya Afrika ya Kusini. Ubadhirifu wa zaidi ya EPA.
Kwanza nashukuru umekubali kwamba Mkono is right.
But let me make it absolutely clear what Mkono is saying so you know exactly what you are agreeing here.
Mkono anasema:
1. Tume yako, tume ya Rais, kutuambia haijapata majibu hiyo ni unacceptable. Tume ya uchunguzi kupendekeza Tume nyingine ya Uchunguzi kujua nani anamiliki mgodi huo ndio Mkono anasema usanii.
Wananchi wamechoka na tume. Kwa nini tume yako, Tume ya Rais, haikuwa na mandate ya kujua nani ana miliki Buhemba?
2. Mkono anasema kabla ya Tume yako, Tume ya Rais, kuundwa ulikuwa unalipigia sana kelele haya mambo. Umeingizwa kwenye Tume halafu ukaenda humo ukanyamaza kimyaaaa!
Kama ungepiga kelele ukiwa ndani ya hiyo Tume ungekuja na majibu, sio maswali mengine, muheshimiwa Zitto.
Jana umehoji inakuwaje madini yanachangia asilimia 40 ya mapato ya mauzo nje ya nchi lakini hapa nchini yanachangia asilimia 3 tu ya pato la Taifa.
Wakina Mkono na wengine jana tulitegemea utuletee majibu. Utuambie yanaenda wapi hayo mapato. Ndio maana Rais Kikwete akakuweka kwenye Tume. Alikuwa na sababu. Na jana umemshukuru kwa kukuweka kwenye Tume japo ulikuwa sio favorite wa wabunge wenzio. He had a reason, the president did.
Wewe tena unapendekeza Tume. Wananchi wamechoka na hizi Tume na Kamati za Bunge na Rais.
Halafu, mheshimiwa Zitto, unatuambia ripoti ya Shelukindo ndio more "radicle." Kwa nini wewe hukuifanya ile uliyokuwemo wewe iwe "radicle" ? People expect more from you Zitto.
We huoni mpaka Mbunge mwenzako, the high-powered and well-placed Mkono nae anaweka matumaini yake kwa mtu kama wewe, Mbunge mwenzie. Wewe unakuwa held to a different standard. Unapotuambia ripoti ya Shelukindo ndio radical na kupendekeza tume nyingine, na kuhoji mapato ya madini badala ya kutupa majibu ndio Mkono anasema huo usanii.
Halafu unasema Bungeni kwamba unataka iundwe tena kamati ya Bunge kuchunguza kufukiwa kwa wachimbaji Bulyahulu. Kamati yako ilishindwa nini ? Si umesema kamati yenu, ya Rais, ilipokea malalamiko. Sasa mlipokea malalamiko halafu hamkuyafanyia kazi ? Haikuwa mandate yenu? Sasa mlikusanya malalamiko ya nini ?
Unataka more Tume's and more Kamati's. Wananchi wamezichoka Zitto. Kamati hazi work. Ndio leadership style ya Kikwete administration. Kamati's and more Kamati's!!!
Ndio maana Mkono anasema ni usanii. Mkono anasema it doesn't take more Kamati's to figure out who owns these mines! Mnamwambia Mbunge wa jimbo lenye mgodi kwamba Kamati yenye presidential gravitas imeshindwa kujua nani mmiliki wa mgodi. Sio usanii huo ? Nimrod Mkono is right!