Kikao cha CCM: RA Atema Cheche "Nitajiuzulu...."

CCM wanabore sana hamna hata plan ya maendeleo, kila siku tume na kujitetea flani msafi huyu kaonewa.
 

WildCard,

Unaijua katiba ya Tanzania? akiwasilisha mtu mmoja ndani ya Bunge hoja ya kutokuwa na Imani na Spika na kukafanyika kikao ambacho Spika hutoka nje, mchezo umekwisha!

Mkandara,

La nyongeza, tulishangilia kanyaboya la Mramba na Yona kufikishwa mahakamani, nikaandika https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/21106-paukwa-pakawa.html watu wakafikiri natania!

Leo hii Kiwira imerudishwa kwa Serikali, walionunua kwa bei chee wamerudishiwa pesa zao, hakuna atakayepelekwa mahakamani.

Hizo za EPA, waliopelekwa mahakamani wote ni wale waliojichongea binafsi pembeni ya mchoro orijino wa Saidia CCM Ishinde! Wataungua, mtashangilia lakini KAGODA kamwe hataguswa, Jeetu Patel kapewa tenda mpya ya Bilioni 50, je unaamini kuwa ataendelea kuwa na kesi Kisutu?
 
mkuu tusaidie nani huyo mlishaji ?
 

EDO,

Hili ndilo nimekuwa nauliza siku zote, kwa nini ndani ya Chama hawawaondoi hawa jamaa? Ni miezi 18 tangu wamepewa tuhuma na hata wakaondoka madarakani kwa aibu, kwa nini bado wanalelewa na Chama na kuonewa haya na Mwenyekiti wa Chama?

Je mnataka tuanze kuhoji Uhalali wa Mwenyekiti na kumhoji Uzalendo wake uko kwa nani? Tukifika huko si mtatuita WAHAINI au?
 
Yaani tutumie mamillioni ya kodi kwa ajili ya kutafuta Rostam ajiuzuru! mbona hiki ni kichekesho. dah! Rostam ...

Huyu jamaa ni kama chizi kweli, ameshatuibia vya kutosha kisha tena tuendelee kutumia fedha, kisa yeye ajiuzulu.

Muda wenu umewadia, kilichobaki ni kwenda mbele na hapa CCM ni lazima ichanike
 


Umekasirika?

Juzi uwanja wa ndege ya JK Nyerere nilikutana na kale ka Rais ka Madagascar Bw. Rajoelina
 
Haya maneno gani lakini jamani.. Huyu RA na Wabunge wote Mafisadi hawafahamu kwamba Spika Sitta is third in line ktk uongozi wa nchi?..

Third in line maana yake nini?
 
Huyu jamaa ni kama chizi kweli, ameshatuibia vya kutosha kisha tena tuendelee kutumia fedha, kisa yeye ajiuzulu.

Muda wenu umewadia, kilichobaki ni kwenda mbele na hapa CCM ni lazima ichanike

mtachanika nyie lakini CCM itaendelea kudumu daima
 


Unahitaji wabunge 20 tu kusaini petition na kuweka hoja ya kumwondoa Spika. Anaondolewa kwa simple majority.

Njia nyingine ni chama chake kuondoa udhamini wake na hivyo kuondoka uspika. Hawatafika huko! Wanasema hawataki kutengeneza hero!
 

Mzee Mwkjj,

Suala la kumuengua six likifanikiwa, basi huo utakuwa mwanzo wa Demokrasia mpya, natabiri kuanzishwa chama chenye nguvu zaidi na kitakachoweza kukibwaga chama cha mafisadi na maneno ya Mwl. yatakuwa yametimia "upinzani wa kweli wa CCM utatoka ndani ya CCM"

Siku hiyo naomba wanajamvi wote tukachukue kadi pamoja na familia zetu.
 
Third in line maana yake nini?


Spika hayumo kabisa kabisa line up ya Dola. Mwaka 2005 Katiba ilibadilishwa na line up kuwa Rais, Makamu na PM.
 
Sina cha kuongeza, MTOTO nakuunga mkono asilimia 200%. Huo ndio ukweli hakuna mpiganaji kila mtu ana intrest zake!!!!!!! 😕
 
Rev.
Azimio la Bunge la kumwondoa Spika Madarakani linahitaji theluthi mbili ya Wabunge kuliunga mkono (84.7.d). Kwa mazingira ya sasa hiyo ni ngumu sana. CCM pia wanaelewa madhara yake na ndio maana ile njia rahisi zaidi na ya mkato kupitia NEC yao ilishindikana.
 

Wanamharibia JK?.

No, hawamharibii, bali wanathibitisha kuwa JK is indeed weak, 'dhaifu'. Yaani nasema bila kujiuma uma ulimi, JK ni DHAIFU!.

Niliwahi kukaa na Kinana mahali over gahawa, nikamwambia my honest opinion kuwa JK ni dhaifa, na kama kweli sio dhaifu, basi anaonekana dhaifu. Nilimtolea mifano miwili tuu kuhusu udhaifu wa JK, moja jinsi alivyoyumbishwa kwenye issue ya muafaka, huu ni udhaifu mkubwa sana mbele ya jamii ya kitaifa na kimataifa.

Tatizo hakuna watu wa karibu wa kumweleza. Mbona Nyerere alikuwa na msimamo. Udhaifu wa pili nilioteta na Kinana ni jinsi anavyowakumbatia watuhumiwa wa ufisadi, hata kama hakuna uthibitisho, hili linamchafua na litamuangusha. Mhe. Kinana alimtetea sana JK kuwa sio weak, alikiri kuwa hili la Zanzibar hata JK hafurahishwi na hali ilivyo, bali alizidiwa nguvu ndani ya vikao naye hakutaka kufanya udikteta, kwangu huu ni udhaifu.

Kama hili la kumng'oa spika Six ni la kweli, CCM itampasukia mkononi and this is healthy for opposition, we will at least get serious opposition ili litimie lile neno "Upinzani wa kweli utatoka CCM" - Mwl. J.K Nyerere.
 
Hii kamati ya mzee Ruksa imegeuka kuwa uwanja wa vijembe na mipasho, na mkuu amekaa kimya...
 

wabunge walioko Bungeni.. siyo wabunge wote!
 

Katiba?

Then kuna mgongano mkubwa na kanuni ambazo zimeweka taratibu za kumwondoa Spika. Hata hivyo Katiba prevails. Thanks
 
Umekasirika?

Juzi uwanja wa ndege ya JK Nyerere nilikutana na kale ka Rais ka Madagascar Bw. Rajoelina

Zitto,

Taifa linapoteza muda na kodi kubembeleza upuuzi!

Leo hii pesa zote tulizopoteza katika miaka 10 iliyopita tungekuwa na Reli moja kabambe mpaka jimbo la Kalemi. Tungekuwa na hospitali za Rufaa za kisasa kila mkoa, tungekuwa na vyuo vikuu vya kutosha, barabara zetu zingeunganisha nchi vizuri kabisa, GDP yetu ingekuwa si chini ya $5000 kwa kila mtu, ajira zingekuwapo za kutosha na tungekuwa na suluhisho la kudumu la umeme na nishati!

Nisipokasirika mimi kama ninavyoruhusiwa na Katiba, nimwachie nani jukumu hilo? nilisukume kuwa ni la Zitto pekee? nope ni letu sote!
 
Spika hayumo kabisa kabisa line up ya Dola. Mwaka 2005 Katiba ilibadilishwa na line up kuwa Rais, Makamu na PM.

very good kiongozi kwa ufafanuzi huu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…