Mkandara,
Wakati wa Uchaguzi wa 2005, pesa chafu ya EPA ndio iliyoirudisha CCM Madarakani, ingawa wala hawakuhitaji kuchota.
Uchaguzi wa 2000, pesa za Meremeta na upuuzi mwingine zilitumika vizuri sana maana kulikuwa na kutokuaminiana ndani ya Chama na ngao ya CCM Mwalimu Nyerere alikuwa katutoka
Uchaguzi wa 1995, pamoja na pesa zote zilizokwisha chukuliwa kisanii na CCM, ilibidi wamkimbilie Nyerere ambaye single handedly aliwaangusha Mrema na wenzake wa Muungano na kutumia fimbo ya matakoni kumrudisha Salmin.
CCM ni chama si cha kuaminiwa na wewe unalijua hilo. KInachotokea sasa hivi ni ugomvi wa nani ashike hatamu na kula utamu kwa kutumia CCM na wala si kuhusiana na maslahi ya Taifa.
Waziri wa Usalama wa Taifa anapota kauli kuwa kila mtu ni safi kuhusu RICHMOND na RADA, je unafikiri ni nani aliyetoa baraka kwa kauli kama hiyo kutolewa?
Lowassa, Rostam, Sitta, Mwakyembe na wengineo wana madhambi yao, na tatizo limekuja sasa hivi ni mapiku!
Kama kina Sitta na Wapiganaji wangesikiliza lile tulilowaambia la kutetea maslahi ya Taifa na kufanya kazi kwa manufaa ya Taifa, fedheha kama hii isingetokea na kina Lowassa, Rostam na Sophia wasingediriki kufanya wanalolifanya leo hii!
Kwa miaka mitatu tumekaa tukizungumzia tuhuma kuhusu Rostam na Lowassa, je wameshakalishwa kitako ndani ya Chama au Serikalini na wakachukuliwa hatua?
Je Chenge naye ambaye ni mkuu wa Maadili ndani ya Chama ni lini amekalishwa kitako akaambiwa ajieleze?
Juzi suala la Richmond limegeuzwa kuwa ZeComedy, kina Sitta wanabanwa Golori zao kuttokana na kupenda posho, kina Ngwiliza wanafunuliwa kwa kupata pensheni mbili mbili, huku Richmond, Kagoda, EPA, Rada na sasa Kilimo Kwanza wanapeta na tunadanganywa kuwa ni kukua kwa Demokrasia ndani ya Chama!
Huu ni uhaini wa hali ya juu, na Watanzania tunachezewa akili, tunafujiwa hazina yetu na tunafanywa wapumbavu!
Nilihoji kwa nini Wapiganaji hawajiondoi na UCCM na kupigania mambo ya Taifa? Kwa nini wanaendelea kuogopa panga na rungu la Chama kwa kuendelea kuimba CCM mbele, Tanzania nyuma kam Wakristo wanavyoimba Msalaba Mbele Dunia nyuma?
Kwao Wapiganaji wa CCM, wokovu wao(binafsi) ni kupitia CCM na si kupitia Taifa la Tanzania!
Ni upuuzi kuendelea kuwasikiliza! Kwanza afadhali na tunajua kuwa Lowassa, Rostam na Chenge ni Mafisadi na hilo kila Mtanzania analijua na usishangae kuwa mwakani, viti vyote vya Ubunge Dar vitakwenda CCM na zaidi CCM inaweza kupunguza nusu ya viti vya Upinzani hasa Bara.
Lakini kwa kuwa ni jadi ya kuoneana aibu ndani ya Chama, kina Sitta wamepoteza nafasi moja kubwa sana, walipoleta ripoti ya Richmond wakadai kuna mambo mengine hawatayazungumza ili kuifichia aibu Serikali, hapo ndipo walipouza utu wao na wakapoteza sifa ya kuwa wapiganaji na hata maana ya kuwa na tume.
Kuondoka kwa Lowassa hakukutosha, ilipaswa ripoti ilete mabadiliko ya kweli si ya watu kujiuzulu tuu!
Kama wasingeficha baadhi ya mambo eti kuionea aibu Serikali, leo hii kila lililoovu lingeanza kuweweseka na kuogopa. Lakini midhali waliamua kufukia maovu na uzembe mwingine kwa kuonea huruma na aibu Chama na Serikali, basi ni vigumu sana kwa mabadiliko na vita dhhidi ya uhujumu, uzembe na kutofuata kanuni kufanikiwa.
Lakini swali langu na lile la Mwanakijiji linarudi, Wapiganaji wanapigania nini na wanampigania nani?
Ukiona Sophia na Rostam wanatamba kama walivyofanya sasa hivi, jiulize Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yupo wapi na yupo upande gani?