Kikao cha Dharura: Mashabiki wa team 12 (Vichwa Ngumu) zilizoanzisha "European Super League". Tukutane hapa tujadili jambo hili

Alexander The Great

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2018
Posts
4,509
Reaction score
23,653
Habari Wana Jamii, Habari Wana Soka.

Leo ni "Afe Kipa, Afe Beki - Bukta Chanika, Boxa Vuuka - Lazima Kieleweke" limeanza amsha amsha na kuwekwa wazi kwa team vichwa ngumu barani ulaya, zilizoamua kusaliti kambi na kuanzisha League yake, hii ni baada ya kuona "UEFA & FIFA" ni wahuni na wapangaji wa matokea ya mechi juu ya meza kwa kushinikizwa na makampuni ya kucheza kamali (Betting Companies).

Team zitakazo shiriki michuano hio zitapewa € Billion 3.5 kwaajili ya kujiwekeza katika maswala mbali mbali ya team zao (Kama kuboresha viwanja n.k), nia na madhumuni ni kuwapa mashabiki wa mpira mechi zilizo bora na kali kuliko zinazochezwa katika "UEFA & EUROPEAN LEAGUE" kwa sasa hivi. Mechi ambazo pia zitachezwa katikati mwa week kama zilivyo za UEFA hivi sasa, na weekend kuachia dirisha za mechi za ligi za ndani kama ilivyo.

Ligi itahusisha team 20, 15 ambazo ni timu mama za league na nyingine kupita kwa vigezo vya nafasi watakazopata katika misimamo ya ligi za ndani.

Leo mara baada ya kutangazwa rasmi kwa kuanzishwa League hio ambayo inaonekana kuwa "TISHIO KUBWA KUWAHI KUTOKEA" hasa kwa UEFA & FIFA, taharuki imetanda baada ya tamko kutoka kwa UEFA & FIFA kukemea na kulaani kwa kuanzishwa kwa michuano hio.

Licha ya tamko la UEFA & FIFA kulaani kitendo hicho na kukiita ni ha "KIHUNI KUWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA SOKA", walienda mbali na kusema kwamba "TEAM YOYOTE ITAKAYOSHIRIKI MICHUANO HIO BASI ITAFUNGIWA KUSHIRIKI UEFA, EUROPA NA LEAGUE ZA NYUMBANI KWAO (National League)", na kuendelea kusema kwamba wachezaji watakao shiriki michuani hio watafungiwa kushiriki "WORLD CUP na EUROPE CUP".

Jambo hili limepelekea UEFA kuahirisha kwa muda usiojulikana mechi zilizosalia za Michuano ya UEFA, ambazo ni "MANCHESTER CITY VS PSG" na "CHELSEA VS REAL MADRID". Na kusema wataitisha kikao cha dharura na kujadiliana kumpa ushindi wa mezani PSG kwenye michuano ya "UEFA CHAMPIONS LEAGUE".

Mwenyekiti wa michuano hio mipya ya "EUROPEAN SUPER LEAGUE", anaeitwa na kutambulika na "UEFA & FIFA" kama mhuni mkuu Bwana Fiorentino Pérez nae hakusita kutoa tamko ya kwamba "MKIWAFUNGIA WACHEZAJI WETU KUCHEZA WORLD CUP QATAR, SIO TATIZO KUBWA KWETU KABISA, KWANI TUTAANZISHA NA WORLD CUP YETU".

Team zenyewe ni 12, ambazo zinatambulika kama "WAASISI WA EUROPEAN SUPER LEAGUE", ni;

1) AC Milan (Italy).

2) Arsenal (England).

3) Atletico Madrid (Spain).

4) Chelsea (England).

5) Barcelona (Spain).

6) Internazionale - Inter Milan (Italy).

7) Juventus (Italy).

8) Liverpool (England).

9) Manchester City (England).

10) Manchester United (England).

11) Real Madrid (Spain).

12) Totenham Hotspurs (England).

Updates

● Team za England zote zimetoa tamko la nia ya kujiondoa katika European Super League, baada ya siku mbili tu tokea kutangazwa kuanzishwa League hio.

● Inter Milan na Atletico Madrid wametoa tamko la nia ya kujiondoa kuwaunga mkono walioweka nia hio.

● Fiorentino Perez (Rais Wa Shirikisho La Super League) amesema kwamba mpaka sasa hivi hakuna team hata moja iliojitoa katika shirikisho hilo la Super League, kwasababu kwenye Mkataba Wa kujiunga kuna kipengele kilichosisitiza kwamba hakuna team itakayojitoa au itakayoruhusiwa kujitoa wala kuvunja mkataba huo wa miaka 23 mpaka utakapo fikia tamati. Amesema team hizo zimetoa kauli tu za kuonesha nia ya kujitoa kwenye shirikisho mara baada ya kukutana na vitisho kutoka kwa UEFA & FIFA.

● Perez amesema na kusisitiza kwamba shirikisho hilo halijafa, lipo standby na litaendelea bila hata hizo team za England.

● Mwenyekiti Wa Bayern Munich Bwana Rummenigge ameomba "UEFA & FIORENTINO PEREZ" wake meza moja na kujadiliana kuhusu swala hilo la Super League.

Amesema, binafsi yeye hajafurahushwa na swala la kuanzishwa kwa Super League, ila UEFA haipaswi kusahau kwamba Perez ni kiongozi wa klabu kubwa duniani.



Wadau wa soka na kubeti, nimewaita tujadiliane

Karibuni kutoa mitazamo yenu na updates kuhusu swala hili.
 
😂😂😂😂
Na bado kuna mengine makubwa yanakuja wee subiri tu alihutubie bunge utaskia mengi makubwa tena mazito mkuu...!

Acha tu aisee.
😂Boss yule naamini ataachia rasmi chombo na boss yule mwingine naye ataachia chama hiyo siku itakua mtiti.....Mwenzio wa itifaki keshafungusha.
 
😂😂😂😂

😂Boss yule naamini ataachia rasmi chombo na boss yule mwingine naye ataachia chama hiyo siku itakua mtiti. Mwenzio wa itifaki keshafungusha

Yule mwengine anabaki kubashiri tu mpaka dakika hii haoni mbele wala nyuma kama yupo katikati ya bahari aisee!
 
Bayern Munichen amepewa siku 30 kufanya maamuzi magumu kama anajiunga na hii Super League au anaendelea na UEFA, ndani ya siku 30 anatakiwa atoe msimamo wake. PSG nae amepewa week mbili tu (Siku 14) kufanya maamuzi magumu na yeye kama ataamua kujiunga na Super League au ataendelea na UEFA.

Mwenyekiti Fiorentino Peréz amesema UEFA wanauua mpira wa miguu na kila kitu kinafanywa kisiri siri, akatoa mfano dunia inajua mshahara wa LeBron James ila hawajui mshahara wa Mwenyekiti Wa UEFA wao (Kwanini mshahara wa kiongozi wa UEFA kufichwa siri), amesema wao kama Super League hawataki maswala ya team kuwa vinyonga.

Team hizo 12 za awali wameisha sign mkataba na European Super League wa miaka 23.

UEFA amekamatwa pabaya. Jamaa wapo serious, hawacheki na nyani.
 
Hatari sana, mabosi wetu wanataka kuiua UEFA & FIFA, wanaona zinatupandilia vichwani na mambo yao ya kiswahili swahili mpaka kwenye mpira wa ulaya.
Nimesikia kuna timu tano zitaalikwa kujiunga (ukiacha 15 zisizoshuka daraja) ambazo zitashiriki, msimu ukimalizika zinashushwa kuachia 5 zingine kupanda kushiriki. SWALI LANGU NI... Kama mojawapo ya zilizopanda ikafika fainali au kuwa bingwa, bado itashushwa?

Halafu mi naona hii haipo kimichezo zaidi, ipo kibiashara zaidi maana moja ya sababu alizotoa Infatino ni kuwa "watu lazima waelewe kuwa janga la korona limetikisa vilivyo vilabu hivyo lazima hatua zichukuliwe kama hii ya kuanzisha ligi"

Pia ni michuano ya kibaguzi, kibabe na kidikteta zaidi maana hizo big15 hazishuki milele na milele hata mojawapo ikimaliza michuano inaburuza mkia, bado itayoondolewa ni aliyealikwa! Kuna ladha gani sasa ya mashindano ya hivi, ushindani uko wapo hapo? Huu bi mradi wa vigogo wa timu kujikwamua na janga la kushuka kimapato.. tusi -DEMKE kwa mambo yenye maslahi binafsi ya vilabu na si maslahi ya soka.
 
Hivi vilabu na ESL wamejipanga vilivyo, imagine wameanza kutangaza ushirika na ushiriki wao baada ya vitisho vikali vya UEFA na FIFA bila wasiwasi.

Hii ni wazi lolote liwe au lisiwe wameamua kuanzisha ligi yao. Lakini tunaona kwa umbali kuna nguvu kubwa nyuma hasa kutoka kwa wamiliki wenye ukwasi wa vilabu hivi.

Pamoja na hayo bado tunaona nyuma yake kuna kampuni zinazoona hii ligi itakuwa fursa kwao katika kujitanua zaidi. Sasa tunashudia DAZN wakiweka pesa nyingi kuchukua haki za matangazo ya mashindao haya, Rakúten, Under Armour na Claró nao inasemakana wapo nyuma ya ESL.
 
NBA marekani zile timu huwa hashishuki daraja

Na inapendwa Sana
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] watafungua World cup yao noma iyo aisee mpira umekuwa kama chama cha siasa.
 
UEFA wana hali ngumu sana kwa sababu vilabu vikubwa vya dunia tayari wameshaunga mkono jambo hili bila kupepesa nadhan UEFA na FIFA bora waje matao ya chini kuwe na league 3 ukitoa zile za ndani, hiyo Champion League, Super league na Europa hapa issue kubwa ni biashara kama UEFA wameona ni changamoto basi waongeze mapato kwa hivyo vilabu na kuwa wawazi zaidi ili clubs wanachama wavunje mkataba na Super League.,

Kwa mara ya kwanza soccer linapata mtikisiko wa aina yake, na nadhan hii UEFA hawakuilalia wala kuiamkia imekuja kufumuka tu tayari watu washaingia sokoni kushawishi vilabu.,

UEFA mimi nawachukia sana mwaka 2011 Arsenal ikichecha na Barcalona ikiwa tayari Arsenal wanaitoa barcalona basi walimpa kadi nyekundu Van Parsie kwa mipango tu ili fainali lazima akacheze Barcalona na team nyengine ili wake make more money.,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…