Kikao cha Dharura: Mashabiki wa team 12 (Vichwa Ngumu) zilizoanzisha "European Super League". Tukutane hapa tujadili jambo hili

Hii kitu niliiwaza kabisa na nilisema hapa. Huyu Perez atakuja tengeneza pesa ndefu sana kwenye hivi vilabu vilivyo jifanya kujiondoa Super League. Vilabu vilikurupuka kusaini mkataba wa Super League kwa tamaa za kifedha, sasa kibao kitageuka kwao. Perez anadai hakuna alie lipa fidia ya kujitoa, Hahahahahaaa. Yaani lazima walipe fidia za kuvunja mkataba, Perez ni nyoko sana
 
Fixture ya Arsenal FC katika hii European Super League kwa mwaka huu 2021 ilikua;

1) Arsenal FC VS Juventus.

2) Arsenal FC VS Real Madrid.

3) Arsenal FC VS Barcelona.

4) Arsenal FC VS Inter Milan.

5) Arsenal FC VS Atletico Madrid.

Arteta skin tight ingempwaya. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Kila week timu zingekua zinamlia mingo Arsenal FC namna hii.

View attachment 1760862
 
Hizi fixture mkuu hazina athari kwa Arsenal tu ata rais wa madrid club bora ulimwenguni amelalamikia kuanza kupangiwa na team kubwa pia ni changamoto
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]dah nimecheka kwa sauti!!!
 
Bila shaka wewe ni diehard fan wa Arsenal!

Barca ile ya 2010/11 iliyoidhalilisha Man Utd kwenye fainali, Ferguson akitetemeka kama katolewa kwenye friji, akina Rooney machozi yanawalenga kwa lile soka lililokuwa likipigwa, van Persie ndo angeokoa jahazi la Gunners? Kama kumbukumbu zangu zipo sawa Arsenal alifurushwa kwa aggregate ya mabao 7-1 (3-1/4-0). Hizo bao 4-0 za second leg zote zilipigwa na Messi, akiigeuza kituko defence ya Gunners[emoji16]

Kumbuka pia ni msimu huo Real Madrid aliogeshwa 5-0!
 
Spurs na aseno wangeshuka daraja....
 
Perez na genge lake wanajiandaa kupokea fidia kwa klabu zilizo vunja mkataba
Perez ameongea juzi na kusema hakuna team iliojitoa mpaka sasa hivi, hao wameonesha nia ya kutaka kujitoa ila hawajajitoa.

Amesema kwenye mkataba walio sign una kipengele kinachosema "Hakuna club itakayo jitoa pindi ikisha ingia mkataba (Hakuna kipengele cha kulipa fidia ili ujitoe)". Ukiingia umeingia hakuna kutoka mpaka mkataba uishe miaka 23 ijayo.

Hao waliosema wanataka kujitoa sasa hivi wapo juu ya meza na wanasheria wao kuangalia kama kuna uwezekano wa kujitoa. Halafu ndio watatoa statement.

Perez amewapiga jiti hao jamaa, ila mashabiki hawalijui hilo, wasipokua makini atawafilisi vilabu vyao kwasababu "ATADAI FIDIA YA FAIDA AMBAYO SUPER LEAGUE INGEPATA KWA MIAKA 23 YA MKATABA".
 
Mimi siongelei ukali wa Barca ninachokwambia ile mechi 2011 Arsenal waliweza ku-dominate barcalona mpaka kufikia kiwango cha Arsenal sasa wanasubiri mpira uishe tukacheze finali., ndipo walipompa nyekungu Van Persie bila sababu na kuwapa barcalona penalt ya makusudi ili tu barca waende wao, dunia iliona na alijua kila mtu kwa uwazi kabisa kwamba mpang wa UEFA ni ule.

Ukimuuliza Arsenal wenger leo atakwambia mechi ile ilimuumiza sana iliitwa ni ''criminal in football ama Ant Football''
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…