Bora umehitimisha kwa kusema ni your personal view, ni muhimu sana uelewe rais Uhuru alichaguliwa na Wakenya kwenye platform ya kuboresha Kenya kabla hajawaza mataifa ya jirani. Hapo unapomlaumu kwa masaibu ya EAC unakosea maana wakati anaingia uongozini, yeye ndiye alikua junior ukilinganisha na wazee wote kama Museveni, Kikwete na Kagame. Amewakuta wanasuasua na huu mzigo wa EAC bila kupiga hatua, wanazunguka mbuyu kila siku, akawapa wazo lake na baadhi yao wakalipokea.
EAC haiwezi kuishi kwenye incubation miaka yote, lazima tufikie kwenye hatua za kuthubutu mapya, maana ulimwengu wa sasa upo kwenye kasi isiyo ya kawaida. Ukiwa rais wa Kenya lazima ujiandae kuwaza mambo ya kisasa kwa mifumo ya kisasa maana kizazi cha leo kinakwenda kwa kasi. Raia baina ya hizi nchi wanashirikiana tayari kwa mambo mengi ambayo hata serikali hazifahamu.
Nikirejelea kwa hilo la Raila kuwaza kupunguza kodi za nyumba, mimi binafsi sio shabiki wake lakini kwa hili namuunga mkono Raila na nipo radhi kukinzana na ndugu yangu
Sammuel999 Tunahitaji rais mwenye mipango endelevu inayoeleweka na kuonakana kwa sasa hivi. Mbinu zipo nyingi za kupunguza kodi ya nyimbo, ikiwemo upunguzaji wa taxes zinazohusiana na ujenzi na umilikaji wa properties.
Hayo ya vita dhidi ya ufisadi, asikudanganye mtu, sio rahisi kama unavyofikiria maana kila mmoja wetu kwa njia moja au nyingine ni mfisadi na ukithubutu kulipuka lipuka kama anavyofanya Magufuli utaishia kupoteza na kurudisha nchi nyuma sana. Juzi hapa Wakenya wamejitokeza laki kadhaa kumpa kura fisadi mkuu Waiguru. Raila mwenyewe ameshindwa kuwathibiti magavana wake mafisadi kama akina Kidero maana wanamlea.
Halafu huko namwona Magu anavyofanya kwenu, analea na kujenga visasi na majungu kila uchao, haonekani kuwa na mikakati na ni vigumu kutabiri anakoipeleka nchi, vita dhidi ya ufisadi vinataka mikakati endelevu na taasisi huru. Namwona akiwakimbiza watumishi wa chini kwa ajili ya vyeti feki huku akiwaacha wakuu wa mikoa akina Bashite.
Nikirudi kwenye haya ya Raila na Uhuru, binafsi mimi nataka kiongozi anayeongea na kutaja vitu vinavyoeleweka na kuonekana, sio hayo mambo ya nadharia, watu wajiulize kwanini Peter Keneth amepigwa chini na nadharia zake. Hivyo ni muhimu sana kwa viongozi kufuata mfano wa Raila na kutaja moja kwa moja vitu vinavyofahamika na kueleweka na mwananchi wa kawaida.