KENZY
JF-Expert Member
- Dec 27, 2015
- 32,529
- 76,691
Ilikuwa mida fulani hivi ya saa mbili usiku ile naingia nyumbani kabla sijafika sebuleni nikasikia ndugu zangu wanajadili "Tumemletea tiba leoleo lazima aache hizo pombe zake!"
hapo walikuwa hawajashitukia kama nimeingia na siku hiyo mpk narudi sikua nimeweka vyombo!, wakati nimeendelea kujibanza wakawa wanakazia!, mi nikafikiri kidogo nikaona ngoja nirudi kwanza mtaani nikapige vyombo halafu nirudi niwachane kuwa niliwasikia na hawaniwezi!.
taratibu nikachomoka pasipo wao kujua nikazama kiwanja kimoja chapchap!, bapa kubwa ya kwanza ikaisha nikaisindikiza na bapa nyengine ndogo nilipojiona sasa nipo tayari huyo nikaanza kurudi nyumbani!
ile nafika palikuwa kimya sana mpk nikahisi kama hakuna watu!, wakati nafika sebuleni ghafla nikasikia mtu akisema "huyo hapo mkamateni!!"
wakati nataamaki nikahisi nimebanwa kwa nyuma, ndugu yangu mwengine akaja kwa mbele!. hapo bado bumbuwazi limenikamata mlevi wa watu sijui natekwa ama vipi, halafu natekwaje nyumbani tena na ndugu zangu!.
Wakati hayo yanaendelea nikawa nimewekwa mtu kati, yule aliembele yangu akabwatuka "Mganga njoo haraka mtu wako tayari!!"
sasa hapo ndo nikaelewa hawa binadamu wanataka kunimaliza,wameniletea mganga wakunitibu niache pombe! nikawatikisa kidogo walivyokuwa wamenibana lkn hata hawakutikisika!, nikajisemea moyoni "kwisha habari yangu!"
punde hiyohiyo nikaona mtu anatokeza, huyo ndo alikuwa mganga mwenyewe sasa muonekano wake tu ulitosha kujua leo kazi ipo!
alikuwa amevalia ile kiganga kabisa yani juu kaniki nyekundu chini kaniki nyeusi, huku kichwani akivalia kilemba cheupe!. mkono wake wakushoto akawa ameshika usinga!, kuliponitisha zaidi ni mkono wake wa kushoto akawa na kidude fulani kama chaduara kidogo kikawa kinarukaruka chenyewe hata hakirushi! hapo ndo kijasho mshenzi kikaanza kunitoka!.
Nikajitikisa tena mara hii walionishikiria wakatikisika!, mganga akawa mkabala na mimi akanipiga na ule usinga kwanza hakuna kilichotokea hapo mimi mapigo yanaenda mbio tu!, mara mganga akasema "sasa mbaneni vyema nimshike mdomo amezee hii!" yani kile kidubwasha kinachorukaruka natakiwa nikimeze!.
Kusikia hivyo just from no where nikajirusha kwa nyuma!, kumbe yule wa nyuma akawa hana balansi akanishinda akaniachia si nikaanguka! yule wa mbele akawa anakuja mkuku kunidhibiti pale chini nikamkwatua mguu akaanguka!, ile mi nataka kuinuka yule ndugu mwengine akawa ananivizia anikabe nikamuona akija kama kifaru nikaachia kifuti cha nyumanyuma! akaachia ukelele mzito!.
sasa walivyoona zoezi limeingia ndimu mmoja akawahi switch ya taa akazima!, mchezo ukawa wa gizagiza sasa!.. ghafla nikapigwa mtama kwa jinsi nilivyopigwa ule mtama nikahisi kabisa huyu alienipiga huu mtama alifanya mazoezi kabla!.. hapohapo nikapigwa kabari nyengine nzito ile natapatapa nikasikia "mganga njoo sasa!"
mganga akawa anahangaika kutafuta mdomo ile anaukaribia kaleta vidole nikamuuma! akapiga welelo mkubwa sana!, hawa wengine wakawa wameduwaa nini kimempata mganga!, hapohapo nikatupa kichwa kama mara mbili hivi ya tatu nikasikia mtu anakema nikajua tayari nishacheza na pua ya mtu!!.
hapohapo watesi wangu hawakunilazia damu nikasikia napapaswa zinatafutwa malighafi taifa (vinyanya mshenzi ama mapera ya adamu) zibinywe ili niachie ubingwa mapema!, nikaona hii haiwezekani!..
Nilizunguka kwa nguvu bila kuangalia nitakutana na nini, sikugusa kitu nikaona kabisa sekunde tano zijazo hawa mazwazwa wataniweza nikaamua kubetuka kwa nyuma nikasikia mtu anapiga kelele!, nikarusha na teke kwa mbele nikahisi limempata mtu!!.
si wakajichanganya wakawasha taa!, kuangalia hivi nipo karibu na mlango!! bila kuangalia nikatokomea kwa spidi ya sgr wakabaki wameduwaa!.
sikwenda mbali nikawa nasikia mtu analia huko ndani, kumbe lile teke lilimpata mganga sehemu mbaya hivyo maumivu yakawa makali, si akapandisha mizimu yake ikaanza kulalamika ati kiti wao ameumizwa!, msala ukahamia kwao wakashindwa kuelewana na mizimu nikiwa nimejibanza nikasikia vishindo watu wakikimbizwa, kumbe ni wale ndugu wawili walikuwa wakikimbizwa na mganga mi kuona hivyo nikazama ndani nikafunga milango nikalala!..
kesho asubuhi wananipigia simu wapo polisi nikawatoe wamekamatwa wote watatu kwa kesi ya uzururaji usiku!.. na shughuli ya kuniachisha pombe ndo ikawa imefia hapo!.😅