Kikao cha kuniachisha pombe nilivyokimaliza kibabe!

Kosa lilikuwa kuzima taa. Michezo ya gizani si mizuri.
 
Marcy
si mbaya ukinywa ki afya, uliza hata ma daktari watakuambia ukweli labda kama unashida za kiafya ndio itakuwa mbaya kwako!.

ipo hivi..
kuna aina nyingi za pombe, na moja ya pombe hizo ni pombe kali hizi naweza sema si nzuri maana ni kali na zinawahi kumchukua mtu, inategemea na kiasi utakachokunywa ila ni nzuri kunywa hii kwa kiasi kidogo sana kwaajili ya kupata hamu ya kula tu!, narudia kwa kiasi kidogo.

kuna wine hizi nashauri watu wanywe kwasababu zimethibitika kuwa na manufaa pia ki afya, ni nzuri sana kunywa wakati wa kula ama baada ya kula!.
pia kuna liqueur hizi zinafaa kunywa baada ya kula ni zinarahisisha mmeng'enyo wa chakula!.

shida ya pombe ni kuizidisha na unakunywa nini kwa wakati gani!.
pombe hutakiwi kunywa mpk ukalelengeta,ukakera watu,kupiga kelele na kero nyengine na ndio maana huwa tunasema sio kwaajili ya kila mtu!, maana si wote wanaiweza pombe kwani wengine wanakunywa kulewa!.
kitu chochote ukikifanya kwa kupitiliza lazima kitaleta tafrani.

hapo vipi marcy..?
 
Hata ungeandika kitabu kizima Bado hujanishawishi
 
🤣🤣🤣🤣🤣usinge nitag kama ndivyo
nimekutag kwasababu nilikuwa nakujibu komenti yako we yakwangu umei quote vibaya hivyo niki reply inashindwa kuja kwenye kibox cha reply so ili uone nikaona niku tag!.
 
We jamaa una kipaji cha uchekeshaji kabisa, kama bado haujaanza comedy show rasmi nakushauli tu anza sasa utapiga hela huko ndio kipaji chako kilipo
 
We jamaa una kipaji cha uchekeshaji kabisa, kama bado haujaanza comedy show rasmi nakushauli tu anza sasa utapiga hela huko ndio kipaji chako kilipo
kwahiyo mimi kusimulia matukio yangu ya kweli ndo kunafanya mimi nionekane nina kipaji cha komedi..?
aisee!
 
kama sio kahawa tea
mkuu,walikukosea sana dawa yakuachisha mtu pombe sio kwanjia hiyo,Mimi ninayo ya unga

sharti namba Moja,hutakiwi kujua Leo unawekewa au kesho

Pili,usimjue katu anayekuwekea mana atakuja kuja kuwa adui mkubwa
TATU ,hapa ndosiku yenyewe mkeo anaweza tafuta mtu wakaribu au hata mama Ako mzazi ukashangaa unaambiwa wikend hii tunaenda wote bar ukatununulie soda ,kimsingi utafurahia

nakufundisha ,hata kama ni mama Ako hakikisha sikuhizo huachi pombe mezani pale kila uendapo chooni hakikisha imeisha yote ,ukizingua tu uache unawekewa huo unga nitakao kuwa nimewapa(Mimi nimganga watiba mbadala)

ukiwekewa ,ukanywa baada ya MUDA utaanza kutapika tapika sana hii dawa ilivyo inakubadilisha kila kilicholadha ya pombe ..itakuwa pona yako ...kwa mawasiliano zaidi karibu gharama ni burekabisa mwenye nia mlevi wako akiacha pombe ndipo unaweza leta asante/takrima
 
mkuu kunywa mwenyewe dawa yako ya unga.
 
Hama hapo nyumbani la sivyo watakuadabisha tu
Pombe siyo sigara
 
kwahiyo mimi kusimulia matukio yangu ya kweli ndo kunafanya mimi nionekane nina kipaji cha komedi..?
aisee!
Kwa nia njema kabisa una kipaji kikubwa cha uchekeshaji unaweza kupata pesa kwenye fani hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…