Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
KIKAO CHA MAUAJI; RUDISHA UPANGA WAKO ALANI, ATUMIAYE UPANGA ATAKUFA KWA UPANGA.
Anaandika, Robert Heriel
Yesu aliwahi kusema, kipimo utakachompimia mwenzako, ndicho hichohicho utakachopimiwa tena Kwa kufurika
Akaendelea kusema; Atumiaye upanga, atakufa Kwa upanga.
Bado akitetea falsafa ileile ya Hukumu ileile umpayo MTU basi hiyohiyo ndio utakayohukumiwa.
Isaac Newton aliwahi kusema katika third law of motion, akasema; for every action (force) in nature there is an equal and opposite reaction
Yesu hapo alikuwa anamkanya Petro asichukue panga lake kujihami dhidi ya wale Askari warumi waliokuja kumkamata.
Falsafa Hii inahoja zifuatazo;
1. Usaliti
Ikiwa utamuua au kumsaliti MTU aliyekuamini na akakupa nafasi, basi elewa kuwa na wewe utauawa na MTU utakayekuamini.
Yaani ikiwa MTU Fulani alikuchukua akakupa msaada akakuamini alafu wewe ukamsaliti elewa kuwa nawe utasalitiwa na kuuawa na MTU anayekuamini.
2. HAKI.
Falsafa hii inazungumzia kuua au kuwadhuru ambao hawastahili kudhuriwa. Yaani unamuua MTU ambaye unajua kabisa Hana hatia lakini unamua. Basi elewa kuwa nawe utauawa au damu ya mauaji haitaondoka katika nyumba yako.
Mara nyingi kwenye Mzunguko wako yaani Watu wanaokuzunguka tambua haya kama wewe ni muovu na wao ni waovu elewa kuwa yupo mmoja ambaye anachembechembe za kupenda Haki.
Na huyohuyo ndiye atakayekuua.
Kihistoria, Mauaji mengi ya kisiasa ya Watu wakubwa iwe matajiri au wafalme na viongozi wa kitaifa waliuawa na watu wa karibu mno. Tena waliokuwa wanawashirikisha mambo Yao machafu.
Wengine waliuawa na watoto wao wa kuwazaa kabisa.
Viongozi wajanja mara nyingi wakitaka kufanya mauaji huwaingiza maadui zao kwenye mizengwe na watu wengine ili wauawe na watu wengine ili wao wasichafue mikono Yao Kwa damu.
Wengi hukwepa Laana hiyo isiyofutika wala isiyosameheka.
Yaani Mimi Taikon ninaugomvi na Kiongozi aitwaye Saboka.
Basi Saboka Kwa kutotaka kuchafua mikono yake anachokifanya ni kuangalia kama ninaadui mwingine kama sina basi atatengeneza adui mfano atamtengeneza adui aitwaye Seki.
Seki labda tunaugomvi naye WA kibiashara au tunang'ang'ania demu Fulani.
Saboka atatumia washirika wake kumchochea Seki anidhuru Taikon.
Hivyo ndivyo Watu wanavyoepuka kuchafua mikono Yao.
Alafu muda huohuo kiongozi Saboka Baada ya kusikia nimedhurika au kuuawa, atamkamata Seki na kumuweka ndani Kwa hasira ili watu waone kuwa yeye sio mhusika(kumbe yeye ni mhusika indirect way) na Seki atahukumiwa Kwa mujibu wa sheria za Nchi.
Hapo Saboka atakuwa ametatua tatizo lake pasipo Kupata madhara makubwa.
Kiroho atakuwa na kesi ya Kuchochea na kushinikiza lakini hatakuwa na kosa la mauaji.
Kesi za namna Hii walifanya Watoto wa Yakobo Kwa Yusufu Ndugu Yao.
Mwanzo 37
20Haya, tumuue na kumtupa ndani ya shimo mojawapo. Baadaye tutasema kwamba ameuawa na mnyama wa porini. Halafu tutaona hizo ndoto zake zitakuwaje.” 21Lakini Reubeni aliposikia maneno hayo, akataka kumwokoa mikononi mwao; basi akawaambia ndugu zake, “Tafadhali, tusimuue. 22Msimwage damu. Ila mtumbukizeni katika shimo hili hapa mbugani, lakini msimdhuru.” Alisema hivyo kusudi aweze kumwokoa Yosefu mikononi mwao, na baadaye amrudishe kwa baba yake
Hawa jamaa katika kikao Chao cha mauaji, mmoja wao akakumbuka kuwa kumwaga Damu ya MTU tena Ndugu Yao asiye na kosa. Ni kipengele.
Sasa akatoa hoja ya kumtupa ndani ya shimo ili kesi Yao iwe walimtupa ndani ya shimo lakini hawakumuua. Njaa au wanyama ndio watakaomuua.
Hiyo ni namna ya kukimbia kesi za mauaji. Lakini Reuben yeye alitoa hoja hiyo ili kumuokoa Yusufu baadaye.
"Kikao cha mauaji, Atumiaye upanga atakufa Kwa upanga"
Sheria zinasema USIUE, Sheria za nchi zinasema USIUE.
Ijumaa Kareem!
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam