Kikao cha NEC Zanzibar: Karume hataki kuongezewa muda!


Strange! Kumbe mwenyekiti hapa aliitisha kikao bila kumshirikisha makamu wake ama? Kama ni hivyo, harufu mbaya!

Au makamu alishirikishwa kabla kikao hakijaitishwa, na bado akakaidi akaamua kuitisha cha kwake huko Zenj! Harufu mbaya zaidi!
 


Hapana, CCM haina discipline. Bosi wa chama hawezi kuitisha kikao halafu eti msaidizi wake naye akaitisha kikao kingine tofauti na kile kilichoitishwa na bosi katika muda ule ule kusudi asihudhurie kile kikao kilichoitishwa na bosi. Hii inaonyesha kuwa CCM kuna uhuni sana. Viongozi wanonyeshana mabavu ya nani zaidi kama vile hawana katiba
 
Ninakumbuka kwamba Karume hakuhudhuria sherehe za miaka 48 ya Uhuru, mwezi uliopita. Sherehe hizi zilifanyika Dar es Salaam December 9, 2009. Sasa naamini kabisa kwamba hautaki muungano. Yaani hata kujificha ameshindwa!
 

bosi mwenyewe wa kuheshimiwa yuko wapi
 
Kituko said:
issue ya umeme kwa kweli inawaumiza sana Wazanzibar, hata kama sasa inawapasa kulipia, lakini ukiangalia mikataba mibovu iliyoingiwa na serikali ya Muungano kwa kweli Wazanzibar kama nchi ni kuwatwisha mzigo usiowafaa na usiowahusu

Kituko,

..ninavyoelewa mimi ni kwamba tatizo la umeme Zenj linatokana na kuharibika kwa submarine cable ambayo ni mali ya Zenj siyo mali ya Tanganyika.

..wakati cable hiyo ilipokuwa nzima Zenj walikuwa wananunua umeme kwa bei ya chini kuliko mtumiaji wa umeme wa Tanganyika. vilevile, Zenj walikuwa hawaathiriki kwa mgawo wa umeme kama wanavyo-experience wa-Tanganyika.

..ukosefu wa umeme Zenj umetokana na uzembe wa SMZ, wa-Tanganyika hawahusiki kabisa ktk hilo.


wa-Tanganyika wenzangu,

..chokochoko za kuvunja muungano zingekuwa zinafanywa na wa-Tanganyika sidhani kama baadhi yenu mngekuwa mnatoa kauli za manung'uniko kama mnavyofanya sasa hivi.

..binafsi sioni faida zozote za muungano huu kwa m-Tanganyika wa kawaida. pia wa-Zenj wakiangalia huko tunakokwenda wanaona muungano hautakuwa na faida tena kwao.

.
 
MKUU,
mbona simu yako muda wote imefungwa?
 
Karume ni muongo wa kutupwa....si kweli kwamba hautaki Urais,ana agenda zake za siri na CUF
 
Mkulu FMes, asante sana kwa kutujuza hapa jamvini. Mkuu GS, kama haweki wazi walichongea na Maalim, basi dhahiri kabisa anataka third term!!!

Yetu macho...
 
no niko online. tena kwa sasa niko kwa ofc
piga zote mbili ya ofc na mkononi utanipata.
naomba uni-piemu tena namba zako.nadhani ulinipa wrong numbers!please
 
Edson,

Kwa jinsi mambo yalivyokuwa tangu jana, ni lazima wakina UWT, TISS na wengineo wamejaa humu kama wageni kufikisha hukooo!!!!
 


Naomba nijiquote kwasababu pengine hii point haijaonekana kinachochezwa sasa hivi ni siasa za nani amvishe paka kengele. Karume ashajua akigombana na CCM dodoma atakiona cha mtema kuni kama kilichompata Salmin na Aboud Jumbe. Unategemea mbele ya Msekwa na Mwinyi atasema kuwa hataki Muungano??? I mean come on lazima atakuwa mjinga sana vilevile hawezi kuwaangusha jamaa zake.

Sasa hivi ni kwamba wakija jamaa wataambiwa wamekubaliana nao. Nao nyuma ya mlango wanafanya vengine. Zanzibar karibuni wanapitisha muswada wa mafuta ambao utaipa meno makali SMZ kuhusiana na uchimbaji wa mafuta. Goma hilo linaiva jamaa wanajiandaa kivilivyo.
 
Muungano si ulifanywa na watu 2? Si waweza pia kuvunjwa na watu 2? ama nakosea?

Ulikuwa ni Karume na Nyerere-
Sasa ni Maalim Seif na Karume
 


It is true Karume alichowafanya Msekwa na Mwinyi in kuwaambia thank you for your presence basi asingeonekana na busara kuanza kujibizana na wazee eti nataka third term utausikia moto wake wiki hii kwenye baraza la wawakilishi tega sikio hautaamini.
 
I can't rule out
 
Dili litakalolipa zaidi kwa "King Maker" ndio utakaokuwa "Mwelelekeo wa Taifa" Nani anabisha?

Mkuu jMushi na wengine,

Unaweza kuwa sawa kwa hali ya sasa. Ila kama kweli huyu jamaa ni Iran na huyu General wanayemsema, kuna haja CIA wakaanza kufuatilia hali ya sasa ya Zanzibar. Kama kweli Waarabu wameanza kuyatoa macho kisiwani hapo na ukichukulia kiulinzi hawa jamaa wa Zanzibar wako weak sana, nje ya Muungano watakuwa ni sehemu ya kufanyia majaribio ya silaha. Itakuwa ni kuonyeshana ubabe kati ya Iran na USA.

Kibaya zaidi ni kuwa kama hali hii itatokea basi ni masikini wa kawaida wataumia wakati huo hawa waamuzi na King Maker watakuwa wameshapanda mapipa na kuja kujificha Tanganyika au Kenya au kurudi kwao Uarabuni/Iran.

Nashindwa kuelewa kulala kwa USA hasa ukichukulia kuwa hawa Iran wanayatolea sana mafuta na Uranium ya Tanzania.

Ingelikuwa vema wananchi wakapewa somo la faida na hasara ya Muungano na baada ya hapo, wote tupige na uamuzi ukiamuliwa na wananchi wa Tanganyika au Zanzibar basi Muungano au UVUNJWE au tuendeleze ila kwa kuufanyia marekebisho makubwa.
 
When it's said and done will winner will be: Rostam Abdulrasul Aziz. Mark my words.....!!!
 
zanzibar itashughulikiwa na katiba ya zanzibar na wazanzibari.Au akili yako inakwambia kwamba ile katiba ya zanzibar ni kama gazeti la sani tu? kwamba ipo lakini haina maana yoyote katika jamii?, lawama zimuendee yule alieanzisha muungano wenye sera ya serikali mbili, sidhani kama haya yangetokea kama kungekuwa na serikali tatu katika muungano.waswahili wanasema "mtaka yote, hukosa yote"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…