Mkuu jMushi na wengine,
Unaweza kuwa sawa kwa hali ya sasa. Ila kama kweli huyu jamaa ni Iran na huyu General wanayemsema, kuna haja CIA wakaanza kufuatilia hali ya sasa ya Zanzibar. Kama kweli Waarabu wameanza kuyatoa macho kisiwani hapo na ukichukulia kiulinzi hawa jamaa wa Zanzibar wako weak sana, nje ya Muungano watakuwa ni sehemu ya kufanyia majaribio ya silaha. Itakuwa ni kuonyeshana ubabe kati ya Iran na USA.
Kibaya zaidi ni kuwa kama hali hii itatokea basi ni masikini wa kawaida wataumia wakati huo hawa waamuzi na King Maker watakuwa wameshapanda mapipa na kuja kujificha Tanganyika au Kenya au kurudi kwao Uarabuni/Iran.
Nashindwa kuelewa kulala kwa USA hasa ukichukulia kuwa hawa Iran wanayatolea sana mafuta na Uranium ya Tanzania.
Ingelikuwa vema wananchi wakapewa somo la faida na hasara ya Muungano na baada ya hapo, wote tupige na uamuzi ukiamuliwa na wananchi wa Tanganyika au Zanzibar basi Muungano au UVUNJWE au tuendeleze ila kwa kuufanyia marekebisho makubwa.