Sijui unaongea nini, toka mfumo wa vyama vingi umeingia hapa nchini wapinzani wenye nguvu wamekuwa wakifanyiwa vitimbwi vya kuumizwa na hata kuuwawa. Wamekuwa kila mara wakitaka tume huru ya uchaguzi na kanuni za uchaguzi kuheshimiwa. Hilo halijatekelezwa hadi sasa, kibaya zaidi kila mara wapinzani wa kweli wanabezwa kama mmekubali kushiriki ina maana mmeridhika na mwenendo wa uchaguzi. Sasa hivi unyama unazidi kuwa wazi huku wapinzani wakikutana na vipigo na ukatili mwingi sana. Imefikia mahali hata kura zinahesabiwa na kupigwa bila mawakala wa upinzani kuwepo. Haya yote yanatokea huku taifa zima likiwa kimya na kuonekana ni sawa na hata wasioridhika wameingiwa na woga na hawathubutu kukemea hali hiyo.
Suala la upinzani kushika dola inategemea kanuni za mchezo wa uchaguzi unafanyikaje, iwapo kanuni za mchezo zinakiukwa ili kukibeba chama tawala basi wapinzani nao inabidi waanze kukiuka kanuni za mchezo na hatimaye itakuwa ni mauaji na machafuko, hatuko tayari kufika huko maana sio wote ni wajinga ama wenye uchu wa madaraka. Wewe hapo ulipo mbali ya kujifanya unaona sisi wengine tumekata tamaa hatujakuona ukienda mahakamani kufungua kesi dhidi ya huu ukatili unaofanywa, unaishia kuleta porojo tu hapa. Watu wanaumizwa na kuachiwa vilema vya maisha na sio jukumu la chama kutibu wafuasi wake walioumizwa tena mara nyingine na vyombo vya dola. Tumeona wabunge wa upinzani juzi na wafuasi wao wakidhalilishwa kisa madaraka. Mbona hatukukuona ukienda kutoa msaada wa kisheria mahakamani?
Kibaya zaidi, narudia kibaya zaidi katika mazingira hatarishi ya hivyo mgombea wa upinzani anaweza kufanikiwa kushinda, kisha haipiti muda anajiuzulu eti anakwenda kumuunga mkono rais!! Kama una akili timamu kupiga kura kwenye mwenendo huu ni upuuzi uliopita kiasi. Kama mnataka watu wapige kura ili kuungopea umma na dunia kwamba kuna demokrasia ili kupatiwa misaada basi safari hii mmenoa. Ukitaka nenda na familia yako na wapambe wako, tena mpige picha mkiwa kituo cha kupigia kura mrushe kwenye facebook hakuna anayekuzuia. Sisi wengine maisha yetu hayategemei siasa bali tunapenda siasa safi sio huu ushenzi unaoendelea sasa.